Tofauti kati ya Mashuhuri na Maarufu

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Wana jamvi kwanza niwape pole kwa msiba wa mwenzetu na mpendwa wetu dada Regia Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Pia naomba kujua tofauti iliyopo au zilizopo kati ya Mashuhuri na Maarufu kwani nimeliona hili meno humu Jamvini na nimeshindwa kuzijua tofauti zake.
Karibuni kutofautisha
 
Maarufu ni popular na mashuhuri ni prominent.

Maarufu ni popular kama ma dj, wanamuziki, wacheza mpira, mastaa wa bongo movies, watangazaji wa redio na tv etc. Maarufu ni mtu yoyote ambaye yuko vinywani mwa watu, hata muuza samaki, muuza karanga au hata mwizi maarufu ni popular sio mashuhuri, prominent.

Mashuhuri ni watu wenye kufanya jambo la heshima ya hali ya juu, viongozi, watu kama mawaziri, maraisi wafanya biashara mashuhuri.
 
Thanx mkuu i got something
 
Maarufu ni kujilikana kwa mtu. Unajua Juma ni mtu maarufu sana. Na mara nyingi msimuliwaji sio lazima athibitishe. Mashuhuri inamaana pana sana - heshima, ujuzi, uwezo, kazi - mara nyingi ukitumie neno hilo basi lazima utaje huo umashuhuri wake. Binti juma alikuwa mashuhuri wa utengenezaji chapati.
 
Back
Top Bottom