tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,835
- 18,248
Nampongeza sana mwenyekiti wa kamati ndogo iliyofuatilia na kuchunguza uhalifu uliotendwa wa Operesheni Tokomeza, Mh James Lembeli (Mb), kwa kuanika uozo wote uliotendwa na wahalifu hawa kwa kisingizio cha kusaka majangili.
Hapa ndipo tofauti kati ya Lembeli na Mwakyembe inapoonekana wazi. Mtakumbuka kwamba wakati wa sakata la Richmond kamati ya Mwakyembe ilificha baadi ya ukweli ( kama ilivyodokezwa na Mwakyembe mwenyewe) ili kuisitiri serikali ya CCM. Kama 'kamati tokomeza' ingeongozwa na watu wanafiki kama Mwakyembe sidhani kama ingepata sifa na mafanikio kama hii ya Lembeli.
Tatizo la CCM ni kwamba ina wanafiki na wachumia tumbo wengi kuliko watetezi wa wanyonge. Wapo tayari kutetea chama na matumbo yao kuliko kutetea masilahi ya wananchi.