Ipi tofauti kati ya Paulina Gekul na Salaah wa Silent Ocean?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,079
40,733
- Paulina Gekul na Salaah wa Silent ocean wote ni watu wenye nguvu na ushawishi katika jamii kwa kadiri ya kada zao za kimajukumu.

- Wote ni wana CCM kindaki ndaki

- Wote walijichukulia sheria mkononi kwa wale waliowatuhumu kuwafanyia makosa katika biashara zao. Salaah aliteka vijana wawili, Eliud na mwenzake, na kuwapa mateso makali sana hadi wataje walipopeleka pesa zake. Hakuna hatua aliyochukuliwa, hata tamko tu la polisi, hakuna.

Paulina Gekul, alifanya ukatili wa kumuingizia Chupa kijana Ally Hashim kwa tuhuma za kutaka kumuwekea sumu. Amekamatwa tayari.

Nini tofauti kuu ya hawa wawili, kiasi mmoja anashughulikiwa na mwingine hata kutajwa tu na vyombo vya dola hakutajwa?

Sasa kama mjuavyo, jinai haina expiry date. Sitaki kuingiza udini, na sina nia hiyo. Serikali haipaswi kuwa na double standards, wahalifu wote dhidi ya ubinadamu washughulikiwe. Jinai haina expiry date, nimerudia.

1.) Salaah: Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72
 
Ya saalah unakuta ni dili zao wanacheza kimafia wanazungukana wanaamua kumalizana hivyo hivyo kimafia maana unakuta mtu kweli mzigo kachukua alafu analeta za kuleta
Vipi kuhusu ‘Innocent until proben guilty in a court of law’? , Serikali imeruhusu na kubariki ‘extra Judicial’ torture?

If so then, Why ‘Gekul’ akamatwe kwa kumuingiza chupa makalioni mtu ambaye yeye anaamini alitaka kumuua kwa sumu?
 
Suala la kuuliwa kwa sumu huyo naibu kwa maelezo jinsi nilivyosoma yeye mwenyewe kaambiwa tu hana uhakika nayo
 
Suala la kuuliwa kwa sumu huyo naibu kwa maelezo jinsi nilivyosoma yeye mwenyewe kaambiwa tu hana uhakika nayo
Kwahiyo Serikali imebariki extra judicial torture pale ambapo mtu unakuwa na uhakika juu ya tuhuma alizopewa mtu bila kumfikisha mahakamani? Gekul nae akisema alikuwa na uhakika wa hizo tuhuma, ataachiwa?
 
Kila kitu sio lazima kiandikwe bruh
Mtu mmepeana mizigo mafichoni huko bila ya kufuata taratibu rasmi ikitokea dhuluma mdai aende mahakamani kufanya nini sasa ni kumalizana kimtaa mtaa
Huyo gekul kwa nafasi aliyokuwa nayo na tukio alilofanya kajichanganya mwenyewe
 
Back
Top Bottom