TOC ya Filbert BAYI na TANDAU Yakalia Kuti Kavu, Washindwa kujibu Tuhuma za Ufisadi

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
310
288
RIPOTA PANORAMA
0711 46 49 84

IKIWA ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kutangaza kuitisha mkutano mkubwa wa waandishi wa habari kujibu tuhuma za ufisadi ambazo zimekuwa zikielekezwa zaidi kwa Katibu Mkuu, Filbert Bayi, kamati hiyo imeshindwa kutekeleza azma yake hiyo.

Mapema mwezi Mei, Bayi, Makamu Mwenyekiti wa TOC, Henry Tandau, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji na waandishi wa habari wawili, Cosmas Mlekani wa Gazeti la Serikali la Habari Leo na Imani Makongoro wa Kampuni ya Mwananchi Communition Ltd MCL waliiambia PANORAMA Blog kuwa wataitisha mkutano mkubwa wa waandishi wa habari kujibu maswali ya tuhuma za ufisadi anazoelekezewa Bayi kwa muda mrefu.

Tandau, ambaye aliongoza kikao pili kilichofanyika ofisini kwa Bayi Kibaha na kilichoitishwa na Bayi mwenyewe kwa ajili ya kujibu maswali aliyokuwa ameulizwa na PANORAMA Blog kuhusu tuhuma hizo, alisema maswali yote yaliyoulizwa na PANORAMA pamoja na mengine yatakayojitokeza yatajibiwa katika mkutano huo.

Akisaidiwa na waandishi wa habari Mlekani na Imani, walimkataza Bayi kujibu maswali aliyoulizwa na PANORAMA na badala yake walisema mzigo wa tuhuma za Bayi utabebwa na Tandau, Mlekani, Imani na TOC na waliitaka PANORAMA kumfikishia Bayi maswali yote yaliyosalia inayotaka yajibiwe na kwamba yatajibiwa kwa ufasaha moja baada ya jingine, jambo ambalo hadi sasa TOC imeshindwa kulitekeleza.


Katika Mkutano huo ambao Tandau alitumia muda mwingi kujigamba na kutoa kauli zenye mwelekeo wa kutishia kabla ya kujaribu kuanzisha vurugu kwa kukwapua simu ya kiganjani ya PANORAMA Blog huku akihoji kwa ukali ni kwanini ilimrekodi Bayi katika mahojiano ya kwanza, alitulizwa na misuli imara ya PANORAMA Blog na kuonywa kuwa asifikirie kabisa kuanzisha vrugu ya aina yoyote kwa sababu itadhibitiwa kikamilifu na badala yake ajielekeze kumsaidia Bayi kujibu maswali aliyoulizwa.

SOMA ZAIDI HAPA NDANI , NASHANGAA WAZIRI YUPO KIMYA

Source: Panorama Blog.
 
Back
Top Bottom