TMDA: Ukivuta sigara hadharani faini Tsh. 200,000 au jela miezi 6

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko na atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Tsh. 200,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TMDA, Gloria Matemu aliyasema hayo Aprili 9, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyo kuhusu madhara ya kutumia tumbaku na adhabu zake.

Alisema TMDA imepewa jukumu la kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya sheria namba 121 kuanzia Aprili 30, 2022.

"Ukibainika unavuta tumbaku hadharani au katika mikusanyiko utatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya miezi sita jela," alisema.

Hivyo, aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe na masoko kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara kwa sababu watu wengi wanaathirika kutokana na watu wachache wanaovuta sigara.

Matemu alisema TMDA imefanya kampeni ya siku tano ya kutembelea kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vituo vya mabasi na masoko, ili kuwaelimisha kuhusu madhara na namna sheria inavyofanya kazi.

Alisema kampeni hiyo imesaidia kufikisha elimu kwa wakazi wa Manispaa ya llala na lengo kuu ni kuwafikia Watanzania wote wafahamu kuhusu jukumu hilo la TMDA katika kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kupunguza madhara yatokanayo na uvutaji huo.

Mkaguzi wa TMDA, Kanda ya Mashariki, Jafari Tolo alisema takwa la sheria ni kuzuia uvutaji wa sigara kwenye mikusanyiko ya watu na wamiliki wa maeneo yanayokusanya maeneo maalum ya wanaovuta kuvuta bila kuathiri wasiovuta.

Alisema pia maeneo yenye mikusanyiko kunapaswa kufungwa vifaa vya kubaini endapo kuna mtu anavuta sigara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Ofisa Afya wa Soko la Kisutu, Aron Matei aliishukuru TMDA kwa elimu waliyotoa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu uvutaji wa sigara katika maeneo yasiyo rasmi.

Source: Nipashe
 
Sasa hivi kila sekta inajitolea kauli tu na kiasi cha fine.

Sasa hapa baada ya hii kauli washamwaga nguvu kazi, utaona mipuuzi iliyopauka mwili na viatu vilivyojaa vumbi na kuisha upande mmoja inafuatilia watu nyuma nyuma kama fisi anavizia mifupa kubambikia vipisi vya sigara na kutaka hongo.
 
Lile tamko la kuzuia watu kuuza bidhaa kwenye vyombo vya usafiri limeishia wapi? Naona Bado wanauza Dawa nk.
Hata wahubiri kwenye mabasi na kukusanya sadaka wamerudi!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko na atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TMDA, Gloria Matemu aliyasema hayo Aprili 9, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyo kuhusu madhara ya kutumia tumbaku na adhabu zake.

Alisema TMDA imepewa jukumu la kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya sheria namba 121 kuanzia Aprili 30, 2022.

"Ukibainika unavuta tumbaku hadharani au katika mikusanyiko utatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya miezi sita jela," alisema.

Hivyo, aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe na masoko kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara kwa sababu watu wengi wanaathirika kutokana na watu wachache wanaovuta sigara.

Matemu alisema TMDA imefanya kampeni ya siku tano ya kutembelea kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vituo vya mabasi na masoko, ili kuwaelimisha kuhusu madhara na namna sheria inavyofanya kazi.

Alisema kampeni hiyo imesaidia kufikisha elimu kwa wakazi wa Manispaa ya llala na lengo kuu ni kuwafikia Watanzania wote wafahamu kuhusu jukumu hilo la TMDA katika kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kupunguza madhara yatokanayo na uvutaji huo.

Mkaguzi wa TMDA, Kanda ya Mashariki, Jafari Tolo alisema takwa la sheria ni kuzuia uvutaji wa sigara kwenye mikusanyiko ya watu na wamiliki wa maeneo yanayokusanya maeneo maalum ya wanaovuta kuvuta bila kuathiri wasiovuta.

Alisema pia maeneo yenye mikusanyiko kunapaswa kufungwa vifaa vya kubaini endapo kuna mtu anavuta sigara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Ofisa Afya wa Soko la Kisutu, Aron Matei aliishukuru TMDA kwa elimu waliyotoa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu uvutaji wa sigara katika maeneo yasiyo rasmi.

Source: Nipashe
Yaani sasa wavutaji sigara wazivute kwa kificho? Hebu watueleze ni sehemu zipi ambazo sigara zinaruhusiwa kuvutwa au maeneo rasmi kwa uvutaji wa sigara ni yepi?
 
Hili tamko kwakweli sio poa kabisa kwa sisi wadau. Sasa ninunue fegi af nitafute chaka nikajifiche? Hivi wanajua alosto kweli?
Hapa ni harakati za kuacha tu
 
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko na atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Tsh. 200,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TMDA, Gloria Matemu aliyasema hayo Aprili 9, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyo kuhusu madhara ya kutumia tumbaku na adhabu zake.

Alisema TMDA imepewa jukumu la kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya sheria namba 121 kuanzia Aprili 30, 2022.

"Ukibainika unavuta tumbaku hadharani au katika mikusanyiko utatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya miezi sita jela," alisema.

Hivyo, aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe na masoko kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara kwa sababu watu wengi wanaathirika kutokana na watu wachache wanaovuta sigara.

Matemu alisema TMDA imefanya kampeni ya siku tano ya kutembelea kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vituo vya mabasi na masoko, ili kuwaelimisha kuhusu madhara na namna sheria inavyofanya kazi.

Alisema kampeni hiyo imesaidia kufikisha elimu kwa wakazi wa Manispaa ya llala na lengo kuu ni kuwafikia Watanzania wote wafahamu kuhusu jukumu hilo la TMDA katika kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kupunguza madhara yatokanayo na uvutaji huo.

Mkaguzi wa TMDA, Kanda ya Mashariki, Jafari Tolo alisema takwa la sheria ni kuzuia uvutaji wa sigara kwenye mikusanyiko ya watu na wamiliki wa maeneo yanayokusanya maeneo maalum ya wanaovuta kuvuta bila kuathiri wasiovuta.

Alisema pia maeneo yenye mikusanyiko kunapaswa kufungwa vifaa vya kubaini endapo kuna mtu anavuta sigara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Ofisa Afya wa Soko la Kisutu, Aron Matei aliishukuru TMDA kwa elimu waliyotoa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu uvutaji wa sigara katika maeneo yasiyo rasmi.

Source: Nipashe

Dawa ni msiuze sigara
 
Nilishasema toka awali, hawa watu wapewe na leseni, na masharti yawe ya leseni ni kwamba usivute hadharani
 
UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO

ila still zinatengenezwa mi hii kauli huwa siielew kabsa
 
Hawa ndio wahujumu uchumi…Bangi kosa la jinai,sigara kifungo …alafu ukizingatia wanapambana na vitu amabavyo si dhambi kwa dini yeyote
 
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema ni kosa kisheria kuvuta sigara hadharani au kwenye maeneo ya mikusanyiko na atakayebainika kufanya hivyo atatozwa faini ya Tsh. 200,000 au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi sita jela.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TMDA, Gloria Matemu aliyasema hayo Aprili 9, 2022 katika Soko Kuu la Kariakoo, wakati wa kampeni ya kutoa elimu katika maeneo ya mikusanyo kuhusu madhara ya kutumia tumbaku na adhabu zake.

Alisema TMDA imepewa jukumu la kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa lengo la kutoa elimu kuhusu matakwa ya sheria namba 121 kuanzia Aprili 30, 2022.

"Ukibainika unavuta tumbaku hadharani au katika mikusanyiko utatozwa faini ya Sh 200,000 au kutumikia adhabu ya miezi sita jela," alisema.

Hivyo, aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe na masoko kutenga maeneo maalum ya kuvutia sigara kwa sababu watu wengi wanaathirika kutokana na watu wachache wanaovuta sigara.

Matemu alisema TMDA imefanya kampeni ya siku tano ya kutembelea kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu kama vituo vya mabasi na masoko, ili kuwaelimisha kuhusu madhara na namna sheria inavyofanya kazi.

Alisema kampeni hiyo imesaidia kufikisha elimu kwa wakazi wa Manispaa ya llala na lengo kuu ni kuwafikia Watanzania wote wafahamu kuhusu jukumu hilo la TMDA katika kudhibiti matumizi ya tumbaku ili kupunguza madhara yatokanayo na uvutaji huo.

Mkaguzi wa TMDA, Kanda ya Mashariki, Jafari Tolo alisema takwa la sheria ni kuzuia uvutaji wa sigara kwenye mikusanyiko ya watu na wamiliki wa maeneo yanayokusanya maeneo maalum ya wanaovuta kuvuta bila kuathiri wasiovuta.

Alisema pia maeneo yenye mikusanyiko kunapaswa kufungwa vifaa vya kubaini endapo kuna mtu anavuta sigara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Ofisa Afya wa Soko la Kisutu, Aron Matei aliishukuru TMDA kwa elimu waliyotoa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu uvutaji wa sigara katika maeneo yasiyo rasmi.

Source: Nipashe
Chanzo kizuri cha mapato
 
Wakavutie wapi?

Wajenge sehemu ZA kuvutia
 
Back
Top Bottom