kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,613
Mashindano ni mengi sana kwa wachezaji walewale. Ligi, FA, CECAFA, Caf champions, AFCON na mechi za kirafiki zote hizi ni muhimu na zina uwezo wa kuzalisha majeruhi kwenye timu yako. Haya mashindano ya Mapinduzi ni muhimu sana kisiasa lakini ratiba yake inaning'inia tu na malengo yake ni hadi uvae miwani kali kuyaona.
Naipongeza Yanga kupeleka kikosi kile kwenye mashindano yale yaliyozaliza majeruhi kwa Okrah, Lomalisa, na Skudu tayari ambayo haijulikani watapona lini ili wacheze ligi na caf champions. Wachezaji wa timu ndogo kwenye mashindano yoyote kama Mapinduzi huwa wanacheza kwa kukamia timu kubwa ili kuonyesha uwezo na kushawishi kusajiliwa na timu kubwa, tabia ambayo inazalisha majeraha mengi sana kwa timu na wachezaji wa timu kubwa. Mfano, mchezaji alimrukia Okrah kutoka kusikojulikana na kumuumiza vibaya bila sababu ya maana.
Ni mashindano mazuri kwa timu kubwa kupeleka wachezaji wasiopata game time kwenye ligi na machindano mengine ya TFF, CECAFA, na CAF na timu ya taifa ili kuwapasha moto lakini sio lazima kwenda kushinda kombe. Timu itakayoshiriki kombe la mapinduzi mechi zote hadi finali itarudi kwenye ligi na mashindano mengine ikiwa dhaifu sana.