kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,316
- 12,614
Wazanzibar wana akili nyingi sana kuliko wale wenzao wa kuleee. Baada ya kuua ligi ya muungano baadae wakagundua kuwa walikosea. Ligi ya muungano ilikuwa sehemu ya wazi ya kuviona vipaji kutoka Zanzibar na kuvisajili kwenye timu za bara (ajira).
Baada ya walevi na ulevi wao wa kuuchukia muungano kuwapanda vichwani na kujitoa kwenye ligi ya Muungano na kuona hasara yao sasa wameirudisha ligi kuu kwa mlango wa nyuma kwa lengo la kuwatafutia masoko vijana wao.
Ukweli ni kwamba mashindano ya Mapinduzi ni mazuri sana lakini ni sehemu kamili ya kuwachosha, kuwaumiza wachezaji na kuzalisha majeruhi wengi wa timu za bara kutokana na ratiba ya mashindano kuwa mbaya, yaani unalazimika kucheza mechi kila baada ya siku moja.
Kama ligi ya muungano ni muhimu basi taratibu zote zifanywe kuirudisha rasmi ligi inayojumuisha timu za bara na visiwani kama zamani kuliko ratiba finyu kama hii, VINGINEVYO NI SAHIHI TIMU ZA BARA KUTUMIA VIKOSI B VYA TIMU ZAO.
Mfano, huwezi kujua kwanini yule mchezaji alimrukia Okrah bila sababu za msingi.
View: https://www.youtube.com/watch?v=g1zrIjZwcj0