Timu ya zamani ya Okwi yatwaa ubingwa wa CAF Confederations Cup

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Timu ambayo aliwahi kupita "Nguli" toka nchini Uganda.. Emanuel Anord Okwi katika safari yake ya kuelekea Europe.. Etoile Du Sahel.. siku ya leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa CAF Confederations Cup.
Hii ni baada ya kuichapa bila huruma Orlando Pirates kwa jumla ya Goli 2-1.

Safari ya Etoile katika kubeba ndoo ilikua hivi..

1448818865814.jpg

NOTE: Etoile Du Sahel ndiyo waliozima ndoto za Wazee Wakimataifa kutakata kimataifa.
Hongereni Etoile Du Sahel.
 
Kipindi timu yake ya zamani ikibeba ndoo ya Shirikisho leo.. "CR7 wa Uganda" aliingia kipindi cha Pili na kuiwezesha timu yake ya SonderjyskE kuibuka na ushindi wa Goli 2-0.
Hii imeifanya kuchupa hadi nafasi ya 4 katika msimamo wa SuperLiga huku ikizidiwa point 4 tu na anayeongoza ligi.

Lazima wazungu watakuelewa tuu.. Kila la kheri Emma.
 
Unamuitaje huyo Kwio!!! CR 7 wa Uganda!!!!

Mkuu hilo jina sijampa Mimi.. Kambatiza Kocha bora kabisa aliyewahi kuifundisha Yanga, ambaye sasa anafundisha timu ya Taifa ya Uganda.. Mtalamu Milutin Micho
Sredojevic
.. Namnukuu..

"He is more than capable of doing it on permanent basis. He is for me Ugandan version of Cristiano Ronaldo but difference is that other one is doing on permanent basis scoring."

Nami naungana na Mtalamu Micho kwa asilimia 100.

Source: http://www.kawowo.com/index.php/foo...andan-version-of-cristiano-ronaldo-micho.html
 
Al ahly alimtoa Yanga akabeba ubingwa

Zamaleki alimtoa Yanga akabeba ubingwa

Etoil du sahel alimtoa Yanga kachukua ubingwa

Je kunani Yang?

Ni daraja la kwenda kumchukua mwali.
 
Timu ambayo aliwahi kupita "Nguli" toka nchini Uganda.. Emanuel Anord Okwi katika safari yake ya kuelekea Europe.. Etoile Du Sahel.. siku ya leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa CAF Confederations Cup.
Hii ni baada ya kuichapa bila huruma Orlando Pirates kwa jumla ya Goli 2-1.

Safari ya Etoile katika kubeba ndoo ilikua hivi..

View attachment 308260

NOTE: Etoile Du Sahel ndiyo waliozima ndoto za Wazee Wakimataifa kutakata kimataifa.
Hongereni Etoile Du Sahel.

Asante sana Mkuu sembo kwa taarifa hii na kukiri kuwa Young Africans SC ilitolewa na Bingwa wa michuano hiyo:

NB: Etoile du Sahel waliitoa Yanga kwa taabu sana, hapo umeshaelewa Yanga ni timu ya namna gani:

LIVE KUTOKA TUNISIA (FULL TIME...BALL POSSESSION etoile 51% yanga 49%): ETOILE DU SAHEL 1 VS YANGA 0 - SALEH JEMBE
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Ni daraja la kwenda kumchukua mwali.

Kuna kikombe kinasubiriwa Yanga maana bila kukutana na hao wababe, Yanga angekuwa bingwa! Kumbuka wote hao wanaufahamu vizuri mziki wa Yanga, waulize watakuambia timu pekee iliyowakosesha raha katika michuano hiyo si nyingine bali ni Young Africans SC ya Tanzania.
 
Nadhani timu iliyowafanya wasilale.. Wakeshe kila siku uwanjani ni Zamalek.

Maana wakiwa mguu mmoja washaungiza katika fainali [wakiwa nusu fainali].. walitandikwa 3-0 wakiwa ugenini na Zamalek.

Walirudi kwao wakiwa vichwa chini.. Wakaumiza vichwa sana wafanyaje ili waweze kuingia fainali.. Wakapiga mazoezi ya kutosha.

Walipokuja Zamalek kifua mbele na ushindi wao wa Goli 3-0,.. waligongwa 5-1 kama wamesimama.

Matokeo yake jamaa wakafuzu kwa ushindi wa goli 5-1.
 
Kuna kikombe kinasubiriwa Yanga maana bila kukutana na hao wababe, Yanga angekuwa bingwa! Kumbuka wote hao wanaufahamu vizuri mziki wa Yanga, waulize watakuambia timu pekee iliyowakosesha raha katika michuano hiyo si nyingine bali ni Young Africans SC ya Tanzania.

Tunaomba link ya hayo yaliyosemwa mkuu kama ushahidi =
 
Back
Top Bottom