Timu ya kampeni ya Dr. Magufuli yasambaratika

Nimeambiwa kuwa ile ya kampeni ya CCM iliyoundwa kwa kumsaidia Dr. Magufuli na Mama Samia imesambaratika jana usiku baada ya kikao cha kimkakati. Nimearifiwa na mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kuwa kusambaratika kwa timu hiyo kunatokana na sababu mbalimbali. Wapo wajumbe waliosusa baada ya kuona wananchi hawaelewi somo la CCM na kuielewa Ilani. Wananchi wamekuwa hawaelewi wanachoambiwa na sasa wajumbe wanaishiwa cha kusema.

Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa wanatuhumiana, na hata na Dr. Magufuli mwenyewe, kuwa ni popo wa kisiasa. Wanaunga mkono harakati za wapinzani kwa kificho na kumharibia Dr. Magufuli majukwaani kwa kutamka maneno ya kukwaza na kukera yanayochochea hasira za wananchi dhidi ya wagombea wa CCM wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.

Wapo wajumbe waliosusa kutokana na kutotimiziwa matakwa yao hasa ya malipo kwa kila siku wanayoifanyia kazi. Wajumbe hao wamesema kuwa hawana muda wa kusubiri kulipwa baadaye kwakuwa uchaguzi ni bahati nasibu na lolote laweza kutokea. Wanasisitiza kulipwa marupurupu yao sasa kwa mujibu wa makubaliano ya kichama na kutoahidiwa kulipwa baada ya uchaguzi.

Wapo wajumbe waliosusa kwakuwa hawapewi uzito na umaarufu kama ilivyotarajiwa. Wanamlaumu Dr. Magufuli na viongozi waandamizi chamani, kwa mfano, kumuamini sana Abdallah Bulembo ambaye hana hadhi kichama, kisera na kihela kupewa nafasi ya kutawala majukwaa kama afanyavyo sasa. Wanalalama kuwa watu maarufu wamewekwa kando na sasa wanaanza kuota utando.

Sasa timu imesambaratika. Dr. Magufuli yuko njiapanda kikampeni. Itambidi kupambana kiume ili kuendelea kujieleza mbele ya wananchi. Apambane kivyake sasa na watakaobaki naye!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kwa sasa tunaomba tukuaminj maana hata magufuli mwenyewe alitoa kauli juzi kuwa kuna watu wanamhujumu,wanakula CCM wanalala Ukawa!
 
Uliyoandika yote ni ya kweli ila huna tofauti na TWAWEZA.....FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE.
 
Hahaha upinzan naona mmeishiwa na bado tare25 ad mtakimbia jamvin .angalia mktano wa geita sasa iv c mafuliko c sunami nizaid ya sunami .kamat tendaj ya kampen yote ipo na inafanya kaz so peleka hiyo hoja hko ukawaaaaaa
 
Labda aongeze na team ya wanamazoezi ili wawe wanapiga pushup pamoja. Naona kama watavutia pia!!!!!!!!!!!!!!!

Halafu, ushauri wangu wa pili, wapite kila nyumba wakigawa kila mpiga kura zile billion 13 walizowagawia wale waliofika bei ili kuhakikisha Watanzania wote wahanga wa ccm wanafika bei.

Kinyume cha pale, wahakikishe wanayo mataulo ya kutosha kujifutia machozi!

Mi nafikiri wamchukue Francis Cheka, wawe wanapiga boxing jukwaani. Au awe anaenda kucheza soka kabisa.
 
VUTA-NKUVUTE wakati nyie mnaandaa riport za J.makamba na TWAWEZA ....jua mamvi kuna kitu anawaaandalia.....anajua michezo sana.

Yawezekana nyie mnaandaa siries nzuri...ila mnai-release sio katika muda muafaka...mamvi atatoa siries, ambayo iakuwa katika muda muafaka.

Siries yenyewe inaweza kuwa kama 24 live another day

Loading.............................................22% (kwa mujibu wa TWAWEZA)
 
[h=2]MAGUFULI ATINGA MKOANI GEITA[/h]

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mnadani, mkoani Geita.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakiwapungia mkono maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya ya Viwanda, pia katika serikali yake itaongeza maeneo ya wachimbaji wadogo na kuwawezesha ili waweze kuchimba vizuri.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Umati wa wakazi wa Katoro ukifuatilia mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli.
 
Hahaha upinzan naona mmeishiwa na bado tare25 ad mtakimbia jamvin .angalia mktano wa geita sasa iv c mafuliko c sunami nizaid ya sunami .kamat tendaj ya kampen yote ipo na inafanya kaz so peleka hiyo hoja hko ukawaaaaaa
Kampeni za chadema tunawaona sumaye na hiza ambao hata haijulikani ni wa chama gani wakati chadema wenyewe wamefukuzwa na mmiliki mpya lakini hilo hawataki kuliangalia. Kweli nyani hata kundule likiachia valve na uharo kupita ovyo, hawezi kuliona.
 
Kumbuka team INA watu 30!
Magufuli mwenyewe anauzito kuliko hata ccm kama chama! Kumbuka JPM ni jeshi la mtu mmoja!

Na hata ukiiombea mabaya team Magufuli unajichosha tu! Kumbuka....
Tembo hata akikonda vipi hawi kama mbuzi!
Team ina watu wengi tu kina Diamond Platinum, kina Wema Yamoto bendi tena waende zao.
 
Back
Top Bottom