Timu ya FIFA ina kasoro, je ya UEFA?


Suala la kukaa na mpira Toure hana pindi alipokuwa Barca ila uwezo wake ulishuka baada ya Pep kumsugua Bench, ukiniambia Pirlo anakaa na mpira muda mrefu hapo mimi sitakupinga hata kidogo Mkuu. Hv Leo hii Toure Yaya akirudi unafikir Sergio B anapata namba pale Barca?
 
inaelekea umeanza kutazama mpira siku za karibuni
 
Sababu ya XAVI kutochezeshwa muda mchache umri wake ni mkubwa ni wanajiandaa kuwapa nafasi warithi wake kina Cesc/Thiago.Iniesta anajulikana ni majeruhi sana ,mara nyingi anaumia sana unapocheza na timu zinazotumia mpira wa nguvu Alonso ni better option ndio maana Barca wanapata tabu sana wakicheza na Chelsea na another advantage Alonso anafunga magoli huwezi mlinganisha na Sergio.Hizi clip za You tube wanachagua only the best hata ukitafuta clip za Diaby utasema ni bonge la mchezaji kumbe hamna kitu
 
Nyie mambo ya ulaya yanawahusu nini?Na nyie tangazeni kikosi chenu bora cha dunia akikosekana Kaseja nyie magumashi.:blabla:
 
Pole sana.
 
Tatizo nimekusoma wewe ligi ya Spain unaangalia el clasico tu,sitashangaa maana wengi wenu wafuatiliaji ligi ya England wachezaji na makocha wa timu zote za England mnawajua,ila Barca utasikia watu wanawajua Messi,Iniesta na Xavi,ndio maana ngumu kwenu kujua na kutambua umuhimu wa mchezaji kama Sergio Busquets,kocha Del Bosque mwenzio kashasema anatamani acheze kama Sergio Busquets,ndio maana hata Cazorla wengi wenu wanazi wa England mmemjua alipokuja Arsenal,Spain kuna wachezaji wengi wazuri,punguzeni kuamini kila the sun ikisema,utasikia Rooney mchezaji bora duniani kisa kafunga bao la tik taka,na hata Busquets nadhani sidhani kama hata unajua kama kishafunga mabao mangapi ktk la liga maana haufutilii si ajabu ukasema hajafunga,na nikikuuliza nani ana mabao mengi msimu huu yeye na Alonso si ajabu ukasema Alonso huku ukikumbuka mabao ya long range aliyofunga akiwa Liverpool,kwa sasa sidhani kama hata utakuwa unajua data za Alonso ktk la liga si ajabu umeona mechi labda real madrid vs barca,ndio nimenoti wengi wenu ligi ya England mnafutilia sana kuliko Spain,ila ni 7bu ndio tawala letu mazingira wengi walipo ni ligi ya England tofauti na mimi wa kazimzumbwi ni la liga kwenda mbele hata rayo vallecano wakiongozwa na Piti vs Real Valladolid ya Manucho sikosi ndio ligi inayoonyeshwa kwetu huku kazimzumbwi,karibu leo Real Sociadad wakina Xabier Prieto na Carlos Vela wapo uwanja wao Anoeta jijini San Sebastian(kwa kina Alonso na Arteta) vs FC Barcelona usikose kuona hii mechi utajiona mengi na utagundua na kunielewa nini nasema kuliko kusubiri results na highlights za sky news ambazo hata Busquets akifunga goli huwezi kujua maana hawatazungumzia zaidi ya Messi 7bu ni anaweka rekodi na anauza magazeti huko ya The Sun ndio maana siku hizi narindima hadi makombe ya mbuzi yanayotekea Spain sio mpaka ikifika el clsico ndio wengi wanakuwa atensheni.
 
wewe nikuache hujui unachoongea,kawaulize kina Mascherano,Keita na Song,Busquets ni kiungo anajua kucheza namba yake na anasaidia sana tofauti na mnavyongoja nyie mpaka sky news sport imsifie mchezaji ndio mnaona kifaa,Cazorla wengi wenu nyie mmemjua yupo Aseno,angalia la liga sio mpk el clasico real madrid vs barca,ndio maana wengi wenu Barca mnawajua wachezaji hata 5 hawafiki ila sema spurs au hata norwich kuanzia kocha wao aliefanana na Obama hadi wachezaji wa akiba,Toure bado ndio mana Ivory Coast inahangaika haina kiungo mkabaji mzuri wote wakaa na mpira,sasa unakuta wa2 wengi miaka yote wanaipa nafasi ivory Coast kufika mbali world cup au kubeba kombe la afrika 7bu kama alivyoimba afande Sele mnatajataja majina tu kwa mistari isiyo na vina,mimi binafsi na uhakika Toure ni mzuri kwa kuwa mchezeshaji kama kina Iniesta ila kiukabaji hamfikii Busquets ambae ni mchezaji wengi wenu mnadai hajui chenga na hamjawahi kumuona akiwa anapiga pasi za visigino ambazo mpira wa chenga sio sana kwake na anajua sema kwa kuwa wengi wenu mpaka msubiri Barca vs Real Madrid huku mpira mzima mkiangalia wachezaji wawili tu Messi na Ronaldo mnakuwa hamumko makini kuangalia wengine ndio mnakuwa hamumjui na wengine hawamjui kabisa Busquets,ndio tatizo makocha na watu wengi wa dunia ya tatu wachezaji wakipiga chenga wanajua huku hakabi,yaani hata kama anaringa atabembelezwa kisa ana mpira wa kupiga kanzu na tobo,ndio inawaponza wachezaji wengi wa South America ambao kocha kama Ferguson wengi hawapi namba eg Anderson au hata Veron alipouzwa wakati ule au hata Djembadjemba na mpira wake wa kugeukageuka kama anacheza ndombolo,Spain ya zamani ilikuwa na wakaa na mpira kina Mendieta,Luis Enrique wakabaji haina ndio mana unakuta chenga nyingi wanafungwa na kutolewa na hata Korea Kusini ila sasa kuja kwa kina Busquets sasa hivi ni ushindi kwenda mbele na rekodi kibao si Barcelona hadi Spain,yaani sasa Barca hata wakikusajili wewe uwe mbele unavizia kila siku unacheka na nyavu tu.
 
sasa kama mnalijua hilo mbona mnalalamika listi ina upendeleo Spain watupu?mimi binafsi namkubali Alonso,ila kwa Busquets anasubiri,Busquets ni kiungo anaekaba kiakili na hana rafu kama Alonso na hata Mascherano ni mzuri sema rafu ndizo zinamuharibia cv tofauti na Busquets.sasa kama umejijibu zote barca msimu huu wameshinda kasoro moja hakuwepo wamefungwa,karibu Barcelona nakukaribisha sana na La furia roja,najua umekaribia baada ya kuwa mabingwa eoro 2012 au world cup 2010
 

Udhaifu wa S. Busquets ni kupenda kujiangushaangusha sana nadhani hilo linamwaribia CV yake....:becky:
 
Nyie mambo ya ulaya yanawahusu nini?Na nyie tangazeni kikosi chenu bora cha dunia akikosekana Kaseja nyie magumashi.:blabla:
ina ukweli ndani yake,ila yaani wenye nchi yao Spain+mimi chini ya coach 1st marques of Bosque Vicente Del Bosque Gonzalez wakipanga listi kwanza jezi anapewa Sergio Busquets i Burgos then wengine wanafuatia.
 
Mkuu, mi huwa nahudhuria mechi uwanjani...:smiling:
Lete risiti mechi gani kajiangusha S Busquets zaidi utasema ile ya Inter Milan semi final uefa 2010 kwa Thiago Motta,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,mkitaka mpende au mchukieni ila mpira anajua na mchezaji bora mkabaji kwa sasa Duniani.
 

kaka naomba nikukosoe,kwani watu wamelalamika kutokuwepo wachezaji wa epl au kuwepo kwa wachezaji wa la liga tu? pia kwa hiyo hujaona tofauti hiyo ya fifa na ya uefa?hiyo ya uefa ni bora zaidi kwangu mimi,angalia inatoa sura ya timu ya ulaya ligi 3 zipo humo!ile ya fifa haina hadhi ya kuitwa timu ya dunia bali kombaini ya real madrid na barcelona with the exceptional of falcao!
 
Duh! kaka umenifurahisha kwelikweli, watangazaji wetu huona fahari kutamka kwa ufasaha majina tu ya timu za England kana kwamba wanafanya usaili, lakini majina ya timu za Spain, Germany (wakoloni wetu), Italia n.k. hawawezi kabisaaaaaaaaaaaaaaa.
 
You wish!
Mambo ya kuangalia match vibandan hayo, kanunue decoder yako Multchoice uone the difference tena make sure ni PVR, sio kuleta siasa hapa!
Muda nilioanza kuangalia mpira hao supersport walikuwa hata hawajaingia ndio maana nakwambia umeanza kuangalia mpira juzi juzi mimi timu yangu Milan unajua nilianza kuiona wapi pia jiulize pamoja na Liverpool haifanyi vizuri kwanini bado ina wapenzi wengi Tanzania wote hao walianza kuishabikia Liverpool wakati ambao supersport walikuwa hawajafika na wala hawategemei kufika kutokana na mahusiano yetu ya wakati ule wewe uliyeanza kuangalia juzi juzi ndio ukahangaike vibandani
 


Wacha wee!
Sasa ilikua unalialia nini eti "tatizo ni supersport wanapromote EPL ndo maana huoni ligi nyingine"
Kama ulikua unaangalia hiyo liverfool yako b4 supersport haijaja bongo sioni sababu ya wewe kuilalamikia Supersport, ungeendelea na utaratibu wako wa zamani.

Its clear kwamba unabananaga vibandani huko ndo maana unajichanganya hapa.
Asshoe!
 
Hao wachambuzi wa soka kwenye radio zetu (wanaocopy/paste watangazaji wa SS) wangekuwa na ufahamu kidogo tu wa hilo ulilonena tungefurahi. Mie siwalaumu sana DSTV kwani wao wanafanya biashara, wanakuja nchini mwako na kukuta ligi ya kwako haioneshwi na local TV yoyote na kukuletea hiyo EPL kwanza, wakiona umeisha iva sasa ndio wanakupa uhuru wa kuchagua kuona ligi nyingine. Hujiuliza hapa barani Africa hakuna club champions leaugue!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…