Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,742
- 107,055
- Thread starter
- #361
Mkuu unanishawishi niongelee kitu kinachoitwa Multi Universe.. sema nikiongea hapa tutazidi kuachana gizani. Matukio ya hvyo kuhusu picha zinapigwa afu intakea jambo lisilo la kawaida kwenye picha nadhani yako mengi.. baadhi yameelezwa kwenye nyuzi humu. Naomba tu siku Time Travelling ikiwa possible watu wote waliosoma uzi huu wawe haiKuna documentary flani niliangalia youtube wanaongelea Time Travellers.
Kuna picha ambayo ilipigwa miaka ya 1980's ukumbini kwenye pambano la Tyson. Kwenye ile picha inaonekana jamaa amevaa miwani ya toleo la miaka ya 2010's
picha nyingine imepigwa mwaka 1926 London uzinduzi wa daraja, kwenye hiyo picha akaonekana jamaa amevaa Tshirt inayobana mwili na ina logo kifuani ya miaka ya sasa hivi.
Kuna video ya charlie champlin yule alikuwa muigizaji mashukuru wa vichekesho ile video ilirekodiwa miaka 1920's cha kustajaabisha kwenye hiyo video anaonekana dada ameshika simu ya kufunua wakati kipindi hicho kulikuwa hamna simu za kigachani.
Kwahiyo kuna binadamu ambao wanasafiri kurudi nyuma na kwenda mbele. Mtu anaweza kutoka mwaka 2060 akaja mwaka 2019 kuangalia show ya Jay z akasepa zake.
Swali linabaki kama kweli hii kitu ipo wanasafirije?
kama ni kifo sidhani yaani mtu anakufa 2019 anazaliwa tena 2060 au vice versa duh labda kama mtu anakufa sayari hii anaenda kuzaliwa sayari nyingine hahahaha
Pia naamini kabisa kwamba binadamu hatupo wenyewe kwenye ulimwengu huu naamini kabisa kuna solar system nyingi, dunia kibao ulimwenguni watu wanaishi kama sisi tunavyoishi.
NASA walitoa waraka kwamba kwenye vyombo vyao wanaona sayari zinazofanana na dunia ila kufika huko chombo kitachukua miaka milioni 20