Time Travel: Je, linaweza kuwa suluhisho la kifo?

Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
SALUTE
Mara nyingi huwa nasema vitu tunavyoona ni vya kijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio huwa na maana na vimeleta mabadiliko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha, hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana.

Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini?
Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)

TIME MACHINE
Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kuwa hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona, kuambiwa au viliwahi kuwepo.

Utawaza Mungu kwakuwa ulisikia kuwa kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web.

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labda kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
Kuna haka kastory niliakandika kitambo kidogo ngoja nikaweke hapa ili tusijaze server za watu. Haka kastori kanahusu viumbe wanaokuja duniani kutoka anga za mbali kuja kututembelea. Sometime waweza jiuliza tu kwanini Roman Catholic ilibadili sala ya Mwanakondo uondoae dhambi za dunia kuwa mwanakondoo uondoae dhambi za ulimwengu! ni kwasababu Teknoljia inazidi kukua pia elimu yazidi kupanuka hivyo wakajua tu haiwezekani katika Galaxy yetu ya Milky way yenye solar system zaidi ya 1mil kuwe na binaadamu/viumbe duniani tu. Kastory kenyewe ni haka.

Ilikua July 1954 ambapo maofisa wa wa uwanja wa Haneda Airport (kwasasa Tokyo Airport) nchini Japan waliripoti tukio la kushangaza lilitokea uwanjani hapo. Msafiri kutoka Ulaya mwenye pasi ya kusafiria ya nchi iliyokua inaitwa Tuared.

Msafiri huyo alikua na mwonekano mwenye ndevu kiasi na mwonekano wa Caucusian kama watu wanaotoka nchi za Ulaya, kwa mujibu wake alisema kua nchi hiyo ya Tuared iko Ulaya pia alikuwa ana fedha za mataifa mbalimbali. Maofisa wa polisi walifikiraia kua watakua na maelezo kidogo tu kuhusu kwanini hawajui nchi hiyo ilipo hivyo wakaamua kumpelekea chemba kwa mahojiano zaidi. Walipoanza kumuuliza taarifa ili wapate kuifahamu hio nchi ilipo. yule msafiri alianza kuwa mkali na kusema kuwa hiyo ilikua safari yake ya tatu hapo nchini Japan kwa safari za kampuni anayofanyia kazi, pia amekua akifanya safari nchini humu kwa muda wa miaka mitano iliyopita.

Msafiri alishangaa kwanini maofisa wanachelewa ku-approve safari yake, lakini maofisa walipoulizia kwenye hiyo kampuni aliyosema ndiyo anakwenda kikazi walikataa kuwa hawamfahamu mtu huyo pia hata hiyo kampuni aliyotoka pia maofisa waligundua kuwa haijawahi kuwepo pia hata hotel aliyosema kafanya Resevation/booking walikataa kua hawamfahamu mtu huyo na hajachukua chumba hapo.

Msafiri huyo alikua anaongea kifaransa, kijapan na lugha nyingine nyingii. Kuongea kwake kijapani kidogo ilikua ni ushahidi kua hua anakuja nchini Japani. Lakini walipomuonyesha ramani ya dunia aonyeshe wapi nchi yake hiyo ya Tuared ilipo alishangaa kuwa haioni kwenye ramani, akaonyesha sehemu inayoitwa Andorra kua ndiko nchi yake hiyo ilikuwepo. Akasema tured ipo miaka zaidi ya elfu hivyo ingekuwepo kwenye ramani, akahitaji maofisa wamalizane na hilo swala lake aondoke kachoka kukaa kwenye chumba cha mahojiano.

Hivyo maofisa uhamiaji wale walimtafutia chumba kwenye hotel iliyopo jirani na uwanja wa ndege, maafisa uhamiaji wawili walipangwa kulinda chumba chake hicho usiku kucha ili kesho yake aendelee kufanyiwa uchunguzi. Asubuhi kulipokucha walikuta Yule msafiri katoweka. Haikujulikana alipitia wapi maana kama ni dirisha la chumba cha hoteli lilikua juu kabisa hotelini pia mtaa ule ulikua bize muda wote hivyo angeonekana dirisha pia lilikua limefungwa. Hadithi ya msafiri huyo inaishia hapo maana hakuonekana tena mpaka leo na hakuna mtu aliyewahi kujua nchi hiyo ya Tuared iko wapi japo wanahistoria mbalimbali kutoka Japan walijaribu kufuatiia nchi hiyo uwepo wake miaka iliyopita.
 
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
3,244
2,000
Nakazia tu pia tafuta movie ya Interstellar hii concept ya time travel imeelezewa vizuri
kwa ufupi mdingi amesafiri kwenye future kamuacha binti yake akiwa na miaka 10,
yeye kwenye future alitumia kama dakika 30 tu,lakini huku duniani ni kama miaka 60 imeenda
anarudi duniani anakuta binti wake ni kibibi kizee kikongwe, wakati yeye ametumia dakika 30 tu.
 
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
21,069
2,000
Kwa nini chochote kiwe suluhisho la kifo? Kwani kifo ni tatizo? Kifo ni muhimu na ni lazima ili Dunia na maisha ya viumbe yaendelee kuwepo, bila kifo hakuna maisha, viumbe vingi vinategemea ili viishi tunapata chakula na ardhi yenye rutuba na mazingira ya kuvutia kwa sababu ya viumbe vilivyokufa.

Hivyo kifo ni muhimu na ni lazima, kama kuna jambo jema hapa Duniani kuwahi kutokea basi KIFO!
 
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
3,244
2,000
all in all time travel ili iwezekane lazima uwe na speed kali kuliko ya mwanga,,
hivyo ni impossible kwa time travel kutokea,,hata ikotokea itakuwa umesafiri kwenda past na sio future...........
labda wanasayansi wa CERN wanaweza kuja na jibu kupitia particle accelerator yao............
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
nakazia tu,pia tafuta movie ya Interstellar hii concept ya time travel imeelezewa vizuri
kwa ufupi mdingi amesafiri kwenye future kamuacha binti yake akiwa na miaka 10,
yeye kwenye future alitumia kama dakika 30 tu,lakini huku duniani ni kama miaka 60 imeenda...
anarudi duniani anakuta binti wake ni kibibi kizee kikongwe,wakati yeye ametumia dakika 30 tu................
Hata kwenye avanger endgame baada ya Scott lang/Ant-man kukwama kwenye ule mtambo wa kwenda kwenye Quantum realm alikaa humo masaa matano aliporudi anakuta miaka 5 imepita bintiye cassie ashakua mkubwa akawa anashangaa imekua vipi...
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
all in all time travel ili iwezekane lazima uwe na speed kali kuliko ya mwanga,,
hivyo ni impossible kwa time travel kutokea,,hata ikotokea itakuwa umesafiri kwenda past na sio future...........
labda wanasayansi wa CERN wanaweza kuja na jibu kupitia particle accelerator yao............
Ya tafiti zote naona wanafanya kusafiri kwenda past but trust me kama ikifanikiwa kwenda past basi itakua so simple kwenda future.

Ya inabidi uwe unamwendo mkali kuliko mwanga ili kutengeneza Curveture kwenye Gravity ili kurudisha muda nyuma au kuupeleka mbele
 
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
3,244
2,000
Ya tafiti zote naona wanafanya kusafiri kwenda past but trust me kama ikifanikiwa kwenda past basi itakua so simple kwenda future. Ya inabidi uwe unamwendo mkali kuliko mwanga ili kutengeneza Curveture kwenye Gravity ili kurudisha muda nyuma au kuupeleka mbele
Stephen Hawking kwenye kitabu chake cha "Brief answers to the Big Question" ameelezea posibility ya Time Travel ni ndogo kwa sasa kutokea.mwaka 2009 alihost party kwa ajili ya time travell lakini hakuna aliyetokea hata mmoja.

Hakutuma kadi za mwaliko until party ilivyoisha akiamini kama kuna time traveller wa ukweli wangekuja kwenye party, siku ya party hakuna mtu aliyejitokeza kwenye party.
 
Mr the dragon

Mr the dragon

JF-Expert Member
1,386
2,000
Katika vitu ambavyo vimethibitisha Mimi ni kilaza ni hii time traveling.Mbali na kwamba je inawezekana kutokea hata kuielewa tu nimeshindwa.

Nimesoma Sana kuhusiana na hii kitu plus kuangalia movie Lakini wapi huwa siielewi kabisa.
 
carcinoma

carcinoma

JF-Expert Member
4,781
2,000
Ya tafiti zote naona wanafanya kusafiri kwenda past but trust me kama ikifanikiwa kwenda past basi itakua so simple kwenda future. Ya inabidi uwe unamwendo mkali kuliko mwanga ili kutengeneza Curveture kwenye Gravity ili kurudisha muda nyuma au kuupeleka mbele
Kwani mkuu future tayari ipo?

I mean sasa hivi mimi ambaye hata mke sina kwenye future kuna watoto wangu.
Kwamba mtu akienda future atakuta watoto wangu wakati sina hata mke?
Naona ni easy kwenda past kuliko future maana nahisi future ndio tunaitengeneza sasa hivi haipo tayari
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
BOB OS,
Hata kama mkuu unajua hiyo kitu haiwezi kutoa majibu mojakwa moja kua time travel aint real, unakumbuka Miaka 500 iliyopita binaadamu walijua dunia ni moja na jua inazungukadunia? leo imekuaje? unakumbuka sababu ya kifo cha Galei galileo
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
Kwani mkuu future tayari ipo?
I mean sasa hivi mimi ambaye hata mke sina kwenye future kuna watoto wangu..
Kwamba mtu akienda future atakuta watoto wangu wakati sina hata mke?
Naona ni easy kwenda past kuliko future maana nahisi future ndio tunaitengeneza sasa hivi haipo tayari
Kiukweli am not sure kuhusu hilo la future, kama nilivyosema mwanzo tafiti nyingi zanzungumzia Back time travel na sio future, naweza kukubaliana na kukataa kwa neno lako hilo.
 
BOB OS

BOB OS

JF-Expert Member
3,244
2,000
Na kama time traveling ni suluhisho la kifo,je mtu akiweza kusafiri kwenye past na kuua wazazi wake,je nini kitatokea?

Na nukuu kutoka kitabu cha "Brief Answers to the big questions",Stephen hawking anasema
"In conclusion, rapid space travel and travel back in time can’t be ruled out according to our present understanding.

They would cause great logical problems, so let’s hope there’s a Chronology Protection Law to prevent people going back and killing their parents. But science-fiction fans need not lose heart. There’s hope in M-theory."
 
carcinoma

carcinoma

JF-Expert Member
4,781
2,000
Katika vitu ambavyo vimethibitisha Mimi ni kilaza ni hii time traveling.Mbali na kwamba je inawezekana kutokea hata kuielewa tu nimeshindwa.

Nimesoma Sana kuhusiana na hii kitu plus kuangalia movie Lakini wapi huwa siielewi kabisa.
Mkuu sio kwamba wewe ni kilaza..nop.
Ni kwamba hii kitu haieleweki kwanza ni theory tu ambazo watu wanawaza na sio real..

Imagine eti usafiri urudi mwaka 1970 halafu umuue mshua wako wakati wewe ulizaliwa 1980 ....itakuwaje?
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,418
2,000
Katika vitu ambavyo vimethibitisha Mimi ni kilaza ni hii time traveling.Mbali na kwamba je inawezekana kutokea hata kuielewa tu nimeshindwa.

Nimesoma Sana kuhusiana na hii kitu plus kuangalia movie Lakini wapi huwa siielewi kabisa.
Ni rahisi lakini kama huna hata idea ya physics hii kitu ni ngumu kidogo kuelewa lakini mimi naona huelewi kwakua umeiruhusu akili yako ione hiki kitu ni kigumu kukielewa
 

Forum statistics


Threads
1,424,523

Messages
35,065,902

Members
538,009
Top Bottom