sasa hii mifano yako ndio inayosababisha mparaganyiko wa fikra!! huwezi kujiuliza kitu ambacho logic haikubaliani nacho eti huenda ukagundua kitu usichokijua!!
Logic gani? Unachosema wewe ukikichambua sana utakataza maswali kabisa.
Kitu gani ambacho logic haikubaliani nacho hapo? Uwezekano wa kurudi nyuma kwenye muda? Logic gani hiyo?
Kama Einstein kashatuonesha kwamba time is a dimension of the space-time continuum, what is so illogical about asking if it is possible to move back in time?
Katika physics hakuna kitu chochote strange kwa vitu kurudi nyuma in time, it is just a perfect symmetry of moving forward in time.
Kama unaweza kwenda mbele na nyuma in space, and time is just another dimension of the same space-time continuum, what is so strange about asking about going back in time?
Je mtu akikwambia katika multiverse huko kuna universes zilizo na three dimensions of time and one dimension of space, ambako katika time unaweza ku move dimensions tatu, sio mbele na nyuma tu, bali hata kulia na kushoto na juu na chini, lakini katika space una move mbele tu, utasemaje?
anaeuliza kwa nini rangi ya blue ni blue!! yeye lengo lake ni kujua sababu? au ana jambo lingine anatafuta??
Anataka kujua kwa nini rangi ya blue ni ya blue.
unapoanza kujiuliza kitu unatakiwa uwe na lengo !!
Lengo ndilo hilo, kujua kwa nini rangi ya blue ni ya blue. Hilo si lengo?
Mfano mwingine wa fikra au elimu isio na manufaa ni kama ule wa kwenda kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwa na maisha ktk MARS!!
Manufaa kwa nani? Kwa mtu ambaye nia yake ni kujua jibu la swali, kupata jibu na kukidhi kiu ya kujua tu ni manufaa.
Isitoshe, vitu vingine huwezi kujua manufaa yake mpaka uvigundue na kuvichunguza kwanza.
Maxwel alicheza sana na equations kabla watu hawajaweza kugundua kwamba equations zake zinahusika katika kuonesha uhusiano wa magnetism, electricity and the speed of light. Watu wakazifanyia kazi mpaka wakagundua umeme, leo umekaa kwenye computer na mimi nimekaa kwenye computer tunawasiliana.
Ungekataza utashi wa Maxwell tungeweza kupata umeme kirahisi hivi?
Wakati hii dunia tunayoishi, binaadamu ame occupied only 10% ya dunia! na 90% iko tupu!!
Ame occupy only 10% kwa kigezo gani?
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "Extinction Level Event" wewe? Dunia ikipigwa kimondo kufikia "Extinction Level Event" bila ku explore sehemu nyingine watu watafanyaje?
Unafikiri kila mtu anafikiria kula ugali na kulala?
NA wakati huo huo USA wanatumia billions of dollars kwenda kwenye misheni zisizo na faida WAKATI NYUMBA KWAO KUNA ALMOST 3 MILLION PEOPLES HOMELESS!! WAKATI WA WINTER WATU WANAKUFA NA BARIDI KWA KULALA MITAANI!!
Wewe yanakuhusu nini? Waache watu wao waseme.
sasa hii time travel ina lengo lipi??
Unaifahamu GPS ile? Basi ile GPS system ile, inayosaidia watu kufahamu ramani kwa kutumia satellite, imeanzia kwenye hesabu na physics huko, kwenye Relativity ya Einstein hii hii tunayoiongelea inayohusika katika Time Travel. Kwa hiyo kama mtu asingejiuliza swali kuhusu habari za time travel, leo kusingekuwa na GPS. Hii ni application moja tu kati ya nyingi sana zinazoweza kutokana na research hizi.
Hayo ma weather satellite yote yanayowapa watu utabiri wa hali ya hewa na kutabiri vimbunga na mvua yanaweza kufanya hivyo kwa kutumia principles za relativity.
Kwa hiyo fikiri kama haya mambo ma GPS, ma satellite systems yanayotabiri hali ya hewa na kuongoza ndege, yanayotupa notice kwenye vimbunga yasingekuwepo kwa sababu hakuna watu waliouliza maswali ya time travel, leo tungekuwa wapi.
Everytime a plane lands safely, the GPS system used, the weather prediction system used, the tower control system used, all are using relativity and principles of time travel that you so readily dismiss without understanding.
hebu nisaidie hapo!! manake ukiishughulisha sana akili kwenye mambo yasio na maana! jamii inaweza athirika na wewe huna hata habari!! KAMA HAO WAZUNGU WANAOJIFANYA KUWAV NA AKILI NYINGI!!
Basically kila kitu kinachohitaji high precision in time kinahitaji Special Relativity na mambo ya time travel yanaingia hapo. Kuna processor za research computers zinatumia kanuni za relativity kupata accuracy in performance. Zinatumia relativity katika kuhakikisha magnetic field ya storage media ina store data accurately.
Hebu tuumize vichwa kujaribu kutatua matatizo tulionayo kwanza!! tena yako mengi mno!! Hii time travel tuiache kwenye MOVIES KWANZA!!
Kama hujaelewa the principles behind the concept, and the relevant questions, how could you dismiss that which you do not understand?
Historia ya sayansi na ugunduzi imejaa mifano ya vitu ambavyo viligunduliwa kabla ya kujulikana kwa matumizi yake.
Ukitaka watu wahangaikie ugunduzi wa vitu ambavyo wanavielewa matumizi yake tu unajionesha jinsi ulivyokosa kuelewa historia ya uvumbuzi.