miles45
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 3,468
- 8,287
Wanaume mnisikie!
Unapotumia Fedha kama chambo cha kumpata binti ujue kuna haya mambo mmawili
1. Wewe ni mshamba usiyejiamini na usiyejua namna ya kuzungumza,
2. Wewe ni mshenzi unayemlinganisha mwanamke na bidhaa
Sasa ukitapeliwa unaanza malalamiko.
Mwanaume anayejiamini, anayejua anataka nini HATUMII FEDHA kama chambo. Husimama yeye kama yeye na sio kujificha nyuma ya fedha.
Kimsingi mnawageuza wanawake kama chombo mnapotaka kuwanunua kwa vipande vya fedha. Hii ni dharau kubwa sana, sijui kwa nini wanawake wanakubali kudharauliwa kwa kukubali kununuliwa kama soksi... Ikichakaa inatupwa. Mnasema, 'mwanamke nakupa kila kitu, bla bla bla...' kisa umemalizia fedha zako hapo ukidhani zitakusaidia
Mjue kuwa mwanamke bora thamani yake hailinganishwi na chochote. Zaidi sana ni heshima na upendo ndio vyatakiwa. Utampa fedha na kesho yake anatorokea kwa asiyempa fedha. Unalaani wala laana haimpati kwa kuwa ulidhani ananunulika kwa fedha.
Muache kutumia fedha kama chambo cha kupata penzi. Iko wazi kuwa mwanaume HAMPI mwanamke fedha kama haoni dalili ya kupata anachotaka. Anapotoa fedha ni kama anarahisisha mambo, aweze kupata sababu ya kudai anachotaka. Na ndio maana akitoswa analalamika
Msikilize mpenzi wako, mpe muda wako, msifie, jiamini ukiwa naye mbele za watu, Mwombee, mchekeshe, mtulize, mlinde. Usifanane na wanaorusha hela wanadhani zitafanya kila kitu. Wapo mabilionea, wanahonga na hawapati mke.
Kama mwanamke kaongea wewe ni nani ubishane nae.....?
USIMPE MWANAMKE FEDHA
Ni hayo kwa leo.
️Bibi Happy Wa Joseph