Tiketi ya kupendwa sio kuhonga. Twende na mwanadada happy

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
545
1,000
Wanaume mnisikie!
Unapotumia Fedha kama chambo cha kumpata binti ujue kuna haya mambo mmawili
1. Wewe ni mshamba usiyejiamini na usiyejua namna ya kuzungumza,
2. Wewe ni mshenzi unayemlinganisha mwanamke na bidhaa

Sasa ukitapeliwa unaanza malalamiko.

Mwanaume anayejiamini, anayejua anataka nini HATUMII FEDHA kama chambo. Husimama yeye kama yeye na sio kujificha nyuma ya fedha.

Kimsingi mnawageuza wanawake kama chombo mnapotaka kuwanunua kwa vipande vya fedha. Hii ni dharau kubwa sana, sijui kwa nini wanawake wanakubali kudharauliwa kwa kukubali kununuliwa kama soksi... Ikichakaa inatupwa. Mnasema, 'mwanamke nakupa kila kitu, bla bla bla...' kisa umemalizia fedha zako hapo ukidhani zitakusaidia

Mjue kuwa mwanamke bora thamani yake hailinganishwi na chochote. Zaidi sana ni heshima na upendo ndio vyatakiwa. Utampa fedha na kesho yake anatorokea kwa asiyempa fedha. Unalaani wala laana haimpati kwa kuwa ulidhani ananunulika kwa fedha.

Muache kutumia fedha kama chambo cha kupata penzi. Iko wazi kuwa mwanaume HAMPI mwanamke fedha kama haoni dalili ya kupata anachotaka. Anapotoa fedha ni kama anarahisisha mambo, aweze kupata sababu ya kudai anachotaka. Na ndio maana akitoswa analalamika

Msikilize mpenzi wako, mpe muda wako, msifie, jiamini ukiwa naye mbele za watu, Mwombee, mchekeshe, mtulize, mlinde. Usifanane na wanaorusha hela wanadhani zitafanya kila kitu. Wapo mabilionea, wanahonga na hawapati mke.

Kama mwanamke kaongea wewe ni nani ubishane nae.....?

USIMPE MWANAMKE FEDHA
Ni hayo kwa leo.
️Bibi Happy Wa Joseph
 
Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,303
2,000
Nimewahi seat ya mbele kabsa mkuu, nimeona unawazo chanya kabxaaa. Fanya uni pm tuyajenge😅😅
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,748
2,000
kama chambo. Husimama yeye kama yeye na sio kujificha nyuma ya fedha.
Unaposema husimama yeye kama yeye una maanisha anatumia nini katika mwili wake kumnasa mwanamke ?

Kwa sababu unaposema hatumii fedha ambayo anayo ni yake,anatumia nini kingine ambacho sio chake kumnasa mwanamke ?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
36,264
2,000
Unaposema husimama yeye kama yeye una maanisha anatumia nini katika mwili wake kumnasa mwanamke ?

Kwa sababu unaposema hatumii fedha ambayo anayo ni yake,anatumia nini kingine ambacho sio chake kumnasa mwanamke ?
Mwanamume kamili anatumia kauli za ushawishi na lugha ya picha, sio kuhonga pesa ili ampofushe mwanamke. Kuhonga ni quick solution inayotumiwa na wapenda shortcut ila gharama zake ni kubwa sana mbeleni.
 
miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
545
1,000
Unaposema husimama yeye kama yeye una maanisha anatumia nini katika mwili wake kumnasa mwanamke ?

Kwa sababu unaposema hatumii fedha ambayo anayo ni yake,anatumia nini kingine ambacho sio chake kumnasa mwanamke ?
Unajitumia wewe mwenyewe sio kujificha nyuma yakimvuli cha pesa
 
The Wolf

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
8,484
2,000
Inategemea na ninachokitaka kwa mda huo, kama ni utelezi tuu natoa hela, ntahonga mpaka pale nitakapochoka naye anichune kwa kadiri ya ushawishi wake.

Kama ninataka uhusiano wa muda mrefu hapo sasa pochi huwa inatumika kwa matumizi ya kustawisha upendo ila siyo kuhonga.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,748
2,000
Unajitumia wewe mwenyewe sio kujificha nyuma yakimvuli cha pesa
Mguu hutautumia kumnasa mwanamke.

Wala damu hautaitumia kumnasa mwanamke.

Wala kucha hautasitumia kumnasa mwwnamke.

Sasa lazima kuna kitu utatumia kumnasa mwanamke katika mwili wako,eidha maneno,au umbile lako,ama busara zako,ama uhandsome wako au ustaarabu wako.

Au uongo na hukukusudia kwamba huwezi kutumia kati ya hivyo kumnasa mwanamke ?
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
11,081
2,000
Wanaume mnisikie!
Unapotumia Fedha kama chambo cha kumpata binti ujue kuna haya mambo mmawili
1. Wewe ni mshamba usiyejiamini na usiyejua namna ya kuzungumza,
2. Wewe ni mshenzi unayemlinganisha mwanamke na bidhaa

Sasa ukitapeliwa unaanza malalamiko.

Mwanaume anayejiamini, anayejua anataka nini HATUMII FEDHA kama chambo. Husimama yeye kama yeye na sio kujificha nyuma ya fedha.

Kimsingi mnawageuza wanawake kama chombo mnapotaka kuwanunua kwa vipande vya fedha. Hii ni dharau kubwa sana, sijui kwa nini wanawake wanakubali kudharauliwa kwa kukubali kununuliwa kama soksi... Ikichakaa inatupwa. Mnasema, 'mwanamke nakupa kila kitu, bla bla bla...' kisa umemalizia fedha zako hapo ukidhani zitakusaidia

Mjue kuwa mwanamke bora thamani yake hailinganishwi na chochote. Zaidi sana ni heshima na upendo ndio vyatakiwa. Utampa fedha na kesho yake anatorokea kwa asiyempa fedha. Unalaani wala laana haimpati kwa kuwa ulidhani ananunulika kwa fedha.

Muache kutumia fedha kama chambo cha kupata penzi. Iko wazi kuwa mwanaume HAMPI mwanamke fedha kama haoni dalili ya kupata anachotaka. Anapotoa fedha ni kama anarahisisha mambo, aweze kupata sababu ya kudai anachotaka. Na ndio maana akitoswa analalamika

Msikilize mpenzi wako, mpe muda wako, msifie, jiamini ukiwa naye mbele za watu, Mwombee, mchekeshe, mtulize, mlinde. Usifanane na wanaorusha hela wanadhani zitafanya kila kitu. Wapo mabilionea, wanahonga na hawapati mke.

Kama mwanamke kaongea wewe ni nani ubishane nae.....?

USIMPE MWANAMKE FEDHA
Ni hayo kwa leo.
️Bibi Happy Wa Joseph
Kwa mke wa kuoa sawa

Ila katika pussy banging category,nothing I hate on this planet earth kama kufata mlolongo wa kutongoza,such a very very stupid way of wasting your time!
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,686
2,000
Kuhonga jamani pako palepale
ina maana sisi tuliooa tutapataje Pisi kali, tuanze tena Hadithi mm sina mwenza kabisa aunilimaliza Mlimani au mm nachhezea timu kubwa
watu wanahonga vyeo, majumba, magari, viti maalum je zote hizo sio suuza roho?
Km nina mke na wanangu wanasubiria matunzo na Ada nikipatacho cha ziada ni kuhonga na kusuuza loho baada ya hapo narudi kwetu,
watu wamefyekwa kuchangia choo cha kike kumbe hamjui penye udhia penyeza .....rupia
 
miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
545
1,000
Mguu hutautumia kumnasa mwanamke.

Wala damu hautaitumia kumnasa mwanamke.

Wala kucha hautasitumia kumnasa mwwnamke.

Sasa lazima kuna kitu utatumia kumnasa mwanamke katika mwili wako,eidha maneno,au umbile lako,ama busara zako,ama uhandsome wako au ustaarabu wako.

Au uongo na hukukusudia kwamba huwezi kutumia kati ya hivyo kumnasa mwanamke ?
Basi endelea kutumia pesa
 
Sir Midabwada

JF-Expert Member
Sep 27, 2020
507
1,000
Hizi research mmezifnyia wap n assumption ilkuw ipi!!?? Mbon mnaongea mambo too general wakat kila aliyejenerolaiziwa ana mtazamo wake
 
miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
545
1,000
Ila kumbukeni wakati nyie mnahangaika ili mpate penzi lazima muwe na pesa kuna wenzenu wanateleza tu na mambo mengine yanaenda. Endeleeni kuumia si mnazani kuumia sifa
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
54,119
2,000
Umeongea vizuri...
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Kutumia pesa it's a quick but not a permanent solution...
Kwanza makubaliano alafu sasa pesa ndiyo huna na thamani...Cc: mahondaw
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,748
2,000
Basi endelea kutumia pesa
Ukija na hoja lazima uweze kuitetea,hutakiwi kuishia njiani.haya ni mambo ya majadiliano tu.

Maoni yako ni batili kwa sababu hayana utetezi wowote kutoka kwako.

Hivyo hautakiwi kuwarudisha wanaume nyuma kutumia pesa kuwapata wake ambao wanawapenda.

Pesa ni kitu ambacho anakuwa nacho mwanaume cha kwake hivyo anahaki ya kukitumia kumnufaisha.

Kama ambavyo maneno mazuri ni kitu anachokuwa nacho mwanaume hivyo anahaki ya kutumia anavyotaka

Na ndivyo hivyo kwa uhandsome,busara,tabia nzuri hivi vyote ni vitu ambavyo mwanaume ikiwa atakuwa navyo basi ni vyake na ana haki ya kutumia atakavyo.

Sasa ubapoitenga pesa kwa mwanaume ambayo tayari anayo na kufanya asitumie kwa namna itakayomnufaisha huku unakubali atumie vitu vingine inakuwa hufahamiki kabisa.
 
miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
545
1,000
Kila siku tunaambizana kuwa mwanaume tengeneza maisha yako kwanza ,ishi maisha yako hawa wanajileta wenyewe tu. Mbona hamuelewi mkaza shingo tu....?

Huoni hawa wasanii wa kigeni wakija bongo dada zenu wanavyo washobokea na kuwalilia unataka kusema waliwapa hela.....? Na hawa wasanii wanaweza wakawavua chupi dada zenu na wasiwape hata buku la maji na dada zenu wakafurahi. Na sio wasanii tu hata wanaume wengi tu wanao jitambua wanawacharaza vizuri tu na hata mia hawawapi na kesho dada anajibeba na kukipeleka tena kikaliwe.

Formula ni hii
Mwanaume tafuta pesa kwa ajili yako, na ujijenge vizuri na misimamo yako. Sio kwa sababu ya hela ndio uanze kuwafukuzia utawakosa na kujichafulia Jina katika mazingira yaliyopo na wote wakakukimbia.

Yaani ukisha zipata tu kuwa mpole jichanganye na makundi yenye jinsia ya kike wengi kama vile jogging, kwaya na mengineyo, watengenezee akili wakutafsiri kwamba unafikika kirahisi, sio utengeneze ukuta. Kuwa mtu wa watu ,usijisikie, kuwa mcheshi kiasi, vimisaada vya uongo na ukweli vya hapa na pale.

Usioneshe urafiki mkubwa na mwanamke mmoja , wote wachukulie sawa kwa kipimo kimoja haijalishi wapoje wenye matako makubwa, wenye pasi wote waweke kwenye mzani mmmoja.

Kuna wale wanawake vimbelembele ambao watataka kuwaonesha wenzao kuwa wamekushika hao ni wa kuWakimbia maana ndio watakao kuharibia shughuli yako

Alafu kuwa msiri sio mpayukaji ili kuwahakikishia ulinzi wale wanao jiheshimu.

Najua hadi kufikia hii hatua watajilahisisha wengi sana kwako na kuanza kufanya mashindano wenyewe kwa wenyewe wakupate , na siku zote mwanamke hanaga cha kutoa zaidi ya kikojoleo chake, sasa hapa ndio wakati wako mzuri wa kuanza kuvuna asali ya mizinga yako hapa pindua mmoja baada ya mwingine na usioneshe kumtaka hata kama umevutiwa nae . Na hapa utagonga wote walio katika mazingira hayo na kama ndio unawakuna vizuri ndio utawaua kabisa . Ila baada ya hapo mimi sipo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom