Tigo kwaherini

Tigo kwaherini

Kampuni ya Tigo nawaaga. Moja kwa moja. Sitatumia tena huduma zenu. Endeleeni na ukamuaji mnaofanya. Sina hata haja ya kuorodhesha kero zenu.

Mungu awalinde
Juzi wakanipigia simu nikawaambia nimehamia voda nilikuwa mteja wao mzuri saana hasa wa airtime na internet.
 
Halafu wezi wa credit. Ukiweka kisalio wanasepa nacho. Ukipiga customer care hakuna msaada. Bora kuwahama wabaki na mazombi yao
 
Mimi nimeagana nao yapata mwezi sasa!
Nasikuondoka hivihivi ..niliondoka na 6000/ yao walonikera vya kutosha!
 
Kampuni ya Tigo nawaaga. Moja kwa moja. Sitatumia tena huduma zenu. Endeleeni na ukamuaji mnaofanya. Sina hata haja ya kuorodhesha kero zenu.

Mungu awalinde
Tigo sina hamu nao. Hasa walipoondoa meseji kwenye kifurushi cha halichachi. Niliwapa mkono wa kwa heri
 
Weka ushahidi hatua stahiki zichukuliwe.

Ushahidi ni kuwa hawahoji kwanini hiyo mitandao ipandishe bei ya vifurushi bila kutaarifu wateja wake. Kama huamini kuwa serikali inajua kinachoendelea, hebu kesho vyombo vya usafiri vipandishe nauli bila ridhaa ya serikali uone kama serikali itakaa kimya.
 
bora ubaki uko kama cm ukipga mnasikiana mana uku airtel unapewa gb 1 na dakika 100 kwa buku ila network utajua ww utaitoa wap mpaka kifurushi kinakata
 
Nahisi laini zinatofautiana hii mm sina.ipo ya 5000 2gb kwa wiki. Sijui kwakuwa lain yangu ya zamani.una bahati au menu yako iko tofauti na ya wengine?

Kwa wiki nikijibana natumia 8000 yaan nanunua voda dk 250 all net kwa 3000 nanunua 2gb tigo kwa 5000 kwa ajili ya net tu. Na hii 2gb haifiki wiki dah

Sasa nawaza nikisajili lain nyingine ntaweza beba simu mbili?
Hama hama itakuwaje na kazini maana wateja washazoea hizo no.dah
Nenda Zantel
 
Huu ni waizi mtakatifu
Nimeachana nao wako wanajishtukia. Siku hizi wananipigia mahuduma yao ya bima sitaki kuyasikia nina NHIF inatosha.
IMG_20210314_225349.jpg
 
Sasa bwana Joseph labda fafanua,bifu la wewe na tigo limeanza kwenye ishu gani,Mimi jengo la tigo huwa napita tu sijui wana shughulika na Nini
 
Usitukane mamba bro, sisi wa vodacom tunatamani kuhamia huko unakotoka!
Mkuu, vifurushi vya tiGO na voda vyote sawa, huku Voda kwa elf 10 unapata 2.5GB kwa mwezi na tiGO ni hivyo hivyo

Laini za mitandao yote hiyo ninazo, kinachonifanya nishindwe kutoka Voda ni spidi ya internet tu

Halotel wananipa 10GB kwa elf 10 kwa mwezi, ila spidi sasa hamna kitu
 
Mkuu kama simu yako ina 4G. nenda kabadili laini iwe ya 4G utakuja kunishkuru. mkuu saiv nachana mawimbi na holotel kama voda tu tena na cheza na online game bila tatizo.
 
Mkuu kama simu yako ina 4G. nenda kabadili laini iwe ya 4G utakuja kunishkuru. mkuu saiv nachana mawimbi na holotel kama voda tu tena na cheza na online game bila tatizo.
Laini niliyonayo ni ya 4G na simu pia ni ya 4G, kutembea na simu mbili ndo sipendi,
Maana hizi laini ya tiGO huu ni mwaka wa 14,
Na laini ya Vodacom huu ni mwaka wa 9

Halotel,
TTCL,
Airtel (hii nataka nikaifutie usajiri kabisa ili wajue siwapendi)
Hizi hata miezi sita bado hazijafikisha
 
Back
Top Bottom