Tigo acheni wizi wa kijinga,nafungua kesi ya madai

kulwa12

Senior Member
Jun 30, 2009
103
28
Naandika ujumbe huu wadau kwa masikitiko makubwa sana,ni kwanini mtandao wa simu wa tigo unakua na wizi wa waziwazi hivi?

Leo ni karibu siku ya tatu napokea ujumbe wa ajabu ajabu kutoka namba 15556,na kila wakikutumia wwanakata tsh 500.

Hii huduma mimi sijajiunga na after all mambo wanayotuma ni ya kijinga na kitoto amabayo mimi siyaitaji, mfano leo wamenitumia ujumbe huu na kunikata tsh.500

" Withney death authorities believe huston may have fallen asleep or lapsed into unconsciousness in the bathtub drowened.water has been found in her lungs"

habari hii si kwamaba mimi naifahamu tu na nilishaisoma kwenye mtandao tmz,wamekopy maneno yote msitari baada ya msitari kutoka mtandao huu,na hawakuonesha source kwamba wametoa kwenye mtandao huu.

Pili habari ni yauongo si ya kweli kwani taarifa rasimi juu ya kifo ya whitney hazijatoka na itachukua wiki mbili mpaka tatu.

Hii authority wanaosema imetoa taarifa hii ni ipi na wao wanauhakika nao upi? Na je wana mamlaka ya kisheri ya kusamabaza habari hizi kwamaba ni rasimi whitney kafa kwa kuzama kwenye maji?

Sasa ninafungua kesi kubwa ya madai amabayo itakua mfano katika nchi hii na fundisho kwa haya makapuni ya simu,niko tayari hata kutumia senti yangu ya mwisho kwa hili.
 
Uliruhusu mwenyewe kupata msg za namna hiyo...Hawawezi kuanza kukutumia usipo'ratify!
Tafuta namna ya ku'unsubscribe!
 
Ninaandika hoja hii kwa masikitiko makubwa hasa baada ya kushuhudia viwango vya gharama ya kupiga simu vikipanda kinyemela bila kutangazwa. Kwa mfano Tigo wanajinadi kila siku kuwa gharama ni sh 1 kwa sekunde ilihali si kweli hata kidogo. Hebu wadau jaribuni kutia elfu 1 kwenye simu yako ya tigo halafu mpigie mtu mwenye tigo uone kama utaongea hata dak 6. Ni wizi wa mchana kweupe jamani wana JF tupige kelele hii hali itoweke au watangaze hizo bei zao mpya. NI WIZI KAMA MAFISADI WENGINE.
 
wako sahihi..kwani garama za uendeshaji zimepanda TBL pekee?hapana.

pata picha enzi zile unapiga simu per minute 500...wamejitahidi sana kushusha garama zao...sema tu hawana utaratibu mzuri wa kutoa taarifa
 
kuna hii caller tuner.. aibobo who is calling my daughter now? imagine mtu kama mimi naekojoa wima..
 
Mkuu mi sio mwehu nilalamike bure,wametuma bila mimi kujiunga na hawajaanza leo kuniunganisha na huduma amabzo sijaomba.
uliruhusu mwenyewe kupata msg za namna hiyo...hawawezi kuanza kukutumia usipo'ratify!
Tafuta namna ya ku'unsubscribe!
 
waripoti tcra..., wana sehemu ya complaints..., mm binafsi staki ujinga kabsaaa, naripoti kila ****** na hua napata ufumbuzi..., nahisi saivi tcra wameshakremu namba zangu za simu
 
Ni kama mwezi wananitumia jumbe ambazo sijajiunga na kunikata hela. Cha ajabu ukisema ondoa wanajibu itatoka baada ya masaa 24 lakini hali ni ileile. Am tired with u Tigo
 
mkuu nami nimefanya hivyo na inauzi sana pale hata unapowaambia hutaki huduma wanaendelea tu kukutata hela mim kila siku mia tano nzima nikiweka tu hela msg zenyewe ujinga tupu
Ni kama mwezi wananitumia jumbe ambazo sijajiunga na kunikata hela. Cha ajabu ukisema ondoa wanajibu itatoka baada ya masaa 24 lakini hali ni ileile. Am tired with u Tigo
 
Mkuu mi nawapeleka mahakamini hawa kabisa kwani hii ni criminal offence,ni wizi kabisa.
waripoti tcra..., wana sehemu ya complaints..., mm binafsi staki ujinga kabsaaa, naripoti kila ****** na hua napata ufumbuzi..., nahisi saivi tcra wameshakremu namba zangu za simu
 
Wanakera hawa!
Na hivi vimeseji vyao vya hadi ucku wa manane vinakera sana

Mie nisha achana naa wanabore sana!
 
Labda nikuulize swali moja hiyo cm yako unaitumiaga peke yako?hakuna mtu mwingine anaye ishikaga? Jaribu kufanya uchunguzi wa kina sio kila kitu una blame alafu usikurupuke tu kwenda mahakamani na hata hiyo kauri yako ya mwisho ya kusema utatumia mpaka senti yako ya mwisho mimi binafsi sidhani kama ni kauri yenye mantiki na kuomba ukae chini tena ufikirie alafu ufanye maamuzi yalio sahii
 
zamani bana...hata ukipigiwa unachajiwa
gharama zimepanda mno,nimeshtuka leo cool blue wamepandisha maji ya dispenser from 3500 hadi 5500 sijui ndio ile gharama ya umeme imeongeza production cost?..huko tuendako ni kizani
 
Mkuu hakuna mtu anaeshika simu yangu zaidi yangu mwenyewe,na nisingefikia maamzi haya kama ingekua ni mara ya kwanza hii ni mara ya tatu wanafanya hivi,mwanzao walianza na kunitumia utabiri wa nyota kila asubuhi na kukata hela,nikatuma msg zaidi ya 20 kuomba kujitoa na huduma hii(japo sikujiunga) bado wanaendelea tu kukata hela,mdau lazima nichukue hatua ili liwe fundisho kwani najua case nyingi sehemu nyingine nini kimetokea na wala sikurupuki najua nachokifanya,na hata kutuma msg yenye tarifa potofu na usiokua na mamlaka ya kuisamabaza ni kosa lingine la kisheria.
labda nikuulize swali moja hiyo cm yako unaitumiaga peke yako?hakuna mtu mwingine anaye ishikaga? Jaribu kufanya uchunguzi wa kina sio kila kitu una blame alafu usikurupuke tu kwenda mahakamani na hata hiyo kauri yako ya mwisho ya kusema utatumia mpaka senti yako ya mwisho mimi binafsi sidhani kama ni kauri yenye mantiki na kuomba ukae chini tena ufikirie alafu ufanye maamuzi yalio sahii
 
Naandika ujumbe huu wadau kwa masikitiko makubwa sana,ni kwanini mtandao wa simu wa tigo unakua na wizi wa waziwazi hivi?

Leo ni karibu siku ya tatu napokea ujumbe wa ajabu ajabu kutoka namba 15556,na kila wakikutumia wwanakata tsh 500.

Hii huduma mimi sijajiunga na after all mambo wanayotuma ni ya kijinga na kitoto amabayo mimi siyaitaji, mfano leo wamenitumia ujumbe huu na kunikata tsh.500

" Withney death authorities believe huston may have fallen asleep or lapsed into unconsciousness in the bathtub drowened.water has been found in her lungs"

habari hii si kwamaba mimi naifahamu tu na nilishaisoma kwenye mtandao tmz,wamekopy maneno yote msitari baada ya msitari kutoka mtandao huu,na hawakuonesha source kwamba wametoa kwenye mtandao huu.

Pili habari ni yauongo si ya kweli kwani taarifa rasimi juu ya kifo ya whitney hazijatoka na itachukua wiki mbili mpaka tatu.

Hii authority wanaosema imetoa taarifa hii ni ipi na wao wanauhakika nao upi? Na je wana mamlaka ya kisheri ya kusamabaza habari hizi kwamaba ni rasimi whitney kafa kwa kuzama kwenye maji?

Sasa ninafungua kesi kubwa ya madai amabayo itakua mfano katika nchi hii na fundisho kwa haya makapuni ya simu,niko tayari hata kutumia senti yangu ya mwisho kwa hili.

Unafungua lini na wapi tuungane mkuu. Mi na ushahidi hapa full wa wizi wa hawa watu.
 
Back
Top Bottom