Tigo acheni wizi wa kijinga,nafungua kesi ya madai

Kwa kweli tigo ni wizi lakini si kiivyo yaani wakuchague wewe tu ndio, mbona sisi hawatuibii kiivyo, mimi ninavyoona wewe ulikuwa unawaibia zamani so na wao wameamua kukuibia kwa sasa, yaani wewe simu yako imeonekana ipo bize wakati wa usiku tu (muda wa ofa tu) sasa wameona hiyo ndio njia mbadala la kuchukua hela yao, Pole bro mimi niliwapaga kubwa mpaka leo full respect
 
nimetuma 100000 to a wrong number kwenye akaunti ya tigopesa wameniambia watanirudishia,yamepita masaa sita sasa,ingawa ni kosa langu lakini wamenihakkshia watairudisha
 
Uliruhusu mwenyewe kupata msg za namna hiyo...Hawawezi kuanza kukutumia usipo'ratify!
Tafuta namna ya ku'unsubscribe!

mkuu, nadhani jamaa yuko right kwa kuwa hata mimi ishanitokea hivyo mara kadhaa bila hata ya kujiunga, nime unsubscribe mara mbili ndio ikaacha, nilipo unsubcribe mara ya kwanza ilikuja message kusema nimejitoa lakini bado wakaendelea kutuma taarifa zao tena huku wakikata hela zangu, hawa tiGO sometimes ni ovyo sana!
 
Tigo wazinguzi yaani kama hizo caller tunes wanakuchomekea bila kujua!!!mbaya zaidi unakuta caLler tune haiendani nawe!ni kudhalilishana kwa wanaokupigia...
 
Kweli mdau hawa ni wezi wakubwa sana na ajabu watu tuko kimya kabisaa...
ninaandika hoja hii kwa masikitiko makubwa hasa baada ya kushuhudia viwango vya gharama ya kupiga simu vikipanda kinyemela bila kutangazwa. Kwa mfano tigo wanajinadi kila siku kuwa gharama ni sh 1 kwa sekunde ilihali si kweli hata kidogo. Hebu wadau jaribuni kutia elfu 1 kwenye simu yako ya tigo halafu mpigie mtu mwenye tigo uone kama utaongea hata dak 6. Ni wizi wa mchana kweupe jamani wana jf tupige kelele hii hali itoweke au watangaze hizo bei zao mpya. Ni wizi kama mafisadi wengine.
 
mdau nitakupm nikupe maelezo,ahsante sana kwa kuniunga mkono na wengine wote wenye ushaidi tuungane tufanye kitu kikubwa,nazani hawa Tigo hawajasikia kuna kampuni y asimu ililipiswa mamilion kwa kudanganya tu wateja uwezo wa mtandao kufikisha mawasiliano kwa haraka.lazima tufanye kitu kwani njia moja wapo ya kupatikana kwa sheria ni kutokana na maamzi ya mahakama,itaokoa vizazi vijavyo pia.
Unafungua lini na wapi tuungane mkuu. Mi na ushahidi hapa full wa wizi wa hawa watu.
 
Hamna tigo siku hizi utakuta watu wakikupigia simu wanasikia miziki ya ajabu ajabu ni upumbafu sana huu na uporaji wa mali za wananchi.

Uliruhusu mwenyewe kupata msg za namna hiyo...Hawawezi kuanza kukutumia usipo'ratify!
Tafuta namna ya ku'unsubscribe!
 
mkuu hata mimi ndio walichofanya,halafu bahati mbaya zaidi msg yenyewe inatoa ujumbe wa uongo kuhusu whitney na wamecopy huo ujumbe kutoka mtaandaoni na wao wanamamlaka yapi ya kisheria kutoa taarifa ya sababu ya kifo cha mtu?
Yaani jana tu mie pia wamenitumia hiyo message ya kifo cha whitney na wala huduma yenyewe sikujiunga
 
Wadau...mjanja kuibiwa ni aibu..! Ni kuwapiga chini tu...! Wizi wao umekuwa zaid ya VODA sasa!
 
Back
Top Bottom