Hongera zake. Lakini wanaompongeza leo na kudai TBC1 sasa imekaa kimagamba ndiyo hao waliomtukana na kutishia kumuua mwandishi wa TBC1 pale viwanja vya jangwani wakidai Tido na TBC yake wanatumiwa na CCM! Hata hivyo mimi sijui kelele za Tido kuonewa zinatoka wapi kwa sababu huyu bwana alikuwa na mkataba ambao ulikuwa unaonyesha wazi mwisho wake na aliondoka baada ya mkataba huo kufika mwisho na ilikuwa ni hiari ya mwajiri wake kuendelea nae kwa kumpa mkataba mpya au kuachana naye kama ilivyotokea. Sasa hizi kelele kana kwamba amefukuzwa kazi au mkataba ake kukatizwa kabla ya muda zinatoka wapi? Tujifunze kupata facts kabla hatujaanza kushutumu mamlaka ya uteuzi kwa sababu tu tuna mapenzi na mlengwa na chuki dhidi ya utawala!