Tido Mhando atemwa TBC

Tido Mhando atemwa TBC

Sijawahi kupata ghadhabu kama kujadili na kuzipa uhai hoja ambazo siyo issues. Suala la Tido Mhando ni non-issue na yeye Mhando anajaribu kutafuta sympathy ya watu wakati yeye anajua kabisa kwamba mkataba wake ulikuwa for a definate period of time. Alijua kwamba kufika tarehe 15 Desemba anataikwa kuondoka, unless kun express renewal ya mkataba wake au hata express intention ya hiyo renewal. Sasa ni ajabu mtu anayejua kwamba anaondoka anaendelea kubaki akivizia kuona kama ataambiwa baki. Angekabidhi ili hata kama anarejea akabidhiwe na kuendelea. Halafu eti watu wanadai amefanya mengi. Ni sawa lakini ndiyo sababu alitafutwa mtu wa aina yake na kulipwa malipo manono kufanya hicho alichofanya (that is what he was contracted to do and that is what he was paid for).

Tido asijifanye ni indispensable. Halafu tujiulize: Huyu bwana anataka aje apumzike lini baada ya utumishi wa zaidi ya miaka 35? The guy is well in his sixties. Hakuna njama wala zengwe. Kamaliza mkataba aishie zake ili watanzania wengine waendeleze yale aliyoyaanzisha ili akumbukwe na vizazi vijavyo.
 
Mimi nafikiri atafuata hoseah wa PCCB maana kamchafua JK kinoma kwa kuanika habari kwa Viongozi wa marekani na Wikileaks kuziweka kwenye mtandao wao juzi.

Peoples power
 
Ila kweli, Hosea nae anaingia kwenye list, anajaribu kujitetea kwa JK lakini utetezi wake ni wa mfa maji. Hayo aliyosema ni ya kweli, nafikiri Hosea angejipongeza kwa kusema kweli kuwa JK ni kikwazo.
 
Hebu watanzania tuache cheap politics

Kilichomuondoa Tido sio CCM, nakumbuka hapahapa jamvini in august to november tuliona jinsi TBC walivyomnyima slaa time kabisa na exposure kwa wapiga kura, tuliona hotuba ilivyokatwa na hata kuona namna ambavyo walikua biased

ni utoto na upuuzi kusema ati hakuipa ccm sapoti, he has left the way he came in

Kuhusu mwema, he has done more than anyone to support CCM, watu lazima muelewe kwamba sapoti si virungu tu, ni hata kulinda mafisadi wasidhurike kwa namna yoyote.... nani amesahau jeshi lilivyochangia kuharibu matokeo popote pale chadema walioonekana kushinda?? the issue hapa ni kwamba sehemu kama mwanza na arusha the people's power was way beyond any control otherwise wangekufa mamia kama si maelfu na ocampo angekua anakuja kutembea mbugani kila baada ya miezi mitatu

sijui huwa tuna-analyse vipi mambo sisi watanzania

disappointing indeed
 
Sijawahi kupata ghadhabu kama kujadili na kuzipa uhai hoja ambazo siyo issues. Suala la Tido Mhando ni non-issue na yeye Mhando anajaribu kutafuta sympathy ya watu wakati yeye anajua kabisa kwamba mkataba wake ulikuwa for a definate period of time. Alijua kwamba kufika tarehe 15 Desemba anataikwa kuondoka, unless kun express renewal ya mkataba wake au hata express intention ya hiyo renewal. Sasa ni ajabu mtu anayejua kwamba anaondoka anaendelea kubaki akivizia kuona kama ataambiwa baki. Angekabidhi ili hata kama anarejea akabidhiwe na kuendelea. Halafu eti watu wanadai amefanya mengi. Ni sawa lakini ndiyo sababu alitafutwa mtu wa aina yake na kulipwa malipo manono kufanya hicho alichofanya (that is what he was contracted to do and that is what he was paid for).

Tido asijifanye ni indispensable. Halafu tujiulize: Huyu bwana anataka aje apumzike lini baada ya utumishi wa zaidi ya miaka 35? The guy is well in his sixties. Hakuna njama wala zengwe. Kamaliza mkataba aishie zake ili watanzania wengine waendeleze yale aliyoyaanzisha ili akumbukwe na vizazi vijavyo.
thanks mkuu

nahisi kama kuna watu wana mamatizo either ya umri au uelewa...

cheers
 
HOsea Kwishney .Jk sio kama ana visasi ni kwamba amezungukwa na watu amboa wanajipendekeza kwake nakujifanya wazuri kwake na yeye kuwaamini na kudhani ni watu wake na kuja kugundua ni sio watu wanao mkubali ni wana jipendekeza na kumsema vibaya pembeni, hata mimi ninge piga kisasi vile vile.
 
Tido; Hosea kuondolewa!...........good riddance shida ni kwamba successors wao hawana neema yoyote kwa Watanzania!
 
Awe kaondolewa au namna gani ...he deserve
  1. alsha jishushia heshma kuwatumikia mafidsadi
  2. mungu hamfichi mnafiki
  3. kwa heri tido .....uliyegeuka kuwa toothless bull dog!
 
Mkuu JK ni mtu wa visasi na ktka hili hana aibu. Kumbuka alivyoingia '05, akina Mashishanga, Mangula at al walienda wapi? Ukubali ukatae huyu ndiyo JK na Visasi na vipenzi vyake ni watu wanaofikiri baada ya kusema/kutenda kama Makamba, Kombani, Shimbo na wengine wengi

Mkuu kwa hao wengine hakuna mwenye ushahidi zaidi ya nadhari, chuki, kukata tamaa zilizojaa vichwani mwa wafikirika (oooh no, wa TZ wachache) kwani hata uwe Malaika lazima utalalamikiwa tu kuwa umemuacha Fulani na umempendelea fulani, nashauri KATIBA ijayo kama kutakuwa na muafaka wa kuunda upya tuweke kipengele cha kuwa WaTZ wote tupate nafasi ya uongozi, nadhani hili litakwisha na kuhusu swala la TIDO jamani mkataba umekwisha na Tido analijua hili zingekuwa Nchi za wenzetu huyu bwana angeshitakiwa kwa njinsi alivyoiacha TBC mitambo ya radio za FM uwezo wake wa kufanya kazi umeshuka, pamoja na kushauriwa lakini hataki kununua spare aondoke tu na safi sana MUUNGWANA na sasa weka Jimama hapo uzidishe History on gender may be Heda Sanga huyu mama ni mchapa kazi na hataki masihara she is very fair ON
 
..huyu si ndiyo alikuwa anawakatia mawasiliano/matangazo Chadema wakati wa mkutano wa kampeni.

..halafu akamuacha Mkapa akitamba na kutoa maneno ya ajabu-ajabu wakati wa mkutano wa CCM.

..sasa leo amefutwa kibarua tayari wananchi mnamuonea huruma.

..huyo ameshakula ameshiba na kuvimbiwa, sasa ampishe mwana CCM mwingine mwenye njaa aingie hapo.

..kutesa kwa zamu nchi hii, lakini lazima uwe CCM.
 
Hapo kwenye red. Ni kweli kabisa huyu jamaa alijifanya mungu-mtu pale TBC akawatesa vyama vya upinzani na hasa Chadema. Sasa yamemfika watu wanamuonea huruma. Ni ajabu sana. Huyu hapaswi kuonewa huruma huyu!! Hana tofauti na wale waliomtoa kibaruani. Suala lake ni sawa na suala la majizi. Majizi yakiwa kwenye mipango ya kuiba huwa yanashirikiana sana. Lakini yakishapata nyara huwa urafiki unaisha - yanadhulumiana nyara na kuumizana hata kuuana. Mwizi mdhulumaji na mdhulumiwa hawana tofauti. Wote ni waovu. Period!
 
Kimatendo mnamkubali JK ila kwenye kusema mnafanya kinyume chake na pia chuki zimewajaa.
Huyo Mwema kajiweka mwenyewe tu hapo? Sio chaguo la JK? Anatekeleza maamzi ya nani? Ndo maana wakati mwingine huwa natumia lugha ya ukali ili angalao mijitu ielewe.
JK ni muungwana sana na ndo maana uongozi wake upo tofauti sana na mtangulizi wake.
Upinzani haukua ICU kabla ya kuja JK? Kuweni wakweli otherwise shame on you.
You need big help!
 
Mkuu JK ni mtu wa visasi na ktka hili hana aibu. Kumbuka alivyoingia '05, akina Mashishanga, Mangula at al walienda wapi? Ukubali ukatae huyu ndiyo JK na Visasi na vipenzi vyake ni watu wanaofikiri baada ya kusema/kutenda kama Makamba, Kombani, Shimbo na wengine wengi

mseme Brigedia Ngwilizi waliokosana tangu wakiwa jeshini na visa vieliendelea hadi leo!!!!! Jk ni mtu wa visasi sana.
 
Mkuu Acid hilo ni gogo la neno! We should pick an issue where there is none! Tido should get to terms with reality.
 
Wana Jf
Nilikuwa siamini kama mchapakazi na mzoefu ktk maswala ya utangazaji hapa Tanzania kashindwa kazi Tbc,lakini baada ya kusoma gazeti la Mwananchi nimetambuwa kuwa Kamanda Tido Mhando ametolewa Tbc baada ya kuruhusu habari za uwazi na ukweli kutangazwa ndani ya Tbc pasipo na upendeleo wowote
inasemekana kuwa bwana Tido mhando imeisababishia serikali ya CCM kupata kura chache baada ya kuruhusu mambombalimbali ambayo ni ya kweli kutangazwa TBC na watu kujuwa ukweli kumekuwepo na wasiwasi serikalini ya kwamba Tido amehusika katika kuifanya TBC itangaze matukio yaliyoikera wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa jana.

Nime amini hii nchi ukiwa mkweli na muwazi juwa kuwa siku zako zahesabika

mapinduziiiii daimaaaaaa
 
Kwa wiki 3 tatu tangu aondoke huoni TBC inavyopanda chati katika hahari za udaku siku hizi na zile za CCM?
 
Back
Top Bottom