Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Mkuu,
Asante sana kwa kutukumbusha wengu tulio na ugonjwa wa kuajiriwa! Na hapo nimemkumbuka kamanda mkuu wa kuajiriwa Tanzania, Dr. Idrisa Rashid. Alitokea BOT akaenda Akiba comercial Bank kisha akahamia Vodacom kabla hajatua Tanesco. Kwa sasa yuko Amana bank....
 
Kweli aisee! Dizaini kama ananyanyasika huyu mshikaji wakati ana CV ya kufa mtu. Bora aende kwenye media za mbele.
 
Cennection ipi hiyo mbona siikamati vizuri hebu funuka kidogo
Ni habari za magazetini asubuhi hii inawezekana kabisa kuna connection na skendo ya kaburi la Balali.

=====
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. “Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri,” alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu,
Asante sana kwa kutukumbusha wengu tulio na ugonjwa wa kuajiriwa! Na hapo nimemkumbuka kamanda mkuu wa kuajiriwa Tanzania, Dr. Idrisa Rashid. Alitokea BOT akaenda Akiba comercial Bank kisha akahamia Vodacom kabla hajatua Tanesco. Kwa sasa yuko Amana bank....

Daaaah! Mkuu nimekukubali!
 
abdla majura ameweza kuwa na redio yake

Hata Le Mutuz naye ana mpango wa kufungua chombo chake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu,
Asante sana kwa kutukumbusha wengu tulio na ugonjwa wa kuajiriwa! Na hapo nimemkumbuka kamanda mkuu wa kuajiriwa Tanzania, Dr. Idrisa Rashid. Alitokea BOT akaenda Akiba comercial Bank kisha akahamia Vodacom kabla hajatua Tanesco. Kwa sasa yuko Amana bank....

Akiba na Amana bank kote ana hisa nyingi pia ni mkurugenzi muanzilishi.kwa hiyo ni kama anafanya kazi katika kampuni yake
 
Man sio lazima kila mtu awe mchuuzi; maisha hayana formula moja, hivi kama uncle Tido akijoin Aljazeera! monthly package yake per month/year na makando kando inamtosha kustaafu raha mustarehe after only two years! Abdalah majura na redio mbao yake anapata shilingi ngapi kwa mwezi kama sio stress tupu na kero za michango ya CCM kila siku.

Kwa mtu mtaalamu kama Tido inatosha kuuza utaalamu wake ukaachana na kero za uchuuzi njaa hapa bongo.

masifa ohh mimi ni Managing Director, mimi ni Chief Executive Officer; ohh mimi ni Chief Operating officer wa kampuni ABC; mapato kwa mwaka laki 6!

Forsa Tido; go Tido

Aljazeera idhaa ya kingoni au? Kiingereza kimo mle mpaka aende Aljazeera? Msitake kuchuma dhambi bure jamani
 
Tido anakwenda kugombea ubunge Muheza Tanga. ataupata tu maana aliyepo ni wale wale wa kupewa lift na kuomba apige honi.

Ahahahaaaaa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Aljazeera idhaa ya kingoni au? Kiingereza kimo mle mpaka aende Aljazeera? Msitake kuchuma dhambi bure jamani

Kufanya kazi Aljazeera siyo lazima uteme ungege kama umezaliwa UK. Mbona akina Mohamed Adow nk wanaongea kiingereza cha kisomali tu. acha kujishusha wewe kaka
 
004.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai. Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Nashauri sana huyu mzee aachane na suala la kuajiriwa.kila anachoanzisha amalizi miaka 10,kwa nini? ana matataizo gani? mbona mwenzake abdla majura ameweza kuwa na redio yake hapa Dodoma?

Kinachotakiwa ni hela tu sio swala la kuajiliwa au kujiajiri boss
 
Story fake ya Balali ndio imemng'oa nini?dah!!
 
tido+mcl.gif

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando akizungumza na wafanyakazi wa MCL jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory

KWA UFUPI
Mkurugenzi huyo mtendaji ameitumikia kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa miaka miwili na nusu.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. "Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri," alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.chanzo.Tido Mhando aaga Mwananchi - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Back
Top Bottom