Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,548
Reaction score
860,660
Ni habari za magazetini asubuhi hii inawezekana kabisa kuna connection na skendo ya kaburi la Balali.

============================


tido+mcl.gif


Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. "Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri," alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.


Chanzo: Mwananchi

 
Wengine huku magazeti yanafika baada ya siku mbili ungefafanua zaidi,
 
Kaachwa au kaamua kutoongeza mkataba anyway ni nguli katika mashirika makubwa ya kimataifa ya habari mwananchi ilikuwa inampunguzia covarage wamuweke francis nanai jembe
 
Ni habari za magazetini asubuhi hii inawezekana kabisa kuna connection na skendo ya kaburi la Balali

Tido mhando aliekuwa mkurugenz.i wa magazeti ya mwananchi,jana amewaaga wafanyakazi wa gazeti la mwananchi baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka 2 na Nusu.
 
Namshangaa sana Tido kwa weledi alionao na alivyo mbobezi ktk fani ya habari anashindwaje kujiari akaanzisha shughuli yake inayohusiana na fani yake ili ajiari mwenyewe?
 
ukiona hvyo kashamaliza kazi yake ya ushushushu aliyotumwa na....... dhidi ya gazeti la wakenya,teh teh teh teh,chezea inteligensia niniiiiii,hahahahaaaaaaa
 
soma mwananchi online wangu, huyo kasikia sasa hivi tu kafungua uzi awe wa kwanza.

We mama mwananchi wanalipost online kuanzia saa saba mchana sio kama daily news wanaopost saa sita usiku siku ikianza.
 
Hata hivyo miaka yake 2 imeleta mabadiliko makubwa sana.
 
Afadhali maana credibility yake na Gazeti lenyewe imeshuka,Mwananchi kutoka kuwa gazeti mahili kwa umakini hadi kuanza kufuata njia ya propaganda kama Jambo Leo na Uhuru kwa tofauti ndogo tu!!!

Kuaga kwake kwa kuisha mkataba ina maanisha kuwa hamna ufanisi mathubuti katika uongozi wake,kwa kifupi kafeli na inabidi aondoke,bado Neville Meena baada ya Denis Msacky kukimbilia kwa Rostam maana Meena pia ni wa CCM!!
 
Back
Top Bottom