Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

nategemea Mwananchi itaendelea walau zaidi ya sehemu nzuri alipoiachia, ikitetereka nntalipotezea kama mengine tu
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu. Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. "Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri," alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Kapumzike salama ukizingatia hawakukupa nafasi ya kuitenda kazi yako vyema.
 
Kuna watu watashangilia sana kuondoka kwake!
 
hivi karibuni Tido alihojiwa kwenye kipindi cha Mcheza Kwao Star Tv akasema baada ya mkurugenzi aliyepita Sam Shollei kuondoka, Mwananchi walimuomba achukue nafasi ya ukurugenzi kwa muda.
 
Duh, jembe linaondoka MCL, sijui sasa upepo utaelekea wapi.
Labda tu nimshauri nguli huyu aanzishe chombo chake cha habari yaweza kuwa gazeti au hata redio....
 
Alianza vizuri ila siku za mwishoni gazeti la mwananchi limegeuka kuwa kama la Shigongo!
 
Barabara mulefu haikosi kona, na mwanamuke muzuri hakosi kasoro. Pombe nayo sio chai. Statistical explanations states that a normal curve is like a doom. It gradually rises up and there is a peak at which that line can no longer raise, rather it falls down naturally Muzee Mhando is accepting the natural phenomenon of a normal curve. Aliiumba upya TBC mpaka ikawa kama BBC mpaka walongozi wake wakamuchukia na kumupiga chini kiaina. History is a very good teacher, Musolin once munyama wa dunia became no more, wako kina Lenini na Urusi, Hitler na Ugerumani, Tharcha chuma cha pua na Marekani haitapona kama Roma the world giant alivyoumbuka.

Weldone Mhando because retiring in peace is worth than being stamped down while you look for a window to escape through! Ng'walimu Nyerere showed us a way to step down kwa furaha, NG'ATUKA sio kufanana na yule bana kuba ya Libya, Museveni kafungwa kitambaa cheusi usoni kama alivyo Mugabe.

Kuwa mwafrika ni kazi kwelikweli, Byebye Mhando, bado una nguvu unawezaomba mahali pengine kwani track record yako is byeeeeee!
 
Afadhali maana credibility yake na Gazeti lenyewe imeshuka,Mwananchi kutoka kuwa gazeti mahili kwa umakini hadi kuanza kufuata njia ya propaganda kama Jambo Leo na Uhuru kwa tofauti ndogo tu!!!

Kuaga kwake kwa kuisha mkataba ina maanisha kuwa hamna ufanisi mathubuti katika uongozi wake,kwa kifupi kafeli na inabidi aondoke,bado Neville Meena baada ya Denis Msacky kukimbilia kwa Rostam maana Meena pia ni wa CCM!!

Mh! Majungu haya
 
Mh! Majungu haya

Utake usitake ufanisi wa Mwananchi siku hizi ni questionable,hivi unafahamu Salva wa Ikulu kabla ya kupewa ukurugenzi na Kikwete alikua gazeti gani na alitumika vizuri kuwachafua wakina Sumaye na Salim Ahmed Salim??!!

Unafahamu kuwa Sumaye aliitisha press conference kulaani Msaka uraisi/wana mtandao kutumia kalamu kuwachafua wapinzani wake na akaonya kuwa hajapata uraisi anatumia kalamu,akiupata atatumia risasi??!!

Unafahamu kuwa Salim Ahmed Salim aliandikwa mfululizo hadi na picha za Adobe shop akishikana mikono na viongozi wa Hizbu na wakaandika pia alishiriki kumuua Karume Sr??!!

Unafahamu kuwa wakati Mwangosi alipouwawa jukwaa la wahariri lilipitisha azimio la kutoshirikiana na Waziri wa Mambo ya ndani ambae alikuwa ni Emanuel Nchimbi lakini akaja akaalikwa na Neville Meena pale mnazi mmoja na kuzusha timbwili??!!
 
Barabara mulefu haikosi kona, na mwanamuke muzuri hakosi kasoro. Pombe nayo sio chai. Statistical explanations states that a normal curve is like a doom. It gradually rises up and there is a peak at which that line can no longer raise, rather it falls down naturally Muzee Mhando is accepting the natural phenomenon of a normal curve. Aliiumba upya TBC mpaka ikawa kama BBC mpaka walongozi wake wakamuchukia na kumupiga chini kiaina. History is a very good teacher, Musolin once munyama wa dunia became no more, wako kina Lenini na Urusi, Hitler na Ugerumani, Tharcha chuma cha pua na Marekani haitapona kama Roma the world giant alivyoumbuka.

Weldone Mhando because retiring in peace is worth than being stamped down while you look for a window to escape through! Ng'walimu Nyerere showed us a way to step down kwa furaha, NG'ATUKA sio kufanana na yule bana kuba ya Libya, Museveni kafungwa kitambaa cheusi usoni kama alivyo Mugabe.

Kuwa mwafrika ni kazi kwelikweli, Byebye Mhando, bado una nguvu unawezaomba mahali pengine kwani track record yako is byeeeeee!

mkuu nimependa filosofia na saikolojia ndani ya mawazo yako kama picha uipatayo ukimdadavua Mzee Mhando, nimefurahi pia kwa mu_afrika kujipima kwa kiwango cha dunia na pia umetukumbusha kiswahili ni lugha ya afrika na lugha ya weusi amerika hivyo ni deni kwetu kuikuza huko kote kwa kuongea na kuandika, tukianzia afrika ya kati.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. “Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri,” alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Gazeti La Mwananchi Kwa Sasa Ni Kama Kijalida Cha Lumumba. Nimeacha Kununua Magazeti Siku Hizi. JAMIIFORUMS YATOSHA MAGAZETI YA NINI?
 
004.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai. Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Nashauri sana huyu mzee aachane na suala la kuajiriwa.kila anachoanzisha amalizi miaka 10,kwa nini? ana matataizo gani? mbona mwenzake abdla majura ameweza kuwa na redio yake hapa Dodoma?
 
Hongera tido kwa kumaliza mkataba wako kwa mafanikio hukutetereka wala huku walamba miguu wanasiasa ambao no waharibifu wakubwa was Tania ya habari Mungu akubariki
 
Mkurugenzi huyo mtendaji ameitumikia kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa miaka miwili na nusu.

Habari Kamili Gonga hapa Chini.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Tido-Mhando-aaga-Mwananchi/-/1597296/2385618/-/baavb6/-/index.html

My Take

Mwananchi limeshapoteza Credibility yake kwa kiasi kikubwa sana.
Sasa wako Busy na Habari ya Kaburi la Balali.
Na wamemtuma mtu Kabisa Marekani na umpilia Malazi na Per Diem kwenda kuona Kabuli la Balali na ku estimate Gharama ya Kaburi lenyewe.
Ningeshangaa sana kwa Mtu Makini Kama Tido Muhando kuendelea kuwa sehemu ya huu upuuuzi tena katika Nafasi ya Juu Kabisa
 
Gazeti La Mwananchi Kwa Sasa Ni Kama Kijalida Cha Lumumba. Nimeacha Kununua Magazeti Siku Hizi. JAMIIFORUMS YATOSHA MAGAZETI YA NINI?

Mukubwa nasikia eti mwananchi ndilo limekua habari ya mujini eti kwa kuleta zile porojo za kaburi hewa la balali? Usilitose bwana waunge mkono maana sasa wamekaribia vile viwango vyetu bora kabisa vya habari leo nk nk. Wanadai eti Mhando hana viwango bora kabisa vya kusimamia ubora wa hali ya juu kama ule wa uhuru. Wasemaje ndugu?
 
Back
Top Bottom