Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Tido Mhando amaliza mkataba wake Mwananchi

Mkurugenzi wa Mwananchi Communications ltd ameamua kuondoka katika kampuni hiyo kutokana na habari za kusadikika juu ya kifo cha dr. Balali aliyekuwa gavana wa tz zinazoendelea kuripotiwa na gazeti la mwananchi.
 
Bado...Jaribu kuweka nyama ili ujumbe ufike kikamilifu
 
inawezekana ikawa kweli sababu Tido asingeikubali habari nyepesi kama ile ichapwe na kutolewa!
 
Mkataba wake unaisha mwisho wa mwezi huu acha maneno ya vijiweni
 
Kamanda wangu Mbowe changamka Tafadhari Jembe hilo linahitajika hapo Tanzania daima.

BACK TANGANYIKA
 
Bado...Jaribu kuweka nyama ili ujumbe ufike kikamilifu
Unataka nyama? Subiri ntakuwekea ya kutosha. Ila fahamu tu kuwa hayupo tena Mwananchi amejiondoa kwenye ripoti za utata juu ya kifo cha Balali.
 
Tido alijichanganya toka kipindi kile anambeba msaliti zzk na kuikandia chadema,kupitia kale kamwandishi.
Halafu huwa nashangaa sana,kwanini gazeti la mwananchi pekee huwa linapatikana maktaba za Tanzania
 
Man sio lazima kila mtu awe mchuuzi; maisha hayana formula moja, hivi kama uncle Tido akijoin Aljazeera! monthly package yake per month/year na makando kando inamtosha kustaafu raha mustarehe after only two years! Abdalah majura na redio mbao yake anapata shilingi ngapi kwa mwezi kama sio stress tupu na kero za michango ya CCM kila siku.

Kwa mtu mtaalamu kama Tido inatosha kuuza utaalamu wake ukaachana na kero za uchuuzi njaa hapa bongo.

masifa ohh mimi ni Managing Director, mimi ni Chief Executive Officer; ohh mimi ni Chief Operating officer wa kampuni ABC; mapato kwa mwaka laki 6!

Forsa Tido; go Tido
 
Tido anakwenda kugombea ubunge Muheza Tanga. ataupata tu maana aliyepo ni wale wale wa kupewa lift na kuomba apige honi.
 
mi nafikiri kwa jinsi tido alivokua amepata exposure ya kutosha hususani katika tasnia ya habari basi nadhani lipo jambo ambalo amepanga na watanzania tutalishuhudia soon
 
Man sio lazima kila mtu awe mchuuzi; maisha hayana formula moja, hivi kama uncle Tido akijoin Aljazeera! monthly package yake per month/year na makando kando inamtosha kustaafu raha mustarehe after only two years! Abdalah majura na redio mbao yake anapata shilingi ngapi kwa mwezi kama sio stress tupu na kero za michango ya CCM kila siku.

Kwa mtu mtaalamu kama Tido inatosha kuuza utaalamu wake ukaachana na kero za uchuuzi njaa hapa bongo.

masifa ohh mimi ni Managing Director, mimi ni Chief Executive Officer; ohh mimi ni Chief Operating officer wa kampuni ABC; mapato kwa mwaka laki 6!

Forsa Tido; go Tido

Uko sawa,siyo kila mtu anaweza kujiajiri.
 
Ni habari za magazetini asubuhi hii inawezekana kabisa kuna connection na skendo ya kaburi la Balali.

=====
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando amewaaga wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu.

Mkataba wa Tido katika kampuni ya Mwananchi utafika kikomo mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Nation Media Group (NMG), Linus Gitahi kwa wafanyakazi wote wa Afrika Mashariki ambako kampuni hiyo inamiliki vyombo vya habari, inasema Mhando anaondoka MCL huku akiacha mafanikio makubwa katika nyanja zote na kwamba atakumbukwa kwa mchango wake.

MCL ni kampuni tanzu ya NMG inayochapicha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010. Awali alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la BBC (1999-2006).

Mhando aliiwezesha MCL kukua kwa kasi kubwa katika mapato na katika mpango wa uchapishaji wa magazeti ya MCL Kanda ya Ziwa ambako wakazi wa mikoa hiyo sasa wamekuwa wakisoma magazeti asubuhi tofauti na zamani.

Wafanyakazi wa MCL walimpongeza kwa kuboresha masilahi yao kwa kipindi cha uongozi wake na kuandaa misingi bora ya uongozi, ikiwamo kumwandaa mrithi wake.

Akiwaaga wafanyakazi jana asubuhi, Mhando aliwashukuru kwa ushirikiano wao pia alisema amejifunza mambo mengi mapya, ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi alikuwa kwenye sekta ya habari ya utangazaji tofauti na uchapishaji. “Safari hii ilinipa uzoefu mpya na wenye changamoto nyingi lakini kupitia ushirikiano wenu wa dhati tulifanikiwa kuiweka kampuni katika hali nzuri,” alisema Mhando.

Gitahi alisema nafasi ya Mhando itachukuliwa na aliyekuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (COO), Francis Nanai.

Nanai alijiunga MCL , Agosti mwaka jana akitokea Kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement (Lafarge Tanzania) ya mkoani Mbeya akiwa Mkurugenzi wa Biashara.

Chanzo: Mwananchi
Balali anaingiaje hapo? Imeshaelezwa kuwa mkataba wake umeisha, sasa tatizo liko wapi? Hiyo hadithi ya Balali ni ya kusadikika tu wanaojua ukweli na undani wake ni wale jamaa wa EPA. Bosi wao si ulimsikia akisema wenzake watakorudisha atawasamehe? Sasa wewe unawajua |"waliorudisha na kiasi walichorudisha?" Hiyo si siri yake na washkaji zake? Na hilo la Balali tumwachie yeye! Hii ni Danganyika mkuu!
 
Back
Top Bottom