Ticha amchinja mwanafunzi

Ticha amchinja mwanafunzi

Kwa mfano kamchinja mtoto aliyeitwa Ally Thabit una maoni gani???!!!!

huku usukumani jina ni jina tu, kuna jirani yangu anaitwa Masoud Khalfan hajuhi kitu kinachoitwa msikiti wala kanisa. Mjomba wanu anaitwa Yasin Shitungulu, hilo jina la Yasin alipewa na baba yake kama ukumbusho wa daktari wa mifugo wa wilaya aliyewafundisha wanakijiji dalili za ugonjwa wa sotoka!
 
O_0oh! kumbe haujanielewa toka mwanzo, SITETEI DINI YOYOTE, infact kila siku huwa nasema UKRISTO+UISLAM=MAJANGA
Kama ulidhani uko kwenye ubishi wa kishabiki wa mkristo na muislam who is better you are wrong bro, mimi si mkristo wala si muislam, kwa hiyo tunapojadili ondoa mawazo ya kidini, kuwa na fikra huru!

1. Hamna ubishi wa kishabiki wala dhana ila ni uhalisia wa mawazo yako na yangu as we deduce from our knowledge; hivi makundi uliyotaja ya kigaid yanagawanyika kwa dini ngapi???!!!!!

2. Yaaani muda wote huu na wewe unamjibu mtu asiyeelewa,insult to OUR cognitive abilities!!!!!!

3. Kama ukristo na uislamu wote majanga ila una evidence ya majanga ya kiislamu na si ya kikristo then hapa unamaanisha ni majanga ya uislamu sababu unaweza ku substantiate hilo!!!!!! I stand to be corrected!!!!

4. Well mimi ni muislamu ila nimesoma darasani maandiko ya Emile Durkhein na Karl Marx juu ya dini na imani so kama ni fikra huru hapa zipo tena za kusoma sio za "kiimani" mkuu!!!!!!!!

5. Unasema huangalii which is better may be; uoiwezaje kujua kuwa zote majanga wakati hyo ni nominal scale tayari, ilipataje hiyo conclusion bila ya kuzipima???!!!!


Lete hoja!!!!!!!
 
huku usukumani jina ni jina tu, kuna jirani yangu anaitwa Masoud Khalfan hajuhi kitu kinachoitwa msikiti wala kanisa. Mjomba wanu anaitwa Yasin Shitungulu, hilo jina la Yasin alipewa na baba yake kama ukumbusho wa daktari wa mifugo wa wilaya aliyewafundisha wanakijiji dalili za ugonjwa wa sotoka!

Nashukuru sana mkuu na nimefurahi kusoma kuwa kuna watu wanaoweza kukaa na kujua hizi labelling ni muendelezo wa imani au dini ambazo kwa undani wake bado tunaweza jikuta kundi ambalo kama angepewa options asingechagua!!!!!!
 
So sad!
Yaani hata binadamu anaelekezwa kibra na kuchinjwa? I wish huyo ticha angehojiwa kwanza na kupimwa akili kabla hajauwawa.
 
1. Hamna ubishi wa kishabiki wala dhana ila ni uhalisia wa mawazo yako na yangu as we deduce from our knowledge; hivi makundi uliyotaja ya kigaid yanagawanyika kwa dini ngapi???!!!!!

2. Yaaani muda wote huu na wewe unamjibu mtu asiyeelewa,insult to OUR cognitive abilities!!!!!!

3. Kama ukristo na uislamu wote majanga ila una evidence ya majanga ya kiislamu na si ya kikristo then hapa unamaanisha ni majanga ya uislamu sababu unaweza ku substantiate hilo!!!!!! I stand to be corrected!!!!

4. Well mimi ni muislamu ila nimesoma darasani maandiko ya Emile Durkhein na Karl Marx juu ya dini na imani so kama ni fikra huru hapa zipo tena za kusoma sio za "kiimani" mkuu!!!!!!!!

5. Unasema huangalii which is better may be; uoiwezaje kujua kuwa zote majanga wakati hyo ni nominal scale tayari, ilipataje hiyo conclusion bila ya kuzipima???!!!!


Lete hoja!!!!!!!

Sasa hivi, wakristo wengi sana ndio magaidi. E.g huko Africa ya Kati, kikundi cha Wakristo kinachinja waislamu kwa kasi ya ajabu!
 
Sasa hivi, wakristo wengi sana ndio magaidi. E.g huko Africa ya Kati, kikundi cha Wakristo kinachinja waislamu kwa kasi ya ajabu!

Huu ndio uhalisia na imekuwa hivi tangu zamani ila haya yanapofungamana na maslahi ya makundi fulani basi utasikia ideological buzz na movements za ajabu kwenye media mpaka UN na sio bahati mbaya ni calculated moves ndio maana response speed ya matukio kama haya kwa waliopewa dhamana ina a significant discrepancy!!!!!!

Marx. K alisema religion is opium na ukiangalia kwa makini kuna wakati usemi huu una akisi ukweli wa maisha!!!!
 
IN GODS WE TRUST !! Mungu ailaze roho ya mtoto pahala pema peponi. Mara nyingine huwa naona ni heri ya sisi tusiofuata sana dini na matendo yake kuliko viongozi wa dini wenyewe. Hukumu ibaki kwa huyu mbaba yeye kama yeye, na sio uislam. IN GOD I TRUST !!
 
Inasikitisha sana kwa kweli,mtoto kuchinjwa kama kuku!! Sipati picha ya babaye na mamaye marehemu!
 
habari iko nusu nusu kabisa .... sababu za kuchinja hazijawekwa kwa nn? maandishi makanjanja bana
 
Inasikitisha san mtt kaenda tafuta elimu ya kumjua mungu, kakutana na ukatili huo. Ss naomba ifikie mahali hawa watu wanaotembea na visu, panga au fimbo pasipo sababu ipatikane sheria ya kuwabana hata kupitia shiria ndg ndg za serekali za mitaa maana tunakaa nao tunawaona na wengine tunawafaham.

Hakuwa mwanafunz wa mdrasa yake
.. alimsindikiza mwnzake ambae anaishi pale kuchukua kalam
 
Najaribu kupaelewa hapa...

Najaribu kufananisha na vile wafanyavyo magaidi tuwaonao kwenye filamu za kimagharibi...

Najaribu kufananisha na vile tuonavyo video clip kutoka mashirika makubwa ya habari namna wanajeshi wa nchi za magharibi wakichinjwa...

Somebody please explain....

MATATIZO YA AKILI
Mdogo wa muuaji Daudi Kurangwa
alisema kati ya mwaka 1996-1997
marehemu kaka yake alishawahi
kuugua ugonjwa wa akili na kutibiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Alieleza kuwa baada ya kuruhusiwa
kutoka hospitali alikuwa akiendelea
kutumia dawa kwa kipindi lakini
aliziacha baada ya kuhisi amepona.
“Kati ya Juni na Julai mwaka jana
aliugua tena na kutibiwa katika
hospitali ya Temeke,” alisema na
kuongeza kuwa hata hivyo juzi
Kurangwa hakuwa na dalili zozote za
ugonjwa huo kumrudia.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi
Temeke, Jonathan Shana,
akizungumzia tatizo la akili , alisema
polisi inaendelea na uchunguzi na
kueleza kuwa kuna taarifa kuwa
muuaji kipindi cha nyuma aliwahi
kuugua maradhi ya akili na kwamba
kwa hivi karibuni alikuwa ni mzima
na hajawahi kuonekana kama
anaumwa.
 
sina maana ya kuwa wakristo n bora kuliko waislamu

namaanisha serikali yaweza kuwa inaogopa joto la kidini ambalo lilishaanza kupoa

lasivyo laana itawatafuna wambagala,geita zanzibar waliochinja watu km mnofu wa bata mzinga

Hakuna laana hakuna nini.... Tatizo lenu mnaangalia mambo kwa jicho moja.... Hebu fuatilieni mtajua nini chazo
 
Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36) wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja mwanafunzi wake.



Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo saa 12.10 jioni kwenye eneo la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili

(hudugu)

-


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi waliomuua ustadhi huyo.

Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.-

"Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili wake kwenye varanda," alisema Kamanda Shana.

Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na kumuua papo hapo.-

Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.-
-Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi.



Read more:-http://www.vitukovyamtaanews.com/2014/02/inasikitishamwalimu-aliyemchinja.html#ixzz2u7Buda2I

USTAADH Mohamed Kurangwa (36),
aliyemuua mwanafunzi wa Shule ya
Msingi Nzasa Jamal Salum (12) kisha
naye kuuawa, ametajwa kuwa
alikuwa ana matatizo ya akili.
Kurangwa alimuua Jamal
mwanafunzi wa darasa la tano juzi
jioni nyumbani kwake Mbagala
Charambe Mianzini, kwa kumchinja
na kuweka kichwa cha marehemu
huyu kwenye miguu ya mtoto huyo,
kisha kuupeleka mwili wake choo
cha nyumba anayoishi, muuaji.
Muuaji huyo alizoa damu ya Jamal
na kuijaza kwenye ndoo kisha
kuiweka pembeni ya nyumba yake
kabla ya kuingia chumbani kwake,
kujifungia na kusoma Koran.
Ustaadhi Kurangwa ambaye aliuawa
na wananchi, wakati wa uhai wake
alikuwa Imam wa msikiti wa Kareem
ulioko Charambe.
MATATIZO YA AKILI
Mdogo wa muuaji Daudi Kurangwa
alisema kati ya mwaka 1996-1997
marehemu kaka yake alishawahi
kuugua ugonjwa wa akili na kutibiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Alieleza kuwa baada ya kuruhusiwa
kutoka hospitali alikuwa akiendelea
kutumia dawa kwa kipindi lakini
aliziacha baada ya kuhisi amepona.
“Kati ya Juni na Julai mwaka jana
aliugua tena na kutibiwa katika
hospitali ya Temeke,” alisema na
kuongeza kuwa hata hivyo juzi
Kurangwa hakuwa na dalili zozote za
ugonjwa huo kumrudia.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Polisi
Temeke, Jonathan Shana,
akizungumzia tatizo la akili , alisema
polisi inaendelea na uchunguzi na
kueleza kuwa kuna taarifa kuwa
muuaji kipindi cha nyuma aliwahi
kuugua maradhi ya akili na kwamba
kwa hivi karibuni alikuwa ni mzima
na hajawahi kuonekana kama
anaumwa.
Kamanda Shana alisema ukweli wa
tukio hilo haujafahamika na kwamba
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
imeunda kikosi kazi cha kuchunguza
tukio hilo.
USHUHUDA WA RAFIKI
Akizungumza na NIPASHE Jumapili
nyumbani kwa wazazi wa marehemu
Jamal, rafiki wa mtoto huyo
aliyenusurika kifo, Ramadhani
Hamisi (11) anayesoma darasa la
tano katika Shule ya Msingi
Chemchem, alisema kabla ya
kuchinjwa Ustaadhi Kurangwa
alianza kumchoma visu mfululizo
shingoni..
Ramadhani alisema anaishi na
mjomba wake katika nyumba ya
Ustadh huyo iliyoko Mianzini
Njiapanda, sehemu ambapo imamu
huyo alimchinja Jamal
“Siku ya tukio nilimuomba
marehemu Jamal, anisindikize
kwenda nyumba kuchukua kalamu,
ilikuwa saa 10:30 baada ya kupata
kalamu hiyo ndani ya chumba
tunachoishi na mjomba tulifunga
mlango na kuanza kuondoka.
“Wakati nafunga mlango marehemu
Jamal alikuwa jirani yangu akiwa
ameshika madaftari na kalamu,”
alisema Ramadhani kwa uchungu.
Aliendelea kueleza kuwa mara
Ustadh Kurangwa alitokea akiwa na
baiskeli, alipowaona aliiweka
pembeni na kuja karibu nao
akafungua pazia la mlango wa
chumba chake, lakini wakati
wanataka kuondoka, ghafla
alimkamata Jamal na kuanza
kumchoma kisu sehemu mbalimbali
shingoni.
"Nilimshuhudia akimchoma kisu
mara nyingi, Jamal alilia akisema
nisamehe Ustadh, nisamehe Ustadh,"
aliongeza mtoto huyo huku akitokwa
na machozi.
Ramadhani alikimbia hadi nyumbani
kwa Jamal na kumueleza mama
yake kuhusu tukio hilo na
yaliyoendelea nyuma hakuweza
kuyashuhudia tena.
JAMAL ACHINJWA
Mjumbe wa nyumba kumi wa Mtaa
wa Mianzin, Ester Msumba,
aliyesema alikuwa wa kwanza
kushuhudia tukio hilo, alieleza kuwa
alifika eneo la mauaji baada ya
kumsikia mwanamke mmoja akipiga
mayowe kuomba msaada baada ya
kuona kiwiliwili cha mtoto kimelala
na kichwa chake kimewekwa
miguuni.
Alisema mwanamke huyo alikwenda
kwenye madrasa ya Ali Munawar
kumpeleka mtoto wake kwa ajili ya
kumuanzishia masomo ya ziada, kwa
vile licha ya kufundisha dini eneo
hilo alilokuwa anaishi Kurangwa
linatoa mafunzo hayo ya ziada.
"Baada ya kusikia sauti ya yule
mama nilikimbilia eneo la tukio,
hapo nilikuta hali ni mbaya kwani
niliona mwili wa mtoto umelazwa
chooni na kichwa chake kiliwekwa
miguuni kwake," alisema msumba.
Alisema wakati wa mauaji hayo sauti
ya mtoto Jamal haikusikika hivyo
ilikuwa vigumu kupata msaada.
Msumba alisema pamoja na mwili
huo, alishuhudia ndoo iliyokuwa na
damu iliyochanganywa na maji kitu
kilichoashiria muuaji alikinga damu
hiyo kuzuia isitapakae na kusambaa
chini.
Sakafu ya choo hicho ilikuwa imejaa
damu na familia ilizuiliwa kukitumia
kwa muda kupisha uchunguzi.
Baada ya kufanya tukio hilo, Ustadh
Kurangwa, alikwenda chumbani
kwake na kujifungia huku akisoma
Kuran.
"Baada ya kumtafuta kwa muda mtu
aliyefanya unyama huo, tuligundua
amejifungia ndani tulipomchungulia
tulimuona akisoma Kuran huku
kanzu yake ikiwa imetapakaa damu,"
alisema mjumbe huyo.
USTADHI KURANGWA AUAWA
Wananchi walimvamia chumbani
baada ya kubomoa dirisha na
kumshambulia kwa matofali na
mawe hadi alipopoteza fahamu na
kumvua nguo kisha kumtoa nje na
kumpiga hadi alipokata roho.
WAZAZI WA JAMAL
Habiba Selemani (27) mama mzazi
wa marehemu Jamal akizungumza
na gazeti hili alisema anamuachia
Mungu kifo cha mwanawe.
"Namuachia Mungu kwanini tukio
hili afanyiwe Jamal," alisema mama
mzazi, hata hivyo, alikumbukia
kuwa kabla ya kifo chake alikuwa
anacheza na mdogo wake mwenye
miezi sita na kumvisha nguo
alipomaliza aliniaga kwamba
anakwenda kucheza.
"Aliniambia anakwenda kucheza
lakini kwa mshangao alinieleza kuwa
anaona nyota nyingi, sikujali
nilimuacha aende zake," aliongeza
kusema.
Kwa upande wake Salimu Ally,
ambaye ni baba mzazi, alisema
amepokea msiba huo mshituko
mkubwa na hakuamini kilichotokea
kwani ni tukio la kinyama.
Alieleza kuwa juzi jioni wakati
anakaribia nyumbani aliwaona
wanawake wanaingia kwenye
nyumba hiyo yalikofanyika mauaji
ya mwanae na kushangaa kwani
walikuwa wanatoka na kulia.
Ally alisema hakujua kilichotokea na
kwamba mawazo yake yalikuwa
kufika nyumbani kwanza.
“Nilipofika nilimkuta mke wangu
analia hajitambui ndipo mpangaji
mwenzangu aliponieleza kuwa
mwanangu Jamal kachinjwa niliumia
sana , sikuweza kuamini,” alisema
kwa huzuni.
Alikanusha kuwa marehemu mtoto
wake alikuwa anasoma kwenye chuo
cha Ustaadh huyo na pia
hawafahamiani japo Kurangwa
alimwita na kuingia naye ndani kisha
kumchinja.
Mwili wake ungezikwa jana saa 10
jioni baada ya kupatiwa kibali cha
polisi kuchukua maiti kutoka
hospitali ya Temeke.
 
Back
Top Bottom