Tiba za Asili: Manufaa ya Asali na Mdalasini


B

bwire jr

New Member
Joined
Jul 2, 2016
Messages
1
Likes
0
Points
3
B

bwire jr

New Member
Joined Jul 2, 2016
1 0 3
Wakuu nimekutana na makala hii nikaonelea nianzishe topic hapa ili tuweze kujadiliana na wataalam wetu na watufahamishe ukweli wake na uwongo wake au kutupa ushauri zaidi ya huu niuonao katika mada hii. Nimejaribu kwa kadiri ya uwezo wangu kuirekebisha kiswahili chake lakini nahisi hakiko sawa bado lakini naaminu ujumbe unafika.

Leo naanza na Manufaa ya Asali na Mdarasini:

MDALASINI NA ASALI

Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.

Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.

Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.

Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.

Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.

Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja 'cha chai' cha asali na kimoja cha mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. Kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.

Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.

Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.

7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.

Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann.

Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.

9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}.

Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.

Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
asante....
 
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2015
Messages
4,158
Likes
3,777
Points
280
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2015
4,158 3,777 280
Dawa ya Kansa zote:
Majani ya Hinna, chemsha vizuri mpaka ile rangi isambae, iache ipoe na kua ya vugu vugu,
Kunywa kila asubuhi kabla ya kula chochote na usiku kabla ya kulala. Glass 1 au 2. Haina shida.

Kwa uwezo wa Mungu utapona.

NB:Hata wa HIV aweza itumia.
 
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2015
Messages
4,158
Likes
3,777
Points
280
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2015
4,158 3,777 280
Je uso wako una Chunusi na madoa madoa?
Usihuzunike,

Chukua unga wa dengu,
Chukua unga wa manjano,
Chukua unga wa mdalasini,
Chukua na chumvi kidogo,

Changanya mchanganyiko wako wote vizuri, kisha weka pembeni,
Chukua kijiko cha chai chota huo mchanganyiko wako weka kwenye kifaa maalum, changanya na 'rose water' au maji ya kawaida tu si mbaya,

Pakaa usoni mpk shingoni (ukipenda) acha kwa dkk 20, nawa kwa maji ya vugu vugu.

Fanya hivyo asubuhi au jioni, kulingana na muda wako.

NB: Wanaume mnaweza mkafanya pia, haina madhara, haichubui ila inaondoa mafuta na madoa usoni.
 
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
11,019
Likes
181
Points
160
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
11,019 181 160
Bahati mbaya sana wazungu walishatuweza kila kilicho cha asili baadhi yetu tunadhani ni ushirikina. Kiukweli kuna mimea mingi ni dawa ila tuliowengi hatuamini hadi wazungu watuhakikishie kwanza

Kwa kweli mambo ya kizungu imetugharimu sana!
 
L

Levictus

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Messages
648
Likes
497
Points
80
L

Levictus

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2014
648 497 80
It's an interesting class kwa kweli
 
Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Messages
3,867
Likes
495
Points
180
Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2011
3,867 495 180
Baadhi ya tambiko kweli unaweza kuzichukulia kuwa ni ushirikina hasa kwa wale tunaoamini katika hizi dini za kigeni. But ndiyo historia yetu. Kwa hiyo mimea sio ushirikina...
Kweli kabisa mkuu tunaamini sana mambo ya kuambiwa na ngozi nyeupe. Je fangasi si ugonjwa? Kama ni ugonjwa tiba yake ni nini?
 
Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Messages
3,867
Likes
495
Points
180
Jacobus

Jacobus

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2011
3,867 495 180
Bahati mbaya sana wazungu walishatuweza kila kilicho cha asili baadhi yetu tunadhani ni ushirikina. Kiukweli kuna mimea mingi ni dawa ila tuliowengi hatuamini hadi wazungu watuhakikishie kwanza
BANGI, ni mmea unaotiba nyingi tu na ni mboga ila kwa kuwa walituaminisha kuwa ni haram sasa wao wameanza kuutumia kama tiba.
 
Raynavero

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Messages
34,628
Likes
43,105
Points
280
Raynavero

Raynavero

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2014
34,628 43,105 280
Je uso wako una Chunusi na madoa madoa?
Usihuzunike,

Chukua unga wa dengu,
Chukua unga wa manjano,
Chukua unga wa mdalasini,
Chukua na chumvi kidogo,

Changanya mchanganyiko wako wote vizuri, kisha weka pembeni,
Chukua kijiko cha chai chota huo mchanganyiko wako weka kwenye kifaa maalum, changanya na 'rose water' au maji ya kawaida tu si mbaya,

Pakaa usoni mpk shingoni (ukipenda) acha kwa dkk 20, nawa kwa maji ya vugu vugu.

Fanya hivyo asubuhi au jioni, kulingana na muda wako.

NB: Wanaume mnaweza mkafanya pia, haina madhara, haichubui ila inaondoa mafuta na madoa usoni.
Asante!!
 
Gwakukahja

Gwakukahja

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
925
Likes
511
Points
180
Gwakukahja

Gwakukahja

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
925 511 180
Naomba tutumie huu uzi kutaja tiba za asili tunazozijua kwani ni wazi kuwa yapo magonjwa yasiyo na tiba muafaka hospitalini lakini kuna watu wanajua tiba za asili.

Lengo ni kuweka kumbukumbu kwani maandishi uliyoweka hapa yanaweza kuja kuwa na manufaa miaka hata 50 ijayo, huwezi kujua.

Najua wengi hatujui majina kwa lugha ya kiswahili, au kisayansi ya mimea mingi tunayoijua ni tiba. Naomba tu uitaje kwa jina la lugha unayoifahamu, inawezekana akatokea mdau anajua jina la mmea huo kwa lugha nyingine tunayoweza kuielewa wengi. Kama unaweza weka picha kabisa ya mmea au tiba unayoongelea.

Binafsi nitaanza na kutaja mimea ya tiba zifuatazo katika posts zitakazofuata, na nitajitahidi kuweka picha pale ninapoweza. Pia nitaandika "tiba" au "tambiko" kwa mujibu wa wazee wangu niliobahatika kukua nao (ingawa kwa sasa sifanyi hizo), kwa lengo tu la kuweka kumbukumbu kwani inawezekana miaka mingi ijayo watoto au wajukuu zetu wakaja kusoma huu uzi katika kujifunza mila na desturi zao.
Baadhi ya tiba nitakazotaja hapa ni zile ambazo niliwahi kuona wazee wangu wakizitumia, zile nilizowahi kutumia mwenyewe, zile nilizowahi kuhadithiwa, na hata zile nilizosoma sehemu mbali mbali ikiwemo humu JF...

Baadhi ya nitakazoweka kwenye posts zinazofuata ni;

1. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (la kuharisha)
2. Mimea inayotibu maumivu ya tumbo (sio la kuharisha)
3. Mimea inayotibu vidonda
4. Mimea inayotibu kiungulia
5. Mmea unaotibu athma (mara moja tu)
6. Mimea inayoongeza nguvu za kiume
7. Mmea unaotibu maumivu ya meno (pamoja na kutoboka)
8. Tiba ya maumivu ya sikio (sio mmea)
9. Mimea inayofunga kizazi kwa wanawake
10. Mmea unaotibu jipu (bila kupasuliwa)
11. Dawa ya kusaidia kutoa kondo la nyuma la ng'ombe
12. Mmea unaotibu minyoo (kwa binadamu na mifugo)
13. Mmea unaotibu mastitis kwa ng'ombe
14. Kadhalika

Pia zipo tiba vyingine ambazo zinahusiana na imani ambazo nitazitaja baade kwa mfano
1. Jinsi ya kumkinga au kumtibu mtoto mchanga dhidi ya "kijicho"
2. Jinsi ya kujizuia "kufanyiwa mchezo" kwa chakula unachokula hadharani au kwenye sherehe
3. Jinsi ya kuzuia mvua isinyeshe siku kuna tukia kama sherehe au mkutano
4. Tambiko ya kuomba mvua
5. Kadhalika

Nawaombeni wanaJF mposti kwenye huu uzi tiba zozote za asili mnazozijua au mlizowahi kusikia. Huwezi jua miaka mingi ijayo akatokea kijana wetu mtafiti akasoma bandiko lako, akafanya utafiti akaibuka na dawa matata ambapo utakuwa umesaidia vizazi na vizazi...
Nasubiri #6
 
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Messages
10,358
Likes
8,221
Points
280
Age
31
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2013
10,358 8,221 280
Seen...
 
Augustine Genius

Augustine Genius

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
417
Likes
228
Points
60
Augustine Genius

Augustine Genius

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
417 228 60
Unaifahamu binzari??

Nashindwa kukuelewesha vzr,
Nakushauri ukagoogle 'Manjano' watakuletea.
Binzari naifahamu,
Kwa hiyo ni unga wa binzari?
 
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2015
Messages
4,158
Likes
3,777
Points
280
everhurt

everhurt

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2015
4,158 3,777 280
Binzari naifahamu,
Kwa hiyo ni unga wa binzari?
Naam, ila manjano ndio kile kiungo (kipo kama tangawizi) kikitwangwa na kuchekechwa, tunapata unga ambao wanauita Binzari au unga wa manjano.
 
Augustine Genius

Augustine Genius

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
417
Likes
228
Points
60
Augustine Genius

Augustine Genius

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
417 228 60
Naam, ila manjano ndio kile kiungo (kipo kama tangawizi) kikitwangwa na kuchekechwa, tunapata unga ambao wanauita Binzari au unga wa manjano.
Asante mkuu
 
BAKOI

BAKOI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Messages
967
Likes
1,858
Points
180
Age
49
BAKOI

BAKOI

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2016
967 1,858 180
Mchanganyiko wa tangawizi + habat sawda+ asali unasaidia nini katika mwili
Cc mzizimkavu, Mshana jr
 

Forum statistics

Threads 1,273,646
Members 490,468
Posts 30,487,567