Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,775
- 2,693
Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.
Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni.
Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na:
1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono
2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu
3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva
4. Ajali kwenye neva
5. Kunywa pombe kupita kiasi
6. Uvutaji wa sigara na bangi
7. Uchovu sugu
8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu
10. Ugonjwa wa kisukari nk
Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutokea na kudumu kwa muda mrefu. Inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa fulani ambao unahitaji matibabu ya haraka.
Kuumwa ganzi kwenye miguu na mikono yako linaweza kuwa ni jambo linaloudhi sana hata hivyo hapa mimi leo nimekuandalia dawa za asili unazoweza kuzitumia kuondokana na tatizo hili
Leo nitakupa njia za kutengeneza dawa ya mtu anayesumbuliwa na ganzi na mafua :
TIBA YA ASILI
Unachotakiwa kufanya ni kuchukua maji ya tangawizi mbichi na kupikia uji, kisha utapima uji kikombe kimoja na kuzidisha unga wa Habat Sauda kijiko kidogo, utatumia asali kwenye uji huo badala ya sukari.