Tiba gani nitumie.

Tiba gani nitumie.

Itoye

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2017
Posts
531
Reaction score
1,026
Wakuu Salaam.

Hongereni kwa shughuli mbalimbali za ujenzi wa maisha binafsi na taifa kwa ujumla.

Naomba msaada wa mawazo. Ninafuga kuku wa mayai ya kisasa na machotara. Sasa for the past two weeks wamekuwa katika tiba, baada ya kuanza kuharisha choo cheupe tulishauriwa na kuwapatia ENROVETo-20. Walipomaliza tukanotice wana choo cha brown, kwa kuwa wote wanataga tukashauriwa kutumia AMPRLIUM 20%.

Sasa kitu ambacho kimejitokeza na kina nipa wasiwasi ni kuwa leo kuku 2 wamekufa na ulaji wao si ule wa kawaida mfano kuku chotara kilo 10 walikuwa wanamaliza for less than 30minutes lakini sasa hata 4 hours chakula unakikuta.

Naomba ushauri hatua zipi nichukue ili kurescue hii situation isizidi kuwa mbaya.

Asanteni sana kwa mawazo yenu.
 
Cheki mafua .... ingawa Enrovet ni dawa ya mafua .... choo cheupe ni typhoid
 
magonjwa mengi yanatokana na kutozingatia usafi, kuwa na hewa ya kutosha, msongamano kwenye banda. ninalokushauri tibu maji yao ya kunywa tumia water guard ya kidonge au ya maji. hili huwa wengi wanalisahau, pia waongezee vitamin wape chakula kizuri kwa kampuni inayoaminika.
jibu yafuatayo
amprolium uliwapa kwa siku ngapi
chakula ulibadilisha au ni kile kile
je wanaonyesha dalili gani kwa sasa, choo chao kikoje


unapotoa dawa safisha banda na kila kitu vyombo nk. tumia disinfectant kali. lasivyo ugonjwa huwa unarudi. maranda yatoe na choma moto. iwe tabia yako kusafisha vyombo na dawa kila mara unapopata ugonjwa. ili ugonjwa usijirudie.
 
Back
Top Bottom