Sera/sheria ya corporate social responsibility [CSR] jinsi inavyonufaisha wachache Tanzania

Maria Nyedetse

JF-Expert Member
Apr 24, 2021
657
1,485
SALAM,
Awali BANDIKO hili nililiandaa kwa ajili ya stories of change hata hivyo kutokana na kukosa muda nikajikuta tarehe ya mwisho ya kupokea maandiko imeshapita!!! Sasa naomba kulileta kwenu kama forum ya elimu (kujifunza) na kujadiliana na kuona namna bora ya utekelezaji wa hili kama nchi.

Napokea mawazo kinzani LAKINI naomba pasiwepo matusi na dhihaka kwani mawili haya hayajawahi kujenga POPOTE PALE.

Sasa endelea...

SERA/SHERIA YA CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY [CSR] JINSI INAVYONUFAISHA WACHACHE TANZANIA

Utangulizi

Ni nini Corporate Social Responsibility [CSR]

Corporate Social Responsibility [CSR]
ni mfumo unaozitaka kampuni kutumia sehemu ya mapato yao kunufaisha jamii ambako kampuni hizi zinafanya kazi na kupata faidi kutokana na jamii hizi. Kampuni zinaweza kutumia fedha hizi kuwekeza kuboresha mazingira, kuwekeza kwenye nishati, huduma za jamii kama ujenzi wa miundombinu, kununua vifaa tiba, madawa au hata utoaji wa elimu na kuboresha vipato vya jamii tajwa. Uwekezaji huu unaweza kufanywa moja kwa moja na kampuni husika, fedha hizi kuingizwa kwenye mipango ya jamii na kusimamiwa na jamii husika au kutumia mtu/taasisi nyingine kufanya kwa niaba ya kampuni na jamii husika na kuhakikisha manufaa yanapatikana.

Ikifanywa sawa sawa Corporate Social Responsibility [CSR] huweza kunufaisha pande zote mbili yaani kampuni kwa kujenga mapenzi ya jamii juu ya bidhaa au huduma zake na kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya jamii husika pamoja na kusaidia jamii kuboresha maisha katika nyanja za mazingira bora, huduma bora za jamii na kuimarisha uchumi wa jamii.

Katika uzalishaji wa makampuni haya yanatumia rasimali au yanasababisha kupungua kwa rasilimali asili za jamii kama utoaji wa hewa chafu ambayo huathiri mazingira, kutumia rasilimali kama maji, madini ya thamani mpaka yale ya ujenzi, ukataji wa mimea ya asili n.k. Kadiri kampuni hizi zinavyofanya kazi husababisha kupungua kwa rasilimali hizi au kukosa uasili wake (kuchafuliwa mfano hewa, maji) hivyo ni vema kampuni hizi kutumia sehemu ya mapato yake kunufanisha jamii hizi ambazo rasilimali zao zinapungua kutokana na uzalishaji wa makampuni haya.

Mukhtadha wa sheria, sera na kanuni za nchi.

Kama zilivyo nchi nyingi duniani, Tanzania inatambua umuhumi wa Corporate Social Responsibility [CSR] kwenye jamii. Umuhimu huu ulianza kuonekana miaka ya 90 baada ya nchi kuanza kubinafsisha rasilimali za umma na kuvutia uwekezaji binafsi ili kuongeza ufanisi hasa kwenye sekta za madini. Kutokana na uwekezaji wa sekta binafsi zilianza kusikika sauti kutoka kwenye jamii na makundi ya wanaharakati wakipaza sauti juu ya jamii kunufaika zaidi kutokana na rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao ambazo zinatumiwa na makampuni haya. Mpaka sasa Tanzania imeingiza kwenye sheria takwa la makampuni haya kutumia sehemu ya mapato yao kusaidia jamii ambazo makampuni haya yanafanyia biashara au uzalishaji wao ambapo yanatakiwa kutoa wastani wa 0.7% ya mapato yao kusaidia jamii hizi. Fedha za Corporate Social Responsibility [CSR] husaidia jamii kwenye maeneo ambayo hayajapata uwekezaji mkubwa wa serikali hivyoo kuunga mkono jitihada za Serikali kuwahudumia wananchi wake.

Hali ilivyo

Katika maeneo mengi ya nchi yetu, Corporate Social Responsibility [CSR] imekuwa ni jukumu la makampuni makubwa ya kigeni kama makampuni ya uchimbaji wa madini, makampuni ya mawasiliano, ujenzi na mfano wa hayo. Na mara nyingi makampuni haya hutoa au kutekeleza Corporate Social Responsibility [CSR] kama sadaka na kwa sehemu kubwa hutegemea utashi wa makampuni haya huku jamii zinazozunguka zikiwa hazina taarifa sahihi juu ya mapato ya makampuni haya na hivyo kutokuwa na sauti ya kudai utekelezaji wa Corporate Social Responsibility [CSR] kwenye maeneo yao.

Sababu za hali hii.

Kwa sehemu kubwa makampuni mengi ya kigeni kwa sababu ya kubanwa na mikataba mbambali ya kimataifa na mikataba ya nchi yanakotoka hivyo hulazimika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye jamii kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] ili kuhakikisha yanalinda sura na sifa za makampuni yao. Changamoto kubwa imekuwa makampuni yanayotoka kwenye nchi ambazo hazina sheria madhubuti za utekelezaji wa Corporate Social Responsibility [CSR] na makampuni ya wazawa. Changamoto hii kwa kiasi kikubwa inasababishwa na mambo yafuatayo:-

Kukosekana utashi wa viongozi wa maeneo ambako makampuni haya yanafanyia shughuli zao hivyo kusababisha makampuni haya kutoona umuhimu wa kutoa sehemu ya mapato yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya jamii kupitia Corporate Social Responsibility [CSR]. Hali hii husababishwa na aidha uelewa mdogo wa viongozi hawa au kukosekana kwa mipango madhubuti ya taasisi au maeneo wanayoyaongoza jambo linalosababisha watendaji hawa kufanya kazi kwa utashi na mawazo yao badala ya kusimamia mipango ya muda mrefu, muda wa kati na muda mfupi ambayo inabainisha wazi fursa zilizopo katika maeneo yao ikiwemo utekelezaji wa miradi kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] za makampuni yanayofanya kazi kwenye maeneo yao.

RUSHWA; Kwa kiwango kikubwa jamii nyingi hukosa fursa ya kutekelezwa miradi mbalimbali kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] ya makampuni yanayofanya kazi kwenye maeneo yao kutokana na rushwa zinazoendekezwa na viongozi wao. Watendaji wengi waliopewa mamlaka ya kuhudumia na kuongoza jamii hupokea fedha na takrima mbalimbali kutoka kwenye makampuni haya jambo linasobabisha makampuni haya kutotekeleza miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] kwani kwa makampuni haya itakuwa kama kuingia gharama mara mbili. Mfano mara kadhaa tunasikia viongozi wetu wakimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali kwa ujumla [Utamaduni uliopo sasa katika nchi yetu] kwa kupeleka fedha nyingi za miradi kwenye maeneo mablimbali ya utawala (Mikoa, Wilaya, Halmashauri) LAKINI CHA KUSHANGAZA UNAKUTA KUNA WAKANDARASI/WAZABUNI/WAFANYABIASHARA WENGI WANAFANYA KAZI AU BIASHARA ZENYE THAMANI KUBWA NA KUNUFAIKA NA FEDHA HIZI HATA HIVYO HUKUTI HATA CHOO CHA SHULE AU BOMBA LA MAJI LILILOVUTWA NA KAMPUNI AU WAZABUNI HAWA KWA AJILI YA JAMII HIZI.

Sababu kubwa utakuta Watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia maeneo haya tayari wanakuwa wamechukua asilimia zao mapema tena wakati mwingine kwa kuongeza gharama ya bidhaa au huduma wanazozitoa hivyo kuwawia vigumu kuyabana makampuni au wafanyabiashara hawa kutoa sehemu ya mapato yao kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kupitia Corporate Social Responsibility [CSR]. Hali hii husababisha uharibifu mkubwa wa rasilimali za asili za jamii kwani wasimamizi wa sheria wanakuwa tayari wamenunuliwa na kukosa kauli thabiti juu ya makampuni/wafanyabiashara hawa na wakati mwingine wakandarasi kukimbia miradi kwa sababu ya wasimamizi wa maeneo husika KUCHUKUA CHAO MAPEMA kwa kiwango ambacho kinafanya kushindwa kutekeleza miradi au zabuni zao. Inafika wakati unajiuliza ni nani hasa anatakiwa kusimamia hili, Je ni Rais wa nchi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Baraza la madiwani? Je wasiposimamia hili nani anawawajibisha? Je wakiwajibishwa watawajibishwa kwa kushtakiwa na kulipa fidia ya hasara hii waliyoisababisha au kuvuliwa vyeo vyao pekee? Na kama ni kuvuliwa vyeo pekee, Je ni nini kitamfanya asimamie utekelezaji wa miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] badala ya KUCHUKUA CHAKE MAPEMA?

Kutokuwa na mikataba inayotamka wazi mkandarasi/mzabuni/mfanyabiashara anawajibika kutoa sehemu ya mapato yake kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] kwenye jamii anakofanyia kazi zake. Hali hii husubiria utashi wa kampuni au mzabuni husika kutoa kadri atakavyojisikia jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi hivyo kusababisha kukosekana kwa matumizi endelevu ya rasilimali za jamii na mahusiano hasi baina ya makampuni mengi na jamii za maeneo yanakofanyia kazi zao. Leo hii tunapokea taarifa nyingi za uharibifu wa mazingira, vyanzo vya maji, kuachwa mashimo n.k. Ifike wakati mikataba yote ya zabuni au kandarasi itamke wazi wajibu wa wazabuni kutoa sehemu ya mapato yao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi au shughuli mbalimbali zenye manufaa kwa jamii kupitia Corporate Social Responsibility [CSR.

Kukosekana kwa muundo rafiki na unaoruhusu uwajibikaji kwenye taasisi zetu nyingi hivyo kusababisha maamuzi kufanywa na wachache kwa niaba ya wengi na walio wengi kukosa namna bora ya kuwawajibisha viongozi hawa ambao wengi ni wateule wa Rais. Mifumo yetu ya kitaasisi imechangia kwa kiwango kikubwa kukosekana kwa ufanisi unaoridhisha wa usimamizi wa miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] kwa sababu ya watendaji wake kuwa na mamlaka makubwa ya kiutekelezaji na hakuna namna bora ya kuwawajibisha viongozi hawa kwani wengi ni wateule wa Mamlaka za juu hivyo jamii kubaki kuumia bila kuwa na la kufanya. Ifike wakati pawepo na mifumo bora ya kitaasisi inayoruhusu jamii kuwawajibisha viongozi hawa wenye madaraka makubwa juu yao kwani kwa sasa fedha nyingi za wazabuni ambazo zingetumika kutekeleza miradi kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] huingia kwenye mifuko ya wachache.

Vyombo mbalimbali vya nchi kama USALAMA wa TAIFA, POLISI, TAKUKURU n.k aidha kutowezeshwa vya kutosha kuangalia eneo hili au watendaji wake kuwa sehemu ya CHUKUA CHAKO MAPEMA, au eneo hili kutokuwa sehemu ya majukumu yao. Ufanisi katika utendaji wa vyombo hivi utasaidia sana jamii kunufaika na miradi hii kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] za makampuni/wafanyabiashara badala ya sasa ambapo fedha hizi huingia kwenye mifuko ya wachache na kukosesha jamii manufaa mapana ambayo yangepatikana kama miradi hii ingetekelezwa. Imefikia wakati wanafunzi wanaweza kukosa hadi choo au dawati wakati kwenye eneo lao kuna miradi mingi na yenye thamani kubwa inatekelezwa ambapo makampuni/wafanyabiashara hawa wangesimamiwa kutoa sehemu ndogo ya mapato yao kutekeleza miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] basi changamoto hizi zingetatuliwa bila kusubiria serikali kuu.

Kwa kutambua umuhimu wa miradi ya Corporate Social Responsibility [CSR] katika uimarishaji wa huduma kwa jamii na kuhakikisha kuwa matumizi ya rasilimali mbalimbali za jamii yanakuwa endelevu, ni wakati sasa kwa mamlaka husika [Mamlaka za Uteuzi] kuhakikisha watendaji wanasimamia Makampuni/Wazabuni kutoa sehemu ya mapato yao kutekeleza miradi kwenye jamii wanazonufaika nazo badala ya kuwa chanzo kingine cha watendaji hawa kujineemesha. Aidha ifike wakati sasa mikataba mpaka ngazi ya chini kuweka wazi kipengele cha utoaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kupitia Corporate Social Responsibility [CSR] na kuhakikisha jamii inanufaika na miradi hii.

Pamoja na kufanyika haya; vyombo vyetu vya Ulinzi Usalama USALAMA wa TAIFA, POLISI, TAKUKURU n.k vifumuliwe na kuundwa upya kuakisi mahitaji halisi ya jamii na nchi kwa ujumla. Nahofia kusema VYOMBO HIVI havina uwezo, LA HASHA!!! Kwani tumeshuhudia yanapotokea matukio yenye maslahi ya kisiasa wahusika husakwa na kukamatwa kwa muda mfupi mfano anapotusiwa kiongozi/mwanasiasa mkubwa; Je ni kwa nini kwenye mambo yenye maslahi mapana kwa jamii hatuzioni jitihada hizi??? Kwa nini mwizi wa kuku anashughulikia haraka zaidi na wabadhirifu wa mali au fursa za umma wanatembea vifua wazi? Je ni mnyororo kuanzia juu hadi chini? Au ni kufanya kazi kwa mazoea??? Ifike wakati vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wasimamie rasilimali na maslahi ya jamii kwa nguvu zao zote nasi raia daima tutawaunga mkono kwa hali na mali…. Vinginevyo wananchi watashindwa kutofautisha kazi ya wanasiasa na watendaji wevi na vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama.

Nawasilisha wanajamvi.

Maria Nyedetse

Mtanzania mwenye Uchungu na Nchi yake
 
Umeongea Jambo kubwa sana ..
MTU unatumiwa SMS umepokea mgao WA kampuni ya simu wa shilingi 50...,sasa ya nini hii..

Why wasijenge hata kiwanja kimoja cha michezo kila mwaka ...kuliko kutugaia gawio la Aina hii
 
Habari sis,,bandiko zuri Sana ,je unaufaham wowote wa namna ya kuandaa proposal kwaajili ya kampuni husika,I'm interested
 
Back
Top Bottom