Three Tanzanians found guilty of plot to kill ex-Rwanda army chief

Three Tanzanians found guilty of plot to kill ex-Rwanda army chief

MUKAMASIMBA, hawa watu bwana...wakati hii inaanza walipiga kelele wee eti ni Kagame kumbe ni watz waganga njaa walikuwa wanataka kumuibia jamaa gari lake
Tuliza boli, huu mchezo ndo kwanza PK anauingia, siye tuko huko long time.
Picha hii haijaisha kama mnavyofikiri, na A Kusini hawanyongi watu kama hao "WaTz" walioshikwa.
Kwa hiyo baada ya kifungo watarudishwa tu bongo, na hapo mbivu na mbovu zitajulikana
 
Hivi hao watu,wote kuvaa barakashea siku ya kesi,Na wote kuwa Na majina ya Ki islamu Ni coincedence au planned? Pili,ukichunguza picha hao watu wamefanana Na Ni Kama wa kutoka ethnic moja,chunguza Sana pua zao. Sisemi hakuna watanzania wanaoweza kuhongwa wafanye uhalifu,pia sisemi hakuna watz wahalifu. Ila inatakiwa serikali ya tz kwa kutumia vyombo vyake ishirikiane Na serikali ya south,wawachunguze hao watu asili Yao,walipata wapo pasports,ndugu zao Na koo zao Ni kina nani Na wamekua wakifanya kazi gani siku zote za maisha Yao ya nyuma. Kunaweza kugundulika mengi.

Ni kweli mkuu, ndo maana nilisema hapo awali. These guys are doing poor chase game. Wanatafuta support ya kimataifa labda. But am sure Tanzanians are not as foolish as they think. Na hiyo inaweza ikawa wanatupandisha mori, ingawa serikali itaonekana kama imepuuzia. But people are working and they will decide where to revenge. Kagame anajitengenezea jinamizi.... MUKAMASIMBA murutongore JMAl mkamasimba
 
Last edited by a moderator:
Tuliza boli, huu mchezo ndo kwanza PK. Ansuingia siye tuko huko long time.
Picha hii haijaisha kama mnavyofikiri, na A Kusini hawanyongi watu kama hao "WaTz" walioshikwa.
Kwa hiyo baada ya kifungo watarudishwa tu bongo, na hapo mbivu na mbovu zitajulikana

Ni kweli mkuu, hata kabla ya hapo. Serikali yetu ina ushirikiano mkubwa na ya south. Hapo walishabadilishana info zamani sana.
Sasa isije ikawa kauli ya mzee Nyerere alivyotaka kumtandika Nduli amin ikatimia kwa kagame. Nia, sababu, uwezo wa kumtandika tunao........ murutongore MUKAMASIMBA JMAl RUCCI @md25 @azusa street @BekaNurdin @lawmaina78 @Kobello @VITA VYA KAGERA @Patrick Elias @Bankobeza Kyamani
 
Last edited by a moderator:
Hao jamaa wanaonekana ndugu na balaghashia zao. By the way, aliyewapa kazi hiyo ni Francois Kanyandekwe mrwanda mwenye uraia wa Belgium.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    39.9 KB · Views: 96
Nimesoma post za watu wengi kuhusu Watanzania waliokamatwa South Africa kwa kutumiwa na Kagame kumuua Nyamwasa. nimekubaliana na wengi kwamba, TANZANIA LAZIMA ITOE TAMKO KALI NA KUOMBA MAELEZO YA KUELEWEKA toka Rwanda kwasababu jina la Tanzania limechafuliwa sana sana.

Watanzania wanaoishi South Africa, Ulaya na Marekani kwasasa watakuwa hawaaminiki sana, wengi watakuwa wanaonekana kama wauaji tu. hapo South Africa kuna uwezekano hata Mtanzania kukosa nyumba ya kupanga kama atajitambulisha kuwa yeye ni Mtanzania, mwenye nyumba ataogopa kupangisha watu wanaoweza kukodiwa kuua. hata kama watu mtabisha lakini ukweli uko palepale, nchi yetu imechafuliwa sana, image yetu imetiwa madoa na Paul Kagame.

Ninashauri pia serikali ya Tanzania ishirikiane na South Africa kubadilishana wafungwa hao jamaa waje watumikie kifungo hapa, watatupatia siri nyingi sana na tutapata nafasi ya kuhakikisha kama kweli hawa jamaa ni watanzania au wameiba tu passport.
 
yap, kusema kweli tumechafuliwa sana aisee.
 
Tumejichafua au tumechafuliwa? Swali ni kuwa ni kwanini "watanzania" wamekubali kutumika? La muhimu ilikuwa ni kuwarudiaha hapa nyumbani halafu watuelekeza kilichotokea, ili tuchukue hatua.
 
kama walikubali kutumiwa wakome na hakuna sababu ya kutumia kodi zetu kuwalisha wauaji. Ila swali langu mbona la madawa ya kulevya hamliona kuwa ni uchafu au kwa kuwa linawahusu viongozi wa serilai tena wa ngazi za juu kabisa, mpaka leo hii hatujajibiwa habari za madawa ya kulevya yanayosemekana kuwa ya Ridhiwani Kikwete yaliyokamatwa China, na yale ya Kinjeketile Kingunge ngombale mwiru ya Agness Msongange, mpaka leo hii vijana wanaosoma vyuo vikuu Afrika Kusini watoto wetu wa sekondari wanaosoma huku wanapekuliwa kama wafungwa, mbona hamsemi serikali itoe tamko kuhusu hili? au na hao wauwaji ni ndugu na watoto wenu, mbona hamsemi habari ya Samwel Sita na wenyeviti wake wa kamati za bunge maalumu la katiba kuwa ni washiriki wake wa biashara hii na haya yanaszungumzwa na wajumbe wenzie wa bunge hilo. Hakuna kutoa Tamko kuhusu Rwanda na wala tanzania ya leo haina ubavu wa kushinda vita yoyote labda zile za Abubakar wa Comoro nchi isiyo na majeshi, lakini Kagame hamumuwezi Jeshi hili la Mwamunyange na Kikwete sio la wakina Musuguri na Mwl Nyerere acheni kujidanganya. Hao wauaji huko Sauzi wanyongwe na kufa, jino kwa jino
 
Mwinyi aliwahi kusema kuwa mjinga mtawale kwa kuwa kagame ni mjinga lazima tumuongoze tu wala tusiwe na haraka naye kabisa.
 
kama walikubali kutumiwa wakome na hakuna sababu ya kutumia kodi zetu kuwalisha wauaji. Ila swali langu mbona la madawa ya kulevya hamliona kuwa ni uchafu au kwa kuwa linawahusu viongozi wa serilai tena wa ngazi za juu kabisa, mpaka leo hii hatujajibiwa habari za madawa ya kulevya yanayosemekana kuwa ya Ridhiwani Kikwete yaliyokamatwa China, na yale ya Kinjeketile Kingunge ngombale mwiru ya Agness Msongange, mpaka leo hii vijana wanaosoma vyuo vikuu Afrika Kusini watoto wetu wa sekondari wanaosoma huku wanapekuliwa kama wafungwa, mbona hamsemi serikali itoe tamko kuhusu hili? au na hao wauwaji ni ndugu na watoto wenu, mbona hamsemi habari ya Samwel Sita na wenyeviti wake wa kamati za bunge maalumu la katiba kuwa ni washiriki wake wa biashara hii na haya yanaszungumzwa na wajumbe wenzie wa bunge hilo. Hakuna kutoa Tamko kuhusu Rwanda na wala tanzania ya leo haina ubavu wa kushinda vita yoyote labda zile za Abubakar wa Comoro nchi isiyo na majeshi, lakini Kagame hamumuwezi Jeshi hili la Mwamunyange na Kikwete sio la wakina Musuguri na Mwl Nyerere acheni kujidanganya. Hao wauaji huko Sauzi wanyongwe na kufa, jino kwa jino
Wanyarwanda wengi hamna akili kama ulivyo wewe mnawaza kuuwana na ukabila tu mburula wewe tuache kama tulivyo watanzania tunajuana wenyewe kwa ustarabu wetu.
 
Hakuna idara mbovu kama uhamiaji na mambo ya nchi za nje( mabalozi zetu) , hao watu wamejitambulisha ni Watanzania na serikali ya South Africa inawatambua hivyo kwa sababu wana document halali za Tanzania ( pasport)
maawali ya kujiuliza
1. Walizipata wapi hizo Pasport?
2. Kama sio halali kama wanavyosema wasemaji wa Tanzania, waliwezaji kusafiri nazo mpaka South Africa?, maana sasa Pasport lazima iwe scaned kwenye Airport na hata border post zote, walipititaje?

juzi tumeona hapa Watu zaidi ya 50 wanaingia kwaa Pamoja ndani ya Tanzania na walikuwa hawana shughuli rasmi ya kufanya, nani alitoa visa kwa watu wote hao?

uhamiaji airport iliwaruhusu vipi kundi kubwa la watu kama hao kuingia bila kuulizwa, angekuwa mmoja sawa, hamsini?
 
Ubungoubungo comment ulioandika mwanzo yote pumba. Labda para ya mwisho tu ndio ina busara. Wale wachukuliwe kule South waletwe tz. Washughurikiwe waseme kinagaubaga walitumwa na nani na mipango ilikuaje(ingawa naskia kule South wameshasema ndio maana yule hakimu through BBC ali conclude kwamba ile attempt iko political motivated!).PK wala msimchokonoe kwani kwanza alisha wakana na alisema wahukumuni mtakavyo,lakini pili' mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani'!
 
Last edited by a moderator:
Pengine inawezekana uko sahihi kwa kutaka kusikia toka kwa hao wafungwa toka TZ, lakini hata bila ya wao kuja kufungwa hapa, tunaweza kupata profiles zao kutoka South Africa.

Sikubaliani na wazo lako la kutafuta visasi kwa Kagame. PK ana sera zake na anapohitaji wataalam kutoka nje katika kutelekza yeye anaweka biashara sokoni. Hakuwateka nyara na kuwapeleka kwa sababu ni Watanzania. Mbona hujasema kwenda kuwapiga wasomalia wa Alshababu walio (na pengine wamesha) recruit wa Tanzania kupitia misikitini kwenda kupigana kule?

Sera yako ya visasi vya kutetea maharamia, siyo. Hawa ni wahalifu tu. Wako tayari kuua mtu pasipo sababu kwa sababu ya pesa. Usishangae ndio hawa wana mitandao ya mauaji ya kutisha yanayoendelea hapa TZ. Kwanza majina yao ni nani?

Kagame hajatuaibisha. Aibu ni ya sisi wenyewe kama vile riz alipokamatwa na madawa ya kulevya kule china, mauaji ya raia kwa misingi ya kisiasa, ukiukwaji ihaki za binadamu, uharamia unaofanywa na ccm katika katiba, ugaidi wa akina mwigulu kinana, masele, matumizi mabovu ya madaraka na raslimali za taifa, kudorora kwa elimu, uchakachuaji n.k, Yote haya ni aibu yetu. Yanahitaji hatua muhimu, sahihi na za haraka badala ya kutafuta ugomvi na PK kwa suala la mambo yetu wenyewe.

Hakuna mtu anatuchafua kwa sababu hatusingiziwi. Uchafu wetu sasa unavuka mipaka ya nchi na hatuwezi kukosa haya kiasi cha kutafuta mchawi wakati nyumba yetu ni chafu chafu chafu na wala hatuna mpango wala nia ya kuisafisha. Huko South, imewafikia harufu yetu. PK katumia uvundo wetu kutengeneza dawa, kosa lake ni lipi?

Safisha nyumba yako kwanza badala ya kulaumu majirani wanaposema harufu yako ina waathiri.
Ubungoubungo
 
Last edited by a moderator:
Mimi nathani hawa sio watz. Na hata kama ni watz,Tanzania government itafanya nini kuzuia such thing. Kama Kagame aliwapa kazi wao wakakubali ni sawa. Na inawezekna kabsia Kagame aliona kwamba wanaweza sio wamekurupuka tu.

Hawa watakuwa watusi wanaoishi tanzania pia. Hio inawezekana.

Kama TISS walikuwa na intel ya mauaji hayo kutokea kwanini hawakutafuta zaidi au kuzuia jina la nchi kuharibika mpaka wamesubri wafike mahakamani? Wangeweza kuzuia hii jambo either to kill them both or extradite them back to Tanzania na kua soo.
Hapa TiSS wamecheza mchezo wa kijinga.
 
Back
Top Bottom