This week in Perspective: Kipindi kinamlenga nani?

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Kuna kipindi "This week in perspective" - kinarushwa na TBC1.

Kipindi hiki nakipenda kwani hua na mijadala mizuri ya kuelimisha jamii. Ila kwa upande wangu naona yanayojadiliwa hayawafikii watu wote, si kwa sababu watu hawana runinga, bali kwa sehemu kubwa lugha inayotumika ni ya kiingereza na watu wengi hawajui lugha hiyo.

Sasa sielewi kama kimewekwa kwa ajili ya watu wanaojua kiingereza tu au ni kwa ajili ya watu wote, kama ni kwa ajili ya watu wote, ingefaa watumie lugha ya Kiswahili ili kila mtu anayekisikiliza/tazama apate kile kilichokusudiwa.
 
Moja ya malengo ya kuanzisha TBC, iliyojulikana kama TVT hapo mwanzo ni KUELIMISHA na KUFAHAMISHA umma wa watanzania pamoja na KUKUZA LUGHA YA KISWAHILI. Haya ni malengo ya msingi TBC inayopaswa kuyatimiza.

Kipindi cha nyuma kulikuwa na mzozo kwanini inaitwa TBC? TBC ni Tanzania Broadcasting Corporation - Kwanini television ya Taifa iitwe kwa kiingereza kama lengo lake ni kukuza kiswahili?

Hichi kipindi cha "This week in perspective" pia nacho kilishazungumziwa sana tu, lakini huyu mzee mwenyewe Mzee Simbei ameonyesha kutopenda idea ya kukitangaza kwa kiswahili.

Ukweli ni kwamba, watanzania tumefika pahala hatujali tena "nani anajua kiingereza na nani hajui". Alimradi tu wewe unajua basi unadhani kila mtu anajua na hatuwajali wale wasiojua!

Hata matangazo muhimu kama ya UKIMWI au MALARIA etc mengine yapo kwa kiingereza, achilia mbali document nyingi za Serikali etc.

Tatizo jingine la hiki kipindi ni uwezo wa kujieleza wa interviewers kwa kiingereza. Kuna wakati unafika mtu ana struggle kutoa point, achilia mbali pronounciation mbaya .... so nashindwa hata mimi kuelewa ni kwa nini ung'ang'anie kiingereza pasipo sababu za msingi na wakati watanzania walio wengi wanafahamu kiswahili fasaha na si kiingereza.
 
mzee mawazo yako yametulia sana kila ulichokisema ni kweli tupu ila tatizo ni mwendeshaji amezaliwa zamani kipindi kiingereza kinatamba hivyo amejisahau kuwa sasa hivi kiswahili kina hadhi sawa na kiingereza,hivyo ukoloni bado umemkaa kichwani
 
Nimeguswa sana na mtazamo chanya wa proffesor Safari (ktk pindi la this week in perspective) kuhusu tendo la wabunge wa chadema ku-walk out bungeni. Mwanazuoni huyo ameonyesha ku support ushujaa huo wa wabunge wa CDM kwa kutazama dhumuni na si tendo peke yake. Huyu ni tofauti na wengi wasio penda kufikiri.

Kwa kusisitiza mwanazuoni huyo aliyebobea ktk sheria ameonyesha kuwa tendo hilo siyo kosa kisheria bali ni njia sahihi ya kidemocrasia kwa mtu kuonyesha hisia zake juu ya jambo fulani kwa njia ya amani. Huyu ni prof. Safari na siyo Ahmad Rashid, aliyepelekea "me to have a second thought about Cuf".

Kafulila unasemaje hapo?
 
Wazee tunaowaamini kwa masuala ya sheria na uchambuzi wa masuala nyeti Jaji Mkuu Mhe. Augustino Ramadhani na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Sinde Warioba walishetoa msimamo wao kuhusu suala la wabunge wa CDM kususia hotuba ya rais. Walichoshindwa kutamka (kwa sababu inayoeleweka) ni kuwa wanawaunga mkono wabunge wa CDM. Lakini wote walisema kwamba wabunge wa CDM hawakufanya kosa lolote na hawakuvunja kipengele chochote cha sheria. Walichofanya ni kutumia haki yao ya kikatiba.

Yeyote anayezungumza kinyume cha msimamo huo, anabwabwaja tu kwa hasira inayotokana na maslahi anayopata kutoka kwa rais na chama chake. Watu kama akina chikigati wanadhani bungeni ni jeshini ambapo kila kitu ni 'ndiyo afande', hawajui na wala hawana muda wa kupitia vipengele vya sheria husika. Akina hamad rashid kinachowasumbua ni njaa tu. Kama siyo njaa chama chake cha kafu kingewezaje kufunga 'ndoa ya mkeka' na ccm!!!! Wana JF tuwapuuze watu hao wa aina ya kina hamad na chiligati wanaofikiri kwa kutumia tumbo badala ya ubongo.
 
Hii ni habari ya bilauri kuwa imejaa nusu au tupu nusu.

CHADEMA wanastahili pongezi kwa kuthubutu kusema uozo ulio katika katiba na mfumo mzima wa uchaguzi. Kwa hakika hili ni suala la kujivunia kwa wnamapinduzi wote, na limeweka rekodi mpya katika siasa za Tanzania, hili nataka niliseme kwanza kabisa ili chochote nitakachosema baadaye kisije kuchukuliwa kama kutoelewa umuhimu wa kitendo hiki.

Lakini wengine tunawalaumu kwa kutofanya cha kutosha wala kupanga vizuri mambo yao. Ukitaka kuonyesha msimamo tu unaweza kuonyesha msimamo mpaka utachoka, CCM kama hawana haya ya kubadilika kutokana na vitendo hivi vya kuonyesha msimamo watabaki hivyo.

Zaidi kinachohitajika ni hatua zenye mikakati ya kisheria na kisiasa, CHADEMA wana mkakati gani wa kutekeleza mikakati hii?

Siku hizi chache zilizopita zimenionyesha CHADEMA ambayo ilitaka kufanya kitu kikubwa (kutomtambua rais) ikashindwa ikabidi ianze ku fumble na kuunga unga huku inaenda, mara hatumtambui rais, mara tunamtambua lakini hatutambui matokeo (WTF ?). Mara wabunge wengine wamesusia kumsusia rais, ili mradi chama kinaonekana hakina ukomavu wa kutosha.

Ni kweli kwamba CHADEMA hawajavunja sheria katika kumsusia rais bungeni, lakini wengine wanaweza kusema hawajaweka sheria mpya vile vile.

Mimi ningeshukuru hata CHADEMA wangevunja sheria, kama sheria zenyewe ni dhalimu, ili mradi wauondoe udhalimu huu. Huwezi ku ininstall operating system ya computer wakati unaitumia hiyo hiyo OS, huwezi kuing'oa nyumba wakati uko ndani ya hiyo nyumba, huwezi kurusha roketi iende kwenye mwezi kwa kuheshimu na kutoipita nguvu ya uvutano ya dunia inayokufunga hapa duniani, huwezi kuushinda utawala dhalimu na katiba yake kwa kutumia katiba hiyo hiyo dhalimu.

Uhuru hauombwi, unachukuliwa. CHADEMA wamejiandaa kuchukua uhuru/ Ushindi wao (kama wanashinda) ? Au wanangojea mpaka CCM watake ? Na CCM wasipotaka kuleta mabadiliko ya katiba mpaka 2015 hali iwe hii hii CHADEMA watafanya nini ?
 
Kiranga, niko na wewe kwenye hili, nilisema mahali 'Chadema Hawajajipanga!' walinishukia, simply because washabiki wao, wanapenda tuu Chadema kiimbiwe nyimbo za sifa na mapambio.

Kiranga, natofautiana na wewe kidogo kwenye mambo mawili, la kwanza nakubaliana nawe huku nikitofautiana nawe ni hili la uhuru, ni kweli, uhuru hauombwi, kama ilivyo haki, wala hauletewi kwenye kisahani cha chai,Kiranga umesema uhuru unachukuliwi as if uko pale unakungojea wewe ujichukulie, mimi naongezea kuwa uhuru, unadaiwa na ikibidi unapiganiwa, hii sasa ndio iwe ajenda ya Chadema kwenye kudai katiba mpya.

Tofauti nyingine na wewe, ni kuwa unaamini ili upambane, ni lazima utoke nje, mtazamo wangu, ili kupambana sio lazima utoke nje, you can fight from within, yaani unapambana kuanzia ndani, ndio maana nimeipongeza Chadema kwa mafanikio iliyoyapata. Nimemuomba Dr. Slaa ajitokeze hadharani atuambie japo asante kwa hicho hicho kidogo kilichopatikana baada ya kuchakachuliwa. 'If you don't get what you want, just take what you get!', usisuse!.

Kwa kufuata mtazamo wako, Chadema walitakiwa kwanza kupambana wakiwa nje mpaka uwanja wa mapambano usawazishwe, ndipo waingie kwenye mapambano. Kitendo cha Chadema kuingia kwenye mapambano, huku kikijua fika kinagombea kisu huku mmoja ameshika mpini na mwingine kwenye makali, matokeo utayajua tuu hata kabla, hivyo wamefanya vema kukubali kuingia, na japo kisu kimewakata,wamefanikiwa kupunguza kidogo ile grip ya kwenye mpini, hivyo mshika mpini anaanza kuteleza na mwisho atapokonywa.

Sasa Chadema wanatakiwa kutumia hiyo nguvu yake Bungeni, japo ndogo, kupambana from within,japo watakumbana na vizingiti vingi vya uchache wao na hii fragmented opposition, lakini wananchi watawaelewa wanapigania nini na come 2015, watawakataa washika mpini kwa nguvu zote na watapokonywa hicho kisu!
 
Sawa kabisa naunga mkono 100% lakini hili la katiba haifai 2015 kufanya uchanguzi na katiba hii,hii na NEC hii hii :thinking:
 
Mkuu Pasco nasikia mikutano yote ya CHADEMA imepigwa marufuku nchi nzima.
 
Hiki Kipindi ni kizuri sana lakini kingeendeshwa kwa kiswahili pia kwani kuna wasikilizaji wengi sana kinawaacha nje kwani zaidi ya asilimia 90% ya watz Kimombo hakipandi
 
Nakumbuka Prof. Saffari ni mtu pekee aliyejitokeza kujaribu ku-challenge leadership ya CUF. Lakini alishindwa kumuengua Lipumba kama mwenyekiti/mgombea Urais wa CUF. Chama cha CUF sasa kimeshatekwa rasmi na CCM. Kime cease kuwa chama cha upinzani baada kuingia kwenye coalition government Zanzibar. CUF is effectively CCM "B" na kitakuwa kinapingana na maamuzi ya CHADEMA daima. Ni dhahiri kuwa wabunge wa CUF wangepinga walkout ya CHADEMA. Pia wabunge wa CUF wamekataa kushiriki kuunda kambi ya upinzani Bungeni na walimpigia kura Anne Makinda wa CCM kuwa spika badala ya Mabere Marando wa CHADEMA.

Ukweli ndiyo huo. Naona huo mdahalo wa leo kati ya mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe na kiongozi wa CUF Hamad Rashid will just be a waste of time and money.

CUF wanapokea amri kutoka kwa CCM.
 
Sawa kabisa naunga mkono 100% lakini hili la katiba haifai 2015 kufanya uchanguzi na katiba hii,hii na NEC hii hii :thinking:
Ndiyo maana nataka kujua kama utawala waCCM hautabadili kitu, CHADEMA itafanya nini?

Hizi habari za marufuku mikutano ya CHADEMA ni uhakika au ?
 
waungwana, hivi huyu baba anayeratibu kipindi hicho hapo juu(This week in perspective) audience yake huwa anawalenga akina nani. Hivi majadiliano yale ni kwa faida ya nani, wangapi wanamsikiliza kwa kiingereza. Kinaweza kuwa kipindi kizuri kwa mada zake lakini wangapi wanampata anachokiongea. Sidhani kama outside Tanzania the discussion is of any interest to them!!! I stand to be corrected!!!!!
 
Umenena vyema mkubwa,mi nadhani anawalenga wale anaokuwa nao kwenye studio,mtanzania wa shule ya kata sijui kama wanaangalia hicho kipindi
 
Walengwa ni wewe na mimi na wageni wengine walioko Tanzania wasiojua Kiswahili vizuri..
 
Walengwa ni wananchi wote hasa wanaoielewa kiingereza. Mi nadhani kulikuwa na mbinu mahususi kile kipindi kurushwa kwa kiingereza, kutokana critical points zinazojadiliwa, na kuwanyima baadhi ya madikteta wa serikali ya magamba wasijue kinachojadiliwa. Si mnajua wengi vilaza?
 
Mkuu upo sahihi kabisa. Hiki kipindi kwangu mimi ni 'lost opporunity'. wanakuwa na mada nzuri sana na washiriki wenye uelewa mkubwa tatizo ni lugha! Sijui wanakusudia nini maana hata kama wanawalenga mabalozi wa nchi za nje tayari wanayajua vema madudu ya Tanzania kuliko hata sasa, after all wanatulisha. Hiki kipindi kingekuwa 'talk of the town' kama kingekuwa kwa kiswahili.
 
kipindi kinahusu watanzania wote lakini wenye minimum literacy level, meaning kama unaweza kusoma na kuandika kwa lugha ya kiingereza,basi utaweza kufuatilia kinachozungumzwa. Tanzania inabidi itambue we are not living in isolation anymore, kuna watu wa kila aina hapa nchini, kwa kifupi tunatakiwa tuende sawa na mabadiliko, ama sivyo tutaendelea kuburuzwa na magamba ambao wao siku zote mtaji wao mkubwa ni ujinga wa mtanzania.
 
Back
Top Bottom