This week in Perspective: Kipindi kinamlenga nani?

This week in Perspective: Kipindi kinamlenga nani?

Pamoja na mapungufu yaliyoainishwa hapo juu, kubwa zaidi ni pale mwenyekiti anapoonesha kuwa anajua kila kitu, kwa ujumla hata kwa kiingereza kipindi hakina mvuto.
 
halafu viongozi wetu wanasema kiswahili kitumike kufundisha mpaka chuo kikuu,wanazidi kujichanganya,hakuna msimamo unaoeleweka kwenye sera ya elimu
 
Nani anajua kitu ambacho huwa wanajadili?Kuna wakati huwa wanajadili sana maisha ya watanzania.Wamesahau kuwa watanzania weng hawajui kingereza.Nadhani ni bora wabadili lugha na kuwa kiswahili.

Tatizo hapa ni lugha? Hiki kipindi wanalenga kundi la watazamaji wanaojua kiingereza, mbona wanayo midahalo mingi ya Kiswahili?
 
Tatizo hapa ni lugha? Hiki kipindi wanalenga kundi la watazamaji wanaojua kiingereza, mbona wanayo midahalo mingi ya Kiswahili?
Kwa mfano mdahalo gani wa kiswahili unaendeshwa na TBC Huwa na hoja nzito zenye maana?
 
Pamoja na mapungufu yaliyoainishwa hapo juu, kubwa zaidi ni pale mwenyekiti anapoonesha kuwa anajua kila kitu, kwa ujumla hata kwa kiingereza kipindi hakina mvuto.

kumbe tupo wengi tusiopenda hii lugha ya kitumwa.yule mzee huwa anajifanya yeye ana akili kuliko wageni wote anaowaalika.
 
Tizo1, kasumba ya matumizi ya lugha ya Kiingereza imetufikisha pabaya, mikutano yote ya maana, semina, warsha na makongamano, yote huendeshwa kwa Kiingereza.

Juzi juzi nimehudhuria mkutano wa uwekezaji Ziwa Tanganyika uliofanyikia Sumbawanga, waliwahamasisha wakazi wa kanda yote hiyo kujitokeza kwa wingi, watu walijitokeza mamia kwa maelfu, wakawafungia vipaza sauti. Mkutano kuanza, eti unaendeshwa Kiingereza huku ukitangazwa live na TBC!, kisa, eti tumewaalika mabalozi na wawekezaji wakubwa!. Mada karibu zote zimeandikwa Kiingereza!.

dah kweli kazi!hawakuleta hata watu wa kutafsir?kweli shida tupu.
 
Jamani mi ninavyofahamu tbc....ni televisioni ya taifa sasa hiki kipindi cha this week in perspective kinachorusha kila ijumaa.....ambacho hujadili mambo mengi kuhusu taifa letu.....ila kinachonikera ni kutumia lugha ya kiingereza kujadili mambo kwani watanzania wengi hawafahamu hii lugha tunaomba wadau wa tbc....msikilize maoni yetu kwani hamuwatendei haki watanzania wasiojua kiingereza
 
This week in perspective ni kipindi kinachorushwa na tbc1 chini ya mtangazaji mahiri wakishirikishwa wasomi na wazalendo wa nchi hii wakiwemo akina mzee lwaitama,prof baregu.Hakika ni kipipindi kinachonijenga mimi kama mwanasiasa mchanga na kunifanya niyajue mambo mengi yahusuyo nchi yangu.vijana wenzangu na hasa wenye malengo ya kujiunga na harakati za kukomboa nchi hii nawasihi wapambanaji wenzangu msikikose hiki kipindi.
 
Kwl bana! Tupo pamoja hapo.nampenda maswli yake hakuna jazba.I wsh kirushwe na channel zote
 
Ni kipindi kizuri sana kwa ambao wamegoma kuangalia TBC wanakosa mengi kwenye kipindi hiki
 
Kwa mfano mdahalo gani wa kiswahili unaendeshwa na TBC Huwa na hoja nzito zenye maana?

Ukiidadavua inaweza pata hitimisho ambalo hakuna mtu atalipenda lakini laweza kuwa ni kweli kabisa, ni hitimisho linaloweza kumalizia na ' watawala wetu kwa kiasi kikubwa ni wachoyo, hii ni mbinu na mkakati wa makusudi ya kupunguza kwa kadri inavyowezekana idadi ya watawaliwa(wananji) wanaojua mfumo wao. Wengi wasijue haki zao.wengi waone bila ccm ni vita, wengi waseme bado kila aendae ikulu ni mtakatifu na mwizi wa kuku ni wa kupigwa mawe hadi afe na akichelewa kufa amwagiwe petroli na kuchomwa moto lakini fisadi serikalini anaye iba mabilioni ya pesa yao asifiwe na kubembelezwa!

Mfumo wa utumwa wa aina yake.
 
kwanza kabisa napongeza iki kipindi sababu ni kizuri na kinaongelea mambo ya msingi sana kuhusu wananchi wa tanzania.lakin iki kipind kinaendeshwa kwa lugha ya kiingereza ambapo sina uhakika kama watanzania wa kawaida wanaelewa japo kipindi kinawagusa sana.
katika nchi zote ambazo zimeendelea,kama channel ni ya english basi lugha za kuendeshea vipind uwa ni english tu bila kuchanganya,kama ni kiswahili basi uwa ni kiswahili.
kipindi ni kizuri sana lakini nimegundua watanzania wengi ubadilisha channel mara tu kipindi icho kinapoanza sababu awaelewi lugha inayozungumzwa umo wakati mambo yanayozungumzwa ni ya msingi sana na ingekuwa vizuri kama wangesikiliza.
bado sijafahamu kipind kinamlenga nani
kipind irushwa usiku siku ya ijumaaa,tbc1
 
Kipindi kinawalenga wanaojua kiingereza na wale wasiosoma magazeti ya Shigongo baaasi,wao ndio angalau wanakula ile keki ya taifa.
 
Acheni mambo yenu kujifanya hamjui hku mnajua hta mahakamani hukumu inaandikwa kwa kiingereza
 
mimi huwa sikosi hiki kipindi, vijana wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa ya wazee!
 
Acheni mambo yenu kujifanya hamjui hku mnajua hta mahakamani hukumu inaandikwa kwa kiingereza

mkuu umesahau juzi watu waligoma mahakamani rufaa ya Lema kusomwa kwa kiingereza hadi ikasomwa kwa kiswahili mwanzo mwisho.!
 
Kinawalenga wanaojua KIDHUNGU tu!
 
Wabadilishe lugha wengi wanufaike, sababu kama wamelenga ujumbe uwafikie mpaka walioko mashambani itakuwa rahisi zaidi
 
Wabadilishe lugha wengi wanufaike, sababu kama wamelenga ujumbe uwafikie mpaka walioko mashambani itakuwa rahisi zaidi

kweli sababu mambo yanayoongelewa yanamgusa mtanzania wa kawaida,sema wengi wanachange channel,kipind kikianza
 
Back
Top Bottom