Ndugu wanajamvi, naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Mida ya saa 10 jioni hii katika eneo la Uswahilini hapa Arusha (Mjini), maaskari wa kituo cha Murieti wamemkamata mke wangu nakumpeleka kituoni kisa nyumba tunayoishi haina matundu yakutosha ya vyoo.
Ukweli uliopo:
1. Nyumba hii huyu mmiliki mpya ameinunua kama miezi 2 iliyopita na katika muda huu mchache katuunganishia maji safi na kafanya utaratibu wote na hivi sasa tunasuburi kuunganishwa kwenye bomba la maji taka. Nyumba hii tayari AUWSA wameshaweka alama kwamba wakati wowote wataiunganisha kwenye mfumo wa maji taka.
2. Mke wangu kakabidhiwa kukusanya kodi ya mwenye nyumba hapa tunayoishi, na siye mmiliki. Mmiliki haishi na sisi. Na hatujui anapoishi. Mke wangu kampigia simu kasema yupo safarini.
3.Kuna matundu 2, ila moja mmiliki mpya kaambiwa asubiri mpaka idara ya maji wakianza kuunganisha mfumo wa maji taka basi watampa maelekezo jinsi yakuiunganisha na mfumo wao.
4. Tangu niishi kwenye hii nyumba, ambapo ni takribani mwaka wa 4 huu, hatujawahi kufwatwa kwa jambo kama hili, ukizingatia kwamba huyu mmiliki mpya huwa ananyonya mara kwa mara choo kikijaa katika nyumba hii. Na leo walivyokuja hawakukuta uharibifu wowote wakimazingira.
Naombeni msaada wenu ndugu zanguni. Nifanyeje???