This is Rostam I know... The Story Behind the Man

IO,
Ukitumia akili yako tu ya kawaida kufanya analysis ya mambo utagundua kuwa hapa kuna undanganyifu wa wazi. Siju kama inaingia akili kweli haya majina (Rostom A. Sakarri, Rostam Sakarri, Rustom Aziz Sakarri, Rustam Sakarri na Rustam Sakaari) yakafanana kwa kubadili au kuhamisha herufi kutoka jina moja kwenda jina lingine kwa kiasi hicho. Kwa hakika RA ni balaa. Atalifilisi hili taifa kama hatashughulikiwa. Anapojitetea kuwa yeye ni mzalendo lakini kwa matendo yake haya anakana na kusema yeye yupo hapa TZ kuchuma na kudhoofisha uchumi wa Tanzania na kama inavyojulikana yeye ana uraia wa nchi tatu (TZ, Iran na Canada) kwahiyo yuko mguu pande. Ooooooh GOD forbid.
Upo sawa, kwa wenzetu ukitaka ku-register kampuni lazima utaje passport number au identity card yako na uthibitishe directors/ shareholders wanaishi na wamefikia umri wa utu uzima. Hapa kwetu unaweza wewe uaaandika chochote na kutoa pesa na ku-register. Hilo tu la majina fake (kama kweli ni feki) basi Rostam yupo guilty tayari!!
 
Mie hapo ndipo sielewi kabisa,hivi mimi hapa naweza kwenda kwenda kusajili kampuni bila kutoa docu zozote?
 
huyu hajakoma sio, tindikali haikumtosha, safari hii watakuua.

Not a nice thing to say..is it?:rolleyes:
Watu wa namna hii ndo wanahitakika Tz kusudi mambo yabadilike. Sio wanaojificha nyuma ya computer na kutumia majina alias na kujifanya wajuaji. Hawa ndo wapiganaji katika taifa letu and WE SHOULD SALUTE THEM!
 
huwa napata taabu sana kuona kuwa m'baya ni Rostam Aziz, lets say anayofanya ni ujambazi au ufisadi,je wale wanaompa hiyo 'go ahead ' ni akina nani?? na tuwaiteje wao??
 
- Sometimes hawa huwa wanachukua habari hapa JF, hizi si tumezisema sana huko nyuma kwamba huyu Rostam hajasajili jina lake kama owner wa kampuni mahali popote, naona habari zinajirudia tena.

____________________________

Field Marshall ES:

Inawezekana wanachukuwa vyanzo hapa lakini wao wamekwenda mbali zaidi. Isitoshe inabidi tuwashukuru kwa kuzimwaga habari kwenye gazeti hilo (Mwanahalisi) lenye circulation kubwa kuliko magazeti yote nchini -- nasikia huchapa nakala 75,000 kila wiki. Wanaoingia humu JF sidhani kama wanafika robo ya hao.

Lakini pia ni dhahiri kabisa kwamba huyu RA daima amekuwa na dhamira zisizo takatifu dhidi ya nchi hii na wananchi wake -- ama sivyo atueleze sababu hasa ya kujificha nyuma ya majina ya wengine iingawa mimi naamini mengi ya majina hayo ni feki tu -- yaani hakuna watu halisi..

Kama ilivyoandikwa huko nyuma hawezi kuthibitisha kinagaubaga majigambo yake kwamba kampuni zake zimeajiri watu 6,000 au kwamba analipa mabilioni kila mwaka kama kodi serikalini. Hawezi, maana tunaweza ku-allege, bila wasiwasi kwamba hizo kampuni siyo zake, na hawezi kulazimisha kusema ni zake wakati hakuna ushahidi wa kimaandishi. Nasikia hata ofisi hana -- anababaisha tu mara hapa, mara kule.

Ni tapeli mkubwa hapa nchini na inasikitisha kuona vyombo vyetu vya dola vinakosa fyoko ya kumgusa.

Kwa mfano, inaaminika kwamba iwapo Mengi angewataja tu "mapapa" wa kizalendo (yaani siyo hao wenye asili ya Kiasia), sidhani kama akina Mkuchika, Maelezo, TCRA etc wangemsumbua Mengi. Kilichomponza Mengi ni kuwagusa wasiogusika katika nchi hii -- hao weupe.

Hawa na wengine wanaomtetea RA wanadhihirisha kweli ule usemi "Miafrika ndiyo tulivyo!" Hatutaendelea daima kwani bado tuko wanyonge sana. Nyerere angalau alijaribu kuondoa unyonge huu lakini sasa unarudi kwa kasi.

Mkuu cha kusikitisha ni kuwa hiyo miafrika ni mimi na wewe pia. Mbaya zaidi hata hao waliojuu tunaowaita kaka na wengine baba, wanajua hilo kuwa jamaa amewiweka nchi mkononi, na hakuna kinachofanyika. Na ubaya ni kwamba unawezashangaa kuwa hata 2010 ataendelea na himaya yake. Kweli ndivyo tulivyo. Tunajua mwizi na anavyoiba, lakini tunajifanya hatuoni, tunamtetea na kumlinda.
 
mi sina hata la kusema jamaa ni kifaru hata huko atown ana mabiashara yamawe maduka na .kadhalika mi namuomba asaidie mashule yale watoto wanakaa chini na vilema wanahangaika hawana ajira wala mlo wasiku maana nae atajibu huko mbele ya mungu kujilimbikizia mijimali hadi wapi mh mh mh

Unamuomba mwizi asaidie ili ahalalishe wizi wake? Yeye hayuko interested na kusaidia chochote katika nchi hii isipokuwa kuiba na kujilimbikizia hata kama ni kwa kusacrifice maisha ya watz wote. Hatuna haja ya kuomba misaada, kwa kuwa hizo ni fedha za jasho la watz, tunachotakiwa ni kumfilisi na kumfunga kwa mujibu wa sheria. Tatizo ni hapo ambapo amejitengenezea mazingira ya kutoguswa, kwa kutojiingiza yeye mwenyewe moja kwa moja, na kununua na kumiliki hata dola. Kama dhamira yake ni safi kwa nini haweki jina lake katika usajili wa makampuni yake. Lazima tukubaliane kuwa huyu ni mtu hatari sana, analoot kila kitu mpaka tubakie masikini wa kutupwa kabisa. Hata kama kuna watu anawapa kula kwa kuwaajiri au kuwapa fedha wajue kuwa wanadeal na mtu hatari atakayefanya lolote kutajirika hata kama ni kwa kuwasacrifice wao, cha msingi tuungane kuondoa elements zote za ufisadi wa namna hii, sio kwake yeye tu na wote wanaohusika. Ifike siku sheria iwe juu ya kila mwananchi hata kama mwananchi huyo ni Rais au ni RA.
 
Hizo habari ni another proof kuwa mheshimiwa mbunge wa Igunga amewaweka mfukoni:
1. wananchi wa Igunga
2. viongozi wa serikali, wakiongozwa na waziri simba, mawaziri wenzie, Mkuchika, n.k.
3. kamati ndogo, kamati ya kati na hata kamati kubwa ya usalama wa nchi
4. Brela na vibaraka wake
5. TCRA, Maelezo
6. TAKURUKU, Polisi, DPP
7. Na wengine wengi ambao hatujawajua, lakini wenyewe wanajijua!

RA una mfuko wenye kina kirefu! Hongera!
 
Tatizo hapa ni mkuu wa nchi ambaye anaonekana kama ni kiboko ya double standards.
Nadhani kabla hajatangaza kuwa biashara na uongozi viwe mbali mbali,yeye na swahiba wake tayari walijua cha kufanya,hizo mali zi zao wote na wamehakikishiana kuwa watanzania ni wajinga hivyo siasa iendelee kutumika kwenye kuhalalisha maovu yao,kwa maana kwamba RA si mfanyabiashara bali mwanasiasa haiwezekani uhujumu wote huu wa mali za nchi unyamaziwe na wakuu wa nchi kama vile hakuna lolote na huku wakisafiri kwenda kuomba misaada ambayo inturn wanaipeleka kwenye kampuni hizo zenye majina ya bandia..Inawezekana mali hizo ni zao wote,haiwezekani uhujumu wote huu wa nchi unyamaziwe kimya na wakuu kama hawanufaiki nao....Inasikitisha sana kuona wananchi tunadharauliwa kiasi hicho,wako wapi wazalendo waliomo ndani ya system ambao hawanufaiki na ufisadi na ambao hawataki kunufaika nao? Hivi inawezekana kuwa wote walioko ndani ya system na wana nafasi ya kutoa mchango wao wameridhika na kufanywa wajinga kama ilivyo kwa wananchi wote ambao bado wanaichagua ccm?
Haya yaliyoandikwa hapo juu kwenye makala ya mwanahalisi ni mambo ambayo mtu mwenye akili timamu atajiuliza kama ni kweli yanatokea na kweli ni ngumu kuamini this is true,yani ni ngumu.
 
Mie hapo ndipo sielewi kabisa,hivi mimi hapa naweza kwenda kwenda kusajili kampuni bila kutoa docu zozote?

Ndugu yangu, yaani Bongo yetu wanaangalia ni nani anayesajili hiyo Kampuni. Akienda kabwela tu atakutana na vizingiti vingi kupita kawaida hata kama yuko genuine lakini basi tu kwa vile hajulikani au inakubidi atoe chochote. Kwa kweli kwa mtaji huu inabidi BRELA imulikwe. Haiwezekani watu kuichezea nchi kiasi hiki. No no no no no no!
 
Tusisahau richmod ilikuwa na bank account kabla hata ya incorporation, sasa nenda wewe au mimi bank bila tin number, incoporation certificate, business licence huone kama utapata bank account..labda deci! hahahahahha
 
Hizo habari ni another proof kuwa mheshimiwa mbunge wa Igunga amewaweka mfukoni:
1. wananchi wa Igunga
2. viongozi wa serikali, wakiongozwa na waziri simba, mawaziri wenzie, Mkuchika, n.k.
3. kamati ndogo, kamati ya kati na hata kamati kubwa ya usalama wa nchi
4. Brela na vibaraka wake
5. TCRA, Maelezo
6. TAKURUKU, Polisi, DPP
7. Na wengine wengi ambao hatujawajua, lakini wenyewe wanajijua!

RA una mfuko wenye kina kirefu! Hongera!

Uko sahihi kabisa mkuu,
Yaani RA ana uwezo wa kuamua nini kifanyike hapa nchini na hakuna wa kupinga. Sasa hivi tunaona mswaada wa sheria unaondaliwa kwenda bungeni kuwapunguzia watu idadi ya umiliki wa vyombo vya habari. Yaani uchague kimoja tu aidha kuwa na magazeti au Television tu na si vyote. Na hapa unaona kabisa wanamlenga Mengi na unaiona kabisa nguvu ya Kingmaker RA nyuma yake. Nakumbuka wakati Zakhia Meghi akiwa waziri wa fedha aliweka utaratibu kuwa wafanyabiashara wakubwa mizigo yao haitakuwa inakaguliwa. Sasa naanza kupata picha kuwa huenda pia ilikuwa ni kum-favour RA kwenye biashara yake haramu ya pembe za Ndovu. Yaani hii nchi sijui tunaenda api mpaka huyu jamaa (RA) atakapokuwa ameikongolosha ndo tutabaki tunalia. Tembo wanatoweka na mali ya umma zinaibiwa.
 
Tusisahau richmod ilikuwa na bank account kabla hata ya incorporation, sasa nenda wewe au mimi bank bila tin number, incoporation certificate, business licence huone kama utapata bank account..labda deci! hahahahahha

I support you Kapinga,
Yaani uvunjaji wa sheria uko wazi wazi namna ile lakini watu hawachukuliwi hatua yoyote. Mtu hana document yoyote ya kampuni yake na anaruhusiwa kufungua akaunti benki, bado leo watu wanatuambia Richmond was a genuine Company. Nonesense and shame on them!
 
Unamuomba mwizi asaidie ili ahalalishe wizi wake? Yeye hayuko interested na kusaidia chochote katika nchi hii isipokuwa kuiba na kujilimbikizia hata kama ni kwa kusacrifice maisha ya watz wote. Hatuna haja ya kuomba misaada, kwa kuwa hizo ni fedha za jasho la watz, tunachotakiwa ni kumfilisi na kumfunga kwa mujibu wa sheria. Tatizo ni hapo ambapo amejitengenezea mazingira ya kutoguswa, kwa kutojiingiza yeye mwenyewe moja kwa moja, na kununua na kumiliki hata dola. Kama dhamira yake ni safi kwa nini haweki jina lake katika usajili wa makampuni yake. Lazima tukubaliane kuwa huyu ni mtu hatari sana, analoot kila kitu mpaka tubakie masikini wa kutupwa kabisa. Hata kama kuna watu anawapa kula kwa kuwaajiri au kuwapa fedha wajue kuwa wanadeal na mtu hatari atakayefanya lolote kutajirika hata kama ni kwa kuwasacrifice wao, cha msingi tuungane kuondoa elements zote za ufisadi wa namna hii, sio kwake yeye tu na wote wanaohusika. Ifike siku sheria iwe juu ya kila mwananchi hata kama mwananchi huyo ni Rais au ni RA.

Kabisa mkuu,
Huyu RA ni mtu hatari mno na hii nchi anaifilisi. Tatizo kubwa analo Kikwete mwenyewe. Yaani hata kama kamuweka madarakani jamani yampasa (Kikwete) sasa amwambie "rafiki yangu sasa hii ni hatari na si sawa". Hata kama ingekuwa ni favour basi ziwe katika uhalisia na si kijambazi namna hii. Kama ni biashara afanye kihalali na alipe kodi vizuri nafikiri hata sisi wananchi tusingepiga kelele na tungemwona kuwa ni mzalendo wa kweli. Lakini kwa haya anayotufanyia watanzania, sikubali kabisa akisema kuwa yeye ni Mzalendo. Uzalendo uko wapi? Wazalendo hufanya mambo yao kihalali kwa maendeleo ya nchi zao, lakini huyu ni mwizi na fisadi mkubwa, mfilisi wa nchi yetu.
 
Hii ndio Tanzania yetu..Mtu kama Rostam pamoja na watu kufahamu yote haya bado wewe mwananchi unatakiwa kuleta ushahidi. yaani wewe mwananchi ndio unatakiwa uthibitishe kuwa majina hayo sii ya Rostam penye haki, na ni ya Rostam napokuwa na tatizo.. Hivyo vitambulisho, photo na sijui passport ya ujsajili huko Brela pia wewe mwananchi unatakiwa uwe na nakala kama ushahidi wako, vile vile ukumbuke utakuwa umevunja sheria ya kuwa na nyaraka za siri za serikali..
Kazi ipo.....sheria za Tanzania sii msumeno bali ni shoka la Msolopagas
 
huyo jamaa ndio muamba wa ccm sasa hivi.na ukimchunguza maovu yake yote kwa kina utakuja kuibua viongozi wa kubwa wengi sana waliojaa maovu kama yeye.sera ya ccm ya kujaribu kumuangamiza mtu yoyote anayetaka kutetea maslahi ya taifa itakuja kufikia mwisho tu siku moja,na hio siku ndio tanzania itakuwa imejikomboa kutoka viongozi wabinafsi wasiojali maslahi wa nchi hii.
 
Wanamapinduzi wa kweli nchi hii wako wapi wale wasiofuata itikadi lakini ukweli? Hakuna watu wanaoweza kujitolea kufa kwa kukataa upuuzi huu wa RA na watu wake by using any means?

Wanaoweza kujitolea wako wengi. Ukweli ni kwamba huhitaji hata kuwaalika. Wameshatoka wako wanaelekea. Utasikia kesho!
 
Magazeti ya kimatifa nayo yanahoji uhalaliwa bwana mkubwa kuwa na makampuni kama uyoga yasiyojulikana chanzo chake na wale proper registration ilihali serikali ya TZ haisemi chochote jamani aliyesoma habari hii kwa undani tutashukuru kwa mchango wake......
 
Hapa anazungumziwa ROSTAM AZIZ mwanasiasa na mfanyabiashara 'hatari' aliyejipatia fedha nyingi Tanzania kwa kutumia udhaifu wa viongozi na wananchi wake waliolala fofofo huku nchi yao ikitafunwa. Huyu hawezi kutumia jina lake kwenye makampuni yake kwa vile ana machale sana. Anajua kuna siku waTZ wataamka toka usingizini na kuanza kumshughulikia kutokana na kuwaibia.
Amevuna sana Tz na sasa taarifa zinasema anamiliki benki kadhaa nchi za nje ikiwemo Dubai. Pia ana vitega uchumi vingi vya kutisha katika nchi mbalimbali. Anawekeza nje kwa sababu anaajijua sio raia wa nchi hii na wakati wowote anaweza kutimkia kwao Iran au sehemu nyingine duniani ambako amenunua uraia.
Nashangazwa sana na baadhi ya waTz wenzetu kumtetea mtu huyu hatari, ambaye sasa anaanza kushtukiwa hata kimataifa.
 
Back
Top Bottom