This is Rostam I know... The Story Behind the Man

Sometimes unaweza ukakufuru Mungu kwa kuumbwa Mtanzania.
Mungu apishilie mbali.
 

Usituhamishe kwenye hoja ,hii sio hadithi hata kama ni hadithi vipi kuhusu ujasusi
 
 
ya kagoda yameisha kwisha kwani hat mawakili wetu na majaji sio waaminifu, Mfano wanasheria wetu waoga na wanapenda sana cha juu kuliko kuhurumia nchi yao zidi ya wahujumu uchumi, kama kweli wanauchungu na nchi yetu angejitokeza mwanasheria kuwashitaki mafisadi kama Kagoda, lakini badala yake wanawashauri wafiche pesa na kuwaambia kuwa wakizionyesha au kuzirudisha kama alivyosema JK watakuwa ameonyesha ushahidi kuwa waliiba, nasikia kagoda karudisha baadhi hivyo hakuna uwezekano tena wa kuishitaki kwani wamekamilisha masharti ya Rais
 
Hiyo mitambo Rostam alikabidhiwa mwaka gani?Baada ya kufa Mwalimu au Kabla?Mwalimu alistaafu Urais 1985!Na hiyo Caspian ilianzishwa lini na kupewa hizo tenda katika migodi?
Hivi Kikwete na wake wangapi?Mara Al kharusy mara Mkwe wa Mama Megji mara huyo mara yule!This is too much kwa kweli!
 
Mkuu umesema mengi ila tatizo hasa la rostam ni nini katika insha yako?

Ni kupewa mitambo na Irani au ni Kuchimba madini au ni kuwa mwakilishi wa nchi ya irani?

mimi naona aibu sana kujaribu kujenga hoja ambazo sina uthibitisho nazo mezani sijui wenzangu.
 
Nimejaribu kupitia Habari ya BWana Iwangwa, lakini mimi nina mtazamo unaopingana kidogo na mtoa mada
naomba ieleweke kuwa mimi sio kama namtetea Rostam lakini habari zinapokuja humu basi angalau ziwe na ukweli kwa kiasi fulani ili tunapounganisha doti basi tuwe na uhakika na tunachokiongea na kukijadili

Sikweli kuwa Caspian wanachukua madini ya Tanzania kwa sasa labda ni kwa siri kubwa sana na ndio tunaitaka hiyo siri,
Caspian imekuwa registered kama construction Company, kama aliachiwa vifaa na hao jamaa wa Iran inawezekana lakini kwa hizi mining equipment/Machines nyingi huwa wanazipata kwa njia ya mkopo hasa pale wanapopata tender ya kufanya mining, wapo wengi tu (KASSCO) waliopata hizo Machines kwa mikopo baada ya kuonyesha mikataba waliopata kwenye mining

Migodi ya Tanzania ni
Bulyanghulu, Buzwagi,Tulawaka, Northmara-Hii migodi hipo chini ya Barrick ambayo ni kampuni ya waCanada na makao makuu yapo huko Canada, japo wana zonal office kila sehemu zenye migodi, kwa zonal ya Africa makao makuu yapo J,Burg
Geita gold mine-Huu mgodi unamilikiwa na Wamarekani (Anglo-Gold) wakiwa pamoja na waghana (Ashanti)
Resolute-Nzega hu mgodi unamilikiwa na Wa Australia
Mwadui Diamond-Huu mgodi unamilikiwa na Wa-South african na Watanzania

katika hiyo migodi Rostam hayupo humo wala hana share humo, isipokuwa Rostam alipata kazi ya kufanya mining kwenye Baadhi ya Migodi (Resolute, Tulawaka, Diamond-Mwadui, Nmara), na ni ukweli usiopingika kuwa alipata hizo kazi isivyo halali kwani kampuni yake imekuwa registered kama Construction na sio kama Mining Company hivyo hakupaswa kupewa hizo kazi za Mining

Kuhusu Uranium, hapo Rostam hawezi tia Mguu kabisa, huo ni mzigo wa Wamarekani na wao wameshaanza kuumonitor tangu miaka mingi, Rostam anaweza kuingia pale kama mining company (Caspian) na anaweza kupewa hiyo kazi kwa sababu ana uzoefu wa mining lakini sio kwa kuonga wala kwa hila (walioomba kumine hiyo Uranium ni wengi na hata Caspian wameomba)

Point ambayo naweza kukubaliana na wewe ni kuwa, Rostam kama yeye ama kama hao Wairan inawezekana wana stratergies za kuingia (sasa bado hajaingia) kwenye hayo mambo ya Madini na Energy kwa hapa Tanzania, na kwa kuanzia Rostam alihakikisha anaitawala wizara ya nishati na madini, kwa kuweka watu ambao atawahitaji Kalamagi, Ngereja, Kafumu, aliyekuwa mkurugenzi wa Tanesco (Rashid) ,

Kwenye sekta ya energy (Umeme) alichofanya Rostam hakuna asiyekijua

Kuhusu swala la madini, cha kwanza alichokifanya ni kuakikisha anapewa kazi ya kumine kinguvu, nasema kinguvu kwa sababu hao jamaa wenye migodi walikuwa wanasign mikataba isiyokuwa na kichwa wala miguu na ten % kubwa aliyokuwa anapewa Kalamagi ni hofa ya kufanya Mining na hili lilifanyika chini ya Rostam kwa kumine na kampuni ya Construction (Not mining Company) sio siri jamaa (Caspian) walikuwa wanauwezo wa kutengeneza zaidi ya 100m kwa siku kwenye mgodi mmoja na alikuwa anafanya (ana-mine) migodi minne (Diamond-mwadui, Tulawaka, Resolute na NorthMara), kuna uchafu mwingi sana ambao Rostam ameshiriki kuiangamiza hii nchi hasa kwenye mikataba hii tulioingia kwenye sekta ya nishati na madini (mimi huwa naiita wizara ya Rostam, kaimaliza kuanzia nywele mpaka....)

Angalizo
Kwa kutumia hiyo wizara na hao watu wake wizarani, Rostam amefanikiwa kupata eneo maeneo ya Kahama na soon ataanza kumine akiwa ni mmiliki wa Mgodi
 
Hii imekaaje hii, mbona yafanania muvi fulani hivi au novel fulani nilisomaga, this is tooooooooooooooooooo much pliz.

Kwa kweli mambo yanavyoenda nchini humu utadhani ni muvi. Inauma sana sana. Najisikia kulia kwa uchungu. Haki huinua Taifa, dhuluma na rushwa huleta laana katika nchi yetu.
 
"Mbali na Tanzania kuibiwa madini yake ,Marekani ambalo ni Taifa kubwa duniani kwa miaka mingi linapambana na ugaidi duniani , vyanzo vya uhakika vinathibitisha kuwa haliwezi kutimiza jukumu hilo bila kwanza kukata mizizi ya Iran iliyojikita nchini Tanzania ambako inachukua bure mdini ya uranium kupitia kampuni ya Caspian construction Tanzania."


Mdau amekuja na hoja nzuri ila inahitaji backup, CIA bado hawana hizi taarifa? maana wangeshachukua hatua kali, nakumbuka marekani na UN walikuja juu sana Iran ilivyotaka tu kurutubisha madini ya uranium Brazil, hivyo mdau aturidhishe zaidi kuhusu Iran kunufaika na Uranium yetu (maana hili ni zito), nimeamua ku-argue namna hii lakini ni mpambanaji wa vita dhidi ya mafisadi (manyang'au) wanaotuibia rasilimali zetu.
 
Mungu anaanza kushughulika na vilio vya Watanzania maskini.Jambo usilolijuwa ni usiku wa giza. Kagoda, Richmond ni mambo yanayofahamika. Lakini hili jipya gumu. LINAWEZA kuwa linaeleza kiburi cha huyu RA?
This is a serious matter.Sisi hawa hatuwezi kuzijuwa facts. Lakini ukaribu huu usio wa kawaida kwa Rais wetu na sasa kwa Speaker wa bunge, na hata kwa EL anayesemwasemwa kuutafuta Uraisi wa nchi yetu baada ya JK is also an interesting and an amazing story. Is it a mere happen stance or a calculated move?!!! Lakini ni kweli pia anachimba uranium? Anaweza kutuambia anauza wapi? Je ni kweli anauza dhahabu,je anasafirisha mchanga nje?Tumekuwa na wahindi wengi sana toka nyakati za uhuru lakini hatujaona vituko kama vya huyu muirani.KUNA JAMBO.Mazingara haya yanaeleza jambo.
 

Hapo nachanganyikiwa maana naona unajicontradict tena unaposema Sikweli kuwa Caspian wanachukua madini ya Tanzania na wakati huo huo tunamwona huyu Fisadi akiwa na mkono wake kwenye migodi 4 kama ulivyoainisha. Nakushukuru na ninamshukuru sana aliyeleta hii mada kwa kutufungua macho. Huyu RA akitoka nadhani hata wazawa wa CCM waliovaa kutu za kifisadi wataanza kuwa binadamu, maana wote ni kama wanyama tena wale wanaoweza tafuna watoto waliowazaa
 

Jamani jamani nji hiii? Lol!:caked:
 
Nafikiri kuna jambo ambalo halijakaa sawa apa.

Yabidi sote tuelewe namna migodi inavyofanya kaz na nafasi ya Caspian katika migodi ya tanzania.

Shughuli ya uchimbaji madini huhusisha makampuni mengi ambayo ujulikana kama sub-contractors, makampuni haya ufanya kazi za blasting, fuel supply, repair & maintenance of machinery, security, food supply, fuel supply, supply ya explosives, supply ya heavy machinery etc.

Kampuni ya Caspian yenyewe imejkita katika shughuli za heavy duty machinery zinazotumika katika shughuli ya uchimbaji.

Vile vile yabidi wote muelewe ya kuwa migodi ya tanzania ina uwezo mdogo sana wa kurefine dhahabu inayochimbwa apa. Kutokana na ilo dhahabu nying na mchanga upelekwa uko Japan for processing kwa kuwa uko ndiko kuna viwanda vya kisasa na vyenye uwezo mkubwa wa shughuli iyo. Vile vile kuna makampuni machache uko ulaya hasa ujerumani zenye uwezo wa kuprocess dhahabu.

Suala la Uranium, nafikiri wote tunajua kuwa kwa Tanzania hazina kubwa ya Uranium inapatikana uko wilaya ya Bahi, dodoma na maeneo ya mtwara karibu na mto mkuju.

Wawekezaj wa kubwa na wamiliki wa kubwa wa leseni za kuchimba Uranium apa nchini ni kampuni kutoka Australia. Kwa kina zaid fatilia taarifa za stock exchange za Australia. vile vile vyanzo vingine vya habari katika eneo hili la extractive industry ni stock exchange ya Canada. Makampuni ya madini yaliyowekeza nchi mbalimbali pamoja na yale yanayotafit madin uchapisha taarifa zao kila baada ya miez 3 katika masoko aya ya hisa.

Ningependa tuwe na kawaida ya kutembelea majarida kama aya kwa taarifa za kina.
 
Wana JF, naona ndugu yetu Muro ameona kama hii story ni ya kawaida sana kwake wakati sisi wengine tumeungana na Mageuzi 1992 kwenda kunywa maziwa na asali ili kuweza kuisoma tena hii case study, hebu ndugu yetu Muro tueleze zaidi kuhusu huyu RA, inaonekana you're three steps ahead.
Pls napenda kujua pia kuhusu connection ya RA na Kagoda pamoja na kwamba kesi imekwisha.
 
Anayoyasema mtoa hoja yana msingi,kwa kuongezea ni kwamba kwao si Igunga ni Nzega ambako ndiko familia imeishi kwa muda mrefu na kuhusika sana na biashara haramu ya pembe za ndovu Igunga alitokezea kiubunge tu.Na mali zake nyingi anashughulikia kaka yake anaitwa Bahram na ofisi yake iko Mirambo hapo,si rahisi kuona sehemu huyu jamaa ana umiliki wa moja kwa moja na anafanya hivyo ili kikitokea chochote asifilisiwe.Na hao ccm wanaopewa mabilioni na mtu ambaye vyanzo vyake vya hela haviko wazi ndio wanaotakiwa kuchukuliwa hatua,kuna sheria ya fedha za uchaguzi inakataa fedha chafu lakini wenzetu ccm wanampa nafasi mwizi anaiba halafu anawachangia huku wakimpa misifa kem kem ingali wanajua fedha hizo ni chafu mpaka nafasi ya CC wamempa kisa ya huo wizi.Haingii akilini mtu kama huyo mchango wake wa halali haujawahi kuonekana popote,bungeni yupo lakini hajawahi kusikika labda kipindi cha kuapa tu,hashiriki katika lolote la maendeleo lakini wanamkumbatia.Lawama ni kwa viongozi wa juu wa nchi kwani wao ndio wanamsaidia huo uharamia wake.
 

Hapo amepewa kazi ya ku-mine na hizo hela ni malipo ya kazi anazozifanya, kazi yake ni kuchukua mali na kupeleka processing unit na pia kuchukua takataka na kuzipelewa dampo, lakini madini sio yake
 
Katika assassin inayoogopeka ni ile inayopangwa na mtu mmoja mmoja.

Kwani ni ngumu kuichunguza na hata kuigundua kabla ya actual event kutokea. Mara nyingi pale
inapofail (miscalsulation), ndio huwa inajulikana. Hivyo naamini kwa chuki iliyopo kuna siku tutasikia
kichwa ch mtu kimeliwa ghafla.... kwa chuki iliyopo dhidi ya viongozi wetu, next 5yrs kutakua na mambo.

wait and see hii miaka
 

Alikwenda Iran bado kijana mwaka 1975 hivi na alirudi mwaka 1988, baada ya kwisha ile vita ya miaka minane ya Iraq na Iran. Huko Iran alikaa katika mji mmoja unaitwa Godda -- na ndiyo alichukulia jina hilo kuunda kampuni ya KAGODA.

Alipewa mradi wa kutengeneza barabara ya Shekilango kwa jumla ya Sh 75 milioni in earyl 1990s ambayo haikuwa na kiwango.

Natafuta dataz zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…