This is Dowans HQ in Costa Rica - (Pictures)

Taarifa katika Tanzania Daima la tarehe 12 Novemba 2009.

Dowans: Tumeonewa
. Yalikana deni la TRA, yaibebesha mzigo Tanesco
. Serikali yafungua makufuli yake, yasubiri korti

Na Deogratius Temba

UONGOZI wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans, imesema serikali imewaonea kufunga makufuli kwenye milango ya kuingia kwenye mitambo yake kwani haina deni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya TRA kuiagiza kampuni binafsi ya udalali ya Majembe Auction Mart, kuifunga milango ya kampuni hiyo kwa minyororo na makufuli hadi iatakapo lipa deni lake la sh bilioni 9, litokanalo na kutolipa kodi ya mapato ya ndani.

Dowans iliirithi zabuni ya kuzalisha umeme wa megawati 100 kutoka kwa kampuni uliyozua mjadala mzito nchini ya Richmond Development LCC, baada ya kushindwa kuzalisha umeme kama ilivyokubaliana na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) mwaka 2006.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans, Stanley Munai alisema uongozi wao umeshangazwa na kitendo hicho kwani kampuni yake haina deni na serikali.

"Waliofunga walirudi kufungua wenyewe, kilichotokea mtawauliza TRA maana wao ndio waliofunga na kufungua, sisi hutawatambui Majembe, tunaona ni kama porojo tu. Kwa maelezo zaidi suala la jana (juzi) hatulielewi na hilo deni hatulitambui" alisema Munai.

Mkurugenzi huyo alizidi kueleza kuwa TRA ilijichanganya katika suala hilo kwani hawaelewi wanadai deni lipi na deni hilo ni nani mlipaji.

"TRA wanaonekana kujichanganya, kwanza hawaelewi deni hilo mlipaji ni nani, aina ipi ya kodi inayotakiwa kwani kuna deni la VAT la Januari hadi Septemba 2007, hilo ni la Tanesco, halituhusu sisi, kama Tanesco wamekataa kulipa wamkamate yeye, Dowans tupo katikati," alisema Munai.

Akifafanua zaidi alisema wanachokifahamu ni kwamba, katika deni la VAT, awali Tanesco iliwaandikia kuwaeleza kuwa hawalipi kwa sababu wana msamaha wa kodi, lakini baadaye wakawaandikia tena wakiwaeleza kuwa wapo tayari kulipa.

Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano baina ya Dowans na Tanesco, anayelipa ni Tanesco.

"Hawa wanajikanganya, sisi tunaonewa, tunaumizwa tu kwani fahali wawili wanapopigana nyasi zinaumia, sisi Dowans ndiyo nyasi zao," aliongeza.

Akijibu swali juu ya mchakato wa uuzwaji wa mitambo hiyo, Munai, alisema mara baada ya kampuni hiyo kutangaza zabuni ya uuzaji wa mitambo yake, wafanyabiashara wengi walijitokeza kutaka kuinunua, lakini kutokana na zuio la mahakama lililowekwa baada ya Tanesco kuishitaki Dowans, ilishindwa kuiuza.

"Kampuni nyingi za kimatifa zilijitokeza kuitaka mitambo, kama si zuio la mahakama tungekuwa tumeiuza. Mitambo yetu bado ni mizima na ikiwashwa tu ndani ya dakika tano inazalisha umeme wa MW 100," alitamba Munai.

Tanzania Daima ilishuhudia milango ya kuingilia katika eneo la mitambo hiyo iliyopo Ubungo ikiwa imefunguliwa huku waangalizi wake wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Meneja Uzalishaji wa Dowans, ambaye pia ni mwangalizi wa mitambo hiyo, Moses Mwandenga, aliliambia Tanzania Daima katika eneo hilo kuwa, alishuhudia maofisa wa kampuni ya udalali ya Majembe wakifika jana jioni na kufungua makufuli waliyoyafunga kwenye milango ya mitambo hiyo.

Kwa upande wao, TRA walikiri kuifungua milango hiyo muda mfupi baada ya kuifunga, lakini walishikilia msimamo kuwa wanaidai kampuni hiyo deni la sh bilioni 9 na lazima walilipe.

Akizungumza katika mahojiano na Tanzania Daima, mkurugenzi wa Huduma na Elimu TRA, Protas Mmanda alisema hatua ya Dowans kutotambua deni lao ni uongo, kwani wao si wendawazimu kwenda kufunga milango hiyo.

"Kusema kwamba hawalitambui deni hilo ni uongo, sisi si wendawazimu, tumekokotoa deni na kuwaandikia kuwa tunawadai, jana (juzi) walikuja wakasema tuwafungulie maana wana kazi muhimu na wanasubiri hukumu.

Mkataba wa Richmond ulizua mvutano kiasi cha kusababisha Bunge kuunda kamati teule kuchunguza, ikiongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk Harisson Mwakyembe (CCM), ambapo ripo yake ilimlazimu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu.

Pamoja na Lowassa, mawaziri wengine wa awamu ya nne waliojiuzulu ni Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha.
 
Imechukua zaidi ya wiki tatu kuwasha mtambo mmoja tu wa megawati 10 wa IPTL na kwa usumbufu na gharama kubwa. Sasa kama haya yanayosemwa ni kweli, ndani ya dakika tano tu, megawati 100 za Dowans zingekuwa zimeingia kwenye grid ya taifa, kwa gharama nafuu na mgawao ungetoweka kabisa.

Hivi kweli nchi hii inaviongozi thabiti?
 
Nadhani suala si uthabiti wa viongozi bali ni mazingira yanayozunguka suala zima la uwepo wa mitambo ya Dowans na uhusiano wake na kampuni tata ya Richmond. Hapo ndipo tatizo lilipo. Kuruhusu Dowans wazalishe umeme ni sawa na kubariki mbinu za kifisadi zilizoileta Richmond.
 
tk na dowans ni kama chanda na kidole oooppsss pete na ring ooopppss chanda na pete or pete na kidole i .... dont know what I am talking about.
 
Kwani tatizo ni mitambo? Tatizo ni kuwa tukiwalipa hata senti moja tutakuwa tumehalalisha biashara na kampuni ya kitapeli. Wanachodaiana JK, RA na Brigedia watafute njia nyingine ya kulipana. Kama serikali inajali wananchi basi iitaifishe mitambo hiyo mara moja.
 
Kwanza ilitakiwa iwe imetaifishwa na wamiliki kuwekwa rumande......shukuruni kwakuwa mlikula na kikwete. Angekuwa rais ni Dk. Slaa.......dowans angekuwa anaongelea keko.
 
Imechukua zaidi ya wiki tatu kuwasha mtambo mmoja tu wa megawati 10 wa IPTL na kwa usumbufu na gharama kubwa. Sasa kama haya yanayosemwa ni kweli, ndani ya dakika tano tu, megawati 100 za Dowans zingekuwa zimeingia kwenye grid ya taifa, kwa gharama nafuu na mgawao ungetoweka kabisa.

Hivi kweli nchi hii inaviongozi thabiti?

Teh teh teh teh teh zao la ufisadi wewe!
 
Ifike kipindi mjadala kuhusu Dowans ufungwe na tusonge mbele.Tunashindwa kufikiria other viable options,huku tukiendelea kuililia Dowans.Its jus another nu brand day,but old same bulsh!T.Damn.
 
Mitambo yetu bado ni mizima na ikiwashwa tu ndani ya dakika tano inazalisha umeme wa MW 100," alitamba Munai.
Hatudanganyiki ng'o!!
Kwanza tatizo siyo uzima wa mitambo ila ni aina ya mitambo na namna inavyotunzwa baada ya kusimama kufanya kazi. Hii inategemea aina ya fuel inayotumika. Mitambo ya IPTL inatumia HFO ambayo ina sulpher content nyingi hivyo ili itunzwe baada ya kuacha kutumuka lazima iondolewe katika hali yake ya kawaida, kwa hali hiyo kuirudisha kwenye hali yake ya hawali kwa matumizi itachukuwa muda.
Mitambo ya Dowans inatumia gas asilia ambaoyo kuiondoa kwenye uzalishaji unahitaji tu kupuliza na compressed air kuomdoa gas na kubaki kama ilivyo tayari kutumika. Lakini kuiwasha na kuwa synchronised itakuchukua masaa kama siyo siku kadhaa!!
 
Ifike kipindi mjadala kuhusu Dowans ufungwe na tusonge mbele.Tunashindwa kufikiria other viable options,huku tukiendelea kuililia Dowans.Its jus another nu brand day,but old same bulsh!T.Damn.

Nadhani mna miss the point. Mjadala huu hauwezi kufungwa kwa sababu kila siku yanajitokeza mambo mapya ambayo hapo awali tulikuwa hatuyajui. Mimi binafsi, kwa mfano, kwanza sikujua kuwa itachukuwa wiki tatu kuwasha mtambo wa megawati 10 wa IPTL. All along I thought that it will take not more than a week kuwasha mitambo yote ya megawati 100. Pili nilikuwa sikujua kuwa kuiwasha mitambo ya Dowans itachukua si zaidi ya siku moja au mbili kupata megawati zote 100. Sasa jambo kama hili lenye maslahi makubwa kwa nchi haliwezi kupita hivi hivi kimya kimya bila kuliweka jamvini. Sasa kosa langu hapa liko wapi?

Tataizo nililonalo mimi si kwamba nasukumwa na ufisadi bali mimi ndie hasa napingana na ufisadi kwa kuonea uchungu ufujaji wa mali za umma.

Kwa kweli mimi nashindwa kuwaelewa. Inakuwaje viongozi wa nchi wanaamua kutekeleza maamuzi ambayo yanaigharimu nchi zaidi ya mara kumi wakati suluhisho la wepesi na gharama nafuu lipo? Ikiwa mimi ninayetetea maslahi ya nchi naitwa fisadi jee ninyi mnao tetea ubadhirifu mtaitwaje?
 
Ulijua lini na wapi kuwa kuiwasha mitambo ya dowans kutakuchukua dk 5 tu?

Tataizo nililonalo mimi si kwamba nasukumwa na ufisadi bali mimi ndie hasa napingana na ufisadi kwa kuonea uchungu ufujaji wa mali za umma.

Huwezi kupingana ufisadi A kwa kutetea ufisadi B. Yaani unataka kureplace ufisadi A (IPTL) na ufisadi B (Dowans)

Kwa kweli mimi nashindwa kuwaelewa. Inakuwaje viongozi wa nchi wanaamua kutekeleza maamuzi ambayo yanaigharimu nchi zaidi ya mara kumi wakati suluhisho la wepesi na gharama nafuu lipo? Ikiwa mimi ninayetetea maslahi ya nchi naitwa fisadi jee ninyi mnao tetea ubadhirifu mtaitwaje?

Maslahi ya nchi hujayaonyesha bado...
 
Ulijua lini na wapi kuwa kuiwasha mitambo ya dowans kutakuchukua dk 5 tu?

Ukweli ni kuwa nimejua leo hii baada ya kusoma habari hizo kwenye Tanzania Daima.

Huwezi kupingana ufisadi A kwa kutetea ufisadi B. Yaani unataka kureplace ufisadi A (IPTL) na ufisadi B (Dowans)

Sawa. IPTL yenyewe ina ufisadi ndani yake. Kwa hiyo ukichukuwa Dowans au IPTL bado umo humo humo kwenye ufisadi. Similarly mikataba mingi iliyoingiwa nchini ni ya kifisadi. Huwezi kukwepa hilo. Sasa tuchukue fisadi mwenye gharama kubwa au mwenye gharama ndogo?

Maslahi ya nchi hujayaonyesha bado...

Tuache hayo mengine yote ya running costs, fast availability etc. tuchukue slahi moja tu kuwa mpaka sasa nchi bado imo katika mgao wa umeme na athari zake kwa uchumi bado zinaendelea kwa ajili ya uzembe huu tu.
 
tk,
Mkuu pamoja na maelezo yako yote kumbuka scandals walizokuwa nazo hao Dowans..mbali na yetu nyumbani shirika hilo lipo ktk Liquidation, wahusika wenyewe wanagombania share zao leo wewe unataka kutuingiza kichwakichwa!
.
Tatizo lako unatazama mitambo kama vile mitambo hiyo haina mwenyewe na ikifungwa basi matatizo yamekwisha..Jamani hii mitambo ni mali ya watu na watu hao ndio wenye matatizo hivyo mali haiwezi kuhalalishwa ikiwa ina mwenyewe.

Inashangaza sana nikisikia mtu akizungumzia mitambo ya Dowans na kuwaacha Dowans nje as if hatutaingia mkataba, kuwalipa ama mitambo hiyo siii mali ya Dowans ila ipo tu mahala... Cha kuokota sii cha kuiba!.
 
Tuache hayo mengine yote ya running costs, fast availability etc. tuchukue slahi moja tu kuwa mpaka sasa nchi bado imo katika mgao wa umeme na athari zake kwa uchumi bado zinaendelea kwa ajili ya uzembe huu tu.

Tk umeingizwa kwenye mtego wa mafisadi! Dowans siyo solution ya matatizo ya kukosekana kwa umeme bali kukosekana kwa umeme ni mradi wa wakubwa. Upungufu wa umeme ulijulikana zaidi ya mwaka sasa, lakini wakubwa wakasubiri tu ili Dowans or IPTL itumike!
Kwanza kumbuka Dowans walipofikisha mitambo yao connection ilishindikana kwa muda gani, sasa leo wanatudanganya kuwa ni dakika tano unawaelewa?
Five min. is part of ufisadi but not reality kwa sababu mgao huu ulitengenezwa kurahisisha mazingira ya kurudishwa Dowans kama si kelele za watanganyika!
 
Imechukua zaidi ya wiki tatu kuwasha mtambo mmoja tu wa megawati 10 wa IPTL na kwa usumbufu na gharama kubwa. Sasa kama haya yanayosemwa ni kweli, ndani ya dakika tano tu, megawati 100 za Dowans zingekuwa zimeingia kwenye grid ya taifa, kwa gharama nafuu na mgawao ungetoweka kabisa.

Hivi kweli nchi hii inaviongozi thabiti?

Mgao utaisha our incompetent Kikwete atakapoachia ngazi. Raisi aliye na mipango ya kimaendeleo na anayeona mbali hili lingekuwa ni tatizo kubwa kwake ambalo angekuwa ameshalipatia ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom