This is Dowans HQ in Costa Rica - (Pictures)

Kwani UWT wapo?
Hao wanaonyesha makucha kwenye ishu zile za kitoto kitoto ndo utawaona wanavyo komaa mnakumbuka yule mtoto wa sec. kanda ya ziwa aliye mpiga swali EL hawa UWT walimsumbua sana dogo.
 
Haya kina Zitto, Dr. Slaa, Mama Kilango na wengine issue ndio hiyo , sasa ni juu yenu kama wawakilishi wa wananchi issue iwe raised bungeni ili serikali iokoe mabillion na hizo hela zipelekwa kujenga zahanati huku vijijini kwetu ili kina mama wajawazito waweze kuishi wakati wa kujifungua watoto salama.

May God Bless Tanzania![/QUOTE]

And may he wake us up from our deep sleep or more correctly from our COMA.
 
Lipumba keshasema na JK na baraza lake lote la mawaziri wanahusika na Richmond. Kauli ambayo ndiyo inadaiwa kusababisha hoja ya RA kuzuiwa bungeni. Kazi kweli kweli
 
Sasa hivi ndo vitu tunataka hapa JF. Will buy Meremeta Special even for $ 100.

Sasa haka kainzi nako, kameenda masafa marefu sana. Kukamilisha kazi, ni vizuri kakatengeneza report ya Matapeli wa Dowans katika Cheche pia.

Kitu kinachonishangaza, ina maana hawa viongozi wetu huwa hawana uwezo wa ku-establish existence na legality ya companies au ni Mabongolala?


Superman,

Uwezo wanao ila utayari wa kufanya hivyo haupo kwa maslahi ya nani ndio tujiulize
 
I don't know about that..what if kilima hiki kikisawazishwa kilima kingine kinaongezewa urefu? Mwisho itakuwa ni kutoa mfuko wa kushoto kwenda mfuko wa kulia!

Mkuu, ukishaona ufalme huu unapigana dhidi ya ufalme huu, jua mambo yameiva.....katika hili hakuna kilima kitakachoongezwa urefu..vyote vitasawazishwa, Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake dhidi ya watu wake......Ufalme wa Roma na ukubwa wake si ulifika miwsho mkuu?
 
Kaaaaaaaaaazi kweli2

Halafu tunasema TUNA IDARA YA USALAMA WA TAIFA

Labda ni Idara ya Usalama wa Vigogo na wala nchi. Hii inasikitisha na kuchukiza. Hao hao idara ya Usalama badala ya kusaka na kuanika Data za madudu haya. Watataka kumsaka aliayeanika uozo huu. Washindwe na Walegee.
 
Mkuu, ukishaona ufalme huu unapigana dhidi ya ufalme huu, jua mambo yameiva.....katika hili hakuna kilima kitakachoongezwa urefu..vyote vitasawazishwa, Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake dhidi ya watu wake......Ufalme wa Roma na ukubwa wake si ulifika miwsho mkuu?

Kaizer!

Mbona unatuletea historia hapa. Habari za kutoka Costa Rica si ilikuwa mwaka jana na ndiyo ilisaidia kuvunjwa kwa mkataba na Dowans Hewa!!

Labda kama unatukumbusha uzumbukuku wa JMK aka Matonya aliyetoa amri ya kuvunjwa kwa makataba na DOWANS Huku akijua ni usanii!!

Alishauriwa zile mashine zitaifishwe kwani zilikuwa haramu na mmliki hayupo lakini huku akijua anachokifanya ndipo alipoamuru wenyewe waziondoe na amri yake ikapingwa vikali na RA ambae actualy ndie Rais wa TZ in force.

Prove me wrong wahauri wa matonya watampeleka kubaya wamemdanganya kuna kesi mahakamani naomba Ngeleja atuambie hiyo kesi kafungua nani na nani ni mshtakiwa na iko mahakama ipi?

Mpaka leo hii mashine bado ziko Ubungo na hawasemi zipo kwa mkataba upi? Dr. Rashid katishia kutakuwepo na kiza mwezi August na leo tarehe 13 July bado wiki mbili nae hajatutangazia hilo giza linaanza lini kwani kwa mujibu wa taratibu za Tanesco wateja wanapaswa kupewa notisi ya siku 14 kabla ya umeme kukatwa kwa kazi ya kupanga na sio dharura!!

Hivi August 2009 ikifika na hakuna giza nchi nzima Rashid atatuambia nini naomba waandishi mumwombe aitishe press conference bila kuruhusu maswali atueleze what is on vinginevyo si arudie tu kwenye Benki yake ya ACB kuliko kuendeleza ubabaishaji Tanesco.

Is Kikwete realLy serious na huyo swahiba wake Idris Rashid au kwa vile ni wanaswali Masjid Moja ?Kama 3 years plan imemshinda sijashangaa wabunge walimpozomea alipojaribu kutoa dira ya 2033 in the name of Power System Master Plan!! NIMEAMINI KWELI RA ndiye rais behind the scenes!!

Labda tu nikushukuru Kaizer kwa kutukumbusha mambo ya mwaka jana!!! Happy birthday amri ya Kikwete!
 
picha kwa sisi wenye connection ya speed ndogo shida kuziona.....mods pls ziwekeni vizuri....
 
Lipumba keshasema na JK na baraza lake lote la mawaziri wanahusika na Richmond. Kauli ambayo ndiyo inadaiwa kusababisha hoja ya RA kuzuiwa bungeni. Kazi kweli kweli

Mzee niaje si Lipumba huyu huyu unadai anavuta kwa RA?
 
Hongereni sana kwa kazi mlioifanya...na sasa tuwaachie wawakilishi wetu kuimalizia. Kuna vichwa vinahitaji kuanza safari hapa...

Lakini wakuu...CHECHE vipi? Yaani ishu ya Meremeta ndo itabaki siri ya wachache katika Taifa la wote?
Siku zote nilisema na nitaendelea kusema...kazi ya uandishi wa habari ni moja ya kazi muhimu sana katika kuleta mwangaza ndani ya giza nono liitwalo serikali. Sasa ningeomba mtekeleze hili jukumu lenu MUHIMU kwa Taifa kwa kutoa hiyo nakala yenye taafira za Meremeta, na ikiwezekana kwa bure kabisa.
 
Hongereni sana kwa kazi mlioifanya...na sasa tuwaachie wawakilishi wetu kuimalizia. Kuna vichwa vinahitaji kuanza safari hapa...

Lakini wakuu...CHECHE vipi? Yaani ishu ya Meremeta ndo itabaki siri ya wachache katika Taifa la wote?
Siku zote nilisema na nitaendelea kusema...kazi ya uandishi wa habari ni moja ya kazi muhimu sana katika kuleta mwangaza ndani ya giza nono liitwalo serikali. Sasa ningeomba mtekeleze hili jukumu lenu MUHIMU kwa Taifa kwa kutoa hiyo nakala yenye taafira za Meremeta, na ikiwezekana kwa bure kabisa.

duh.. hiyo gharama ya kutoa bure nani analipia?
 
Salamu wakuu,
Nilijulishwa na mtu mmoja kuwa tanazania ilishafanyia marekebisho sheria yetu mojawapo ya makosa ya jinai[ TAKUKURU wakatakiwa kuisimamia] mwaka 2007. Katika sheria hiyo ambayo ni kopi ya ile ya Ufaransa with minor modifications, wao wanatakiwa kumkamata mhalifu aliyefanya makosa hayo ya jinai(likiwemo la wizi wa mali ya umma) wanampeleka mahakamani na kufunguliwa mashitaka. Huko muhusika anatakiwa atoe ushahidi yeye mwenyewe. Mfano;-

Hakimu: Kubwajinga chokoraa unashitakiwa kwa ufujaji wa mali ya umma na kuingia mikataba mibovu iliyokupatia mali ulizonazo sasa.ieleze mahakama hii, mali ulizonazo umezipataje?

Kubwajinga Chokoraa: ....mali hizi nilizonazo nimezipata kutokana na .....

Sasa maelezo yake yanaipa mahakama na UwT kufuatilia je kweli that amount is equivalent to the named sources?

Anayeifahamu sheria hiyoya 2007 naomba atuwekee nakala ya sheria hiyo au sehemu yake tu. And we can see influencial towards kuwashitaki haya majizi.

Bravo enigma, hongera Mmkjj kwa kuvituma vi-inzi vyako vitiifu na vimefanya kazi nzuri sana haina mfano.
 
Kuna baadhi ya issue zinaweza kuandikwa pettition hapa na ikiwezekana wa JF toutoe michango ili wana JF wemyewe tufungue shauri au kesi mahakamanii.

ili tuwe na impact tusiishie tu kwenye kutoa fikra amabzo inaoneneka wahusika hawazifanyi kazi.Sijawai kusikia jumuia ya wahadhiri wa chuo kikuu uDSm au wa vyuo vikuu waikungana kutoa tamko juu ya Richmond. Sijawai kusikia chama cha madaktari wakitoa tamko. Taasisi zenye nguvu na zinazotizamwa na watu kama muongozo wao zikikalia kimya uozo na serikali inazidi kupumua.

Naamini pia inawezekana ndani ya serikali waamuzi wanaogopa kuwajibisha wakosaji na wanaomba issue ya kuwawajibisha itoke nje kama issue ya kumwondoa Lowasa serikali ilivyojiweka pembeni ikaonekana imepikwa na bunge.

Nadahani sasa wana JF tuwe mfano ikiwezekana jopo la wanasheria liundwe kama si kushtaki llipate tafsiri ya mahakama juu uatata wa hizi kampuni feki kufanya kazi na serikali. Naamini wengi tuko tayari kutoa mchango wa hali na mali.
 
sorry,
let's take i am willing to buy the jarida!then how do i pay?and how do i get it?
 
sorry,
let's take i am willing to buy the jarida!then how do i pay?and how do i get it?

we can process credit/bank cards (Visa, MC, Express na Diners); but also Western Union or paypal. U'll get in ur email. Hiyo Western Union au fedha Taslimu ni kwa wale walioko Tanzania tu.
 
we can process credit/bank cards (Visa, MC, Express na Diners); but also Western Union or paypal. U'll get in ur email. Hiyo Western Union au fedha Taslimu ni kwa wale walioko Tanzania tu.

Thanks!
Personally i cn do it,sababu ninajua ugumu wa hiyo kazi na gharama zake pia.Tunasubiri maelekezo tu.

Watu wameshaamua bei ya kununulia?nadhani bado,ikiwa tayari labda utatoa maelekezo yote!

Thank U!i can't wait to buy it
 
Back
Top Bottom