Thinking beyond measures: CCM ni 'mafundi' wa kutengeneza 'matukio' na 'Wapinzani feki'

Hata hili la Maembe ni chezo tu, wapinzani wanaingizwa kingi na kumshabikia kachero wanasahau mambo muhimu.... uchaguzi utafika hawana mtu mwenye sifa ‘wakodishiwe’ Maembe au Marandu kama ilivyokuwa kwa Mamvi.
 
"16. Amid the turmoil and tumult of battle, there may be seeming disorder and yet no real disorder at all; amid confusion and chaos, your array may be without head or tail, yet it will be proof against defeat.

17. Simulated disorder postulates perfect discipline, simulated fear postulates courage; simulated weakness postulates strength." ~ The Art of War, Sun Tzu
 
Yaani wewe ni miongoni mwa watu wachache hapa nchini wenye macho ya kuona mbali.
Furaha ya vyama vya upinzani nchini ni kuona mmomonyoko kwenye chama tawala na bahati mbaya iliyopo kwetu sisi watanzania ni wepesi sana KUSAHAU (sisi hatutunzi kumbukumbu). 2015 sakata la Lowasa na CCM lilileta taharuki nchini hadi EL anaenda upinzani na kupewa kijiti cha kupeperusha bendera ya wapinzani.
Tumesahau figisu alizopata WS na kuondoka CHADEMA na hatimaye EL anakuja kuonekana ni tegemeo la mwisho kwa wapinzani na akapewa majukumu ya kuwapeleka kunako nchi ya ahadi.
Kwanini tu wepesi kusahau hivi? Kwanini kila leo tumekuwa watu wa kufurahia mtikisiko wa CCM badala ya watu kukaa na kutengeneza upinzani imara usiotegemea ugomvi wa CCM. Mwenyekiti wa CHADEMA na viongozi wakuu wa chama hicho wala hawana nia ya kutwaa dola hapa nchini na mkitaka kuamini angalieni mwenendo wao chamani, haitakuja kutokea siku CCM ikatoka madarakani kama ambavyo wengi mnaamini endapo bado mtakuwa wazito katika kutunza kumbukumbu.
Sijawahi kuona chama cha upinzani nchini chenye nia ya kuchukua dola....
Hata Mimi naanza kuamini hivyo.Ulaghai tu!
 
Mwenyezi Mungu amenijalia akili ya kufikiri. Naitumia kufikiri vyema kuhusu 'saga' inayoendelea ndani ya CCM. Nimeamua kufikiri vingine tofauti na kuona kuna mtifuano ndani ya CCM na hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula kuona mwisho wake. CCM ni mafundi na mabingwa wa kutengeneza matukio na wapinzani feki.

Wenye kuangalia vyema, kwa undani na kwa umakini watakubaliana nami kuwa CCM huanzisha songombingo kama lililopo sasa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani. Anzia mwaka 1995 (Mzee Mrema alipohama CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi).....kumbuka 2000 (Prof. Lipumba 'alipotikisa' ).....fuatia 2010 (Dr. Slaa alipomkosesha usingizi Mzee Kikwete) na tena usisahau 2015(Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa mgombea wao)

Fikirini tena na kwa umakini. Matukio yanayoendelea ndani ya CCM si ya bahati mbaya. Ni matukio yanayoratibiwa kwa umakini mkubwa na yenye tija kwa chama hicho. Wakati umma na upinzani ukijihusisha na matukio hayo, CCM huitumia nafasi hiyo kujipanga na kufanya mambo yao bila ya kujadiliwa. Mwisho wa matukio haya huwa na zao la 'wapinzani feki' watakaomwagwa kuelekea upinzani kuteka Majimbo na Kata. Na hata kuwa wagombea wa Urais.

Hakika, CCM ni very intelligent and genius katika kutengeneza matukio na wapinzani feki. Hupoteza maboya sana katika kukaribia uchaguzi mkuu. Kwa hilo wanahitaji pongezi!

Waione: Kiranga , tindo , BAK , Evarist Chahali , Daudi Mchambuzi, manengelo , Pascal Mayalla, hearly na wengineo
Ndiyo ninyi mnaomsifia mtoaji wa sadaka kubwa kanisani kwa mbwembwe nyingi huku mkijua Jana tu kavunja na kupora benki!
 
Huo mzunguko wote Mkubwa wa kutengeneza matukio ni kwaajili ya faida gani?.. uchaguzi??
Kwa hili saga la akina nape sidhani kama ni tukio la kutengeneza,kama mahakama,jeshi la wananchi,polisi,Bunge na tume ya uchaguzi vipo chini Yao kuna haja gani ya kutengeneza matukio?

Kwa katiba hii mbovu kuna haja gani ya kutengeneza sinema Kwa Sisi wenye akili tunajua kabisa haya maccm sikuzote wapo kwajli ya matumbo Yao Tu ndio maana huko ndani hawajatulia kuanzia magu Hadi mawaziri wake!
Nadhani hata goli la mkono nalo itabidi kutumia akili sana ili refa asikuone ikibidi hata VAR
 
Haya mahesabu ya mbali upinzani unashindwaje kuyapiga au hauyajui?
Nilishawahi sema mahali fulani, kuwa kama akili inayotumia CCM kushinda chaguzi ingekuwa inatumika kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo, amini nakwambia tungekuwa ni the best economy in Africa saivi,

CCM inatumia akili nyingi sana na mahesabu ya mbali
 
Hili ni neno zito haswaaa
Umeona kuna kelele zozote toka upinzani za mkazo kabisa angalau kwamba tume iwe huru? Zaidi ya wapinzani hasa wa mitandao kumshabikia kinachoitwa mgogoro ndani ya ccm kuna lipi lingine?

Sasa hivi hata Lisu kawekwa kando
 
Kwa kuweka neno "kivile" maana yake yametengenezwa lakini siyo kwa kiwango kama cha nyuma
Tanzania hakuna upinzani, Nyerere (genius yule) aliwapiga mabeberu changa la macho.

Hilo la CCM kufanya fitna ni kweli hata mwalimu alishalisema kimtindo kwa kusema, "vyama hivi ni vyama vya ruzuku tuu".

Kwa ishu hii ya sasa ya kina Nape na Musiba , nakuomba ufikirie tena. Hii kitu haikutengenezwa kivile kama yale mambo ya nyuma. Watu kweli wanahasira na Magu kwa kuwa kawaharibia mambo yao.
 
Mwenyezi Mungu amenijalia akili ya kufikiri. Naitumia kufikiri vyema kuhusu 'saga' inayoendelea ndani ya CCM. Nimeamua kufikiri vingine tofauti na kuona kuna mtifuano ndani ya CCM na hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula kuona mwisho wake. CCM ni mafundi na mabingwa wa kutengeneza matukio na wapinzani feki.

Wenye kuangalia vyema, kwa undani na kwa umakini watakubaliana nami kuwa CCM huanzisha songombingo kama lililopo sasa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani. Anzia mwaka 1995 (Mzee Mrema alipohama CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi).....kumbuka 2000 (Prof. Lipumba 'alipotikisa' ).....fuatia 2010 (Dr. Slaa alipomkosesha usingizi Mzee Kikwete) na tena usisahau 2015(Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa mgombea wao)

Fikirini tena na kwa umakini. Matukio yanayoendelea ndani ya CCM si ya bahati mbaya. Ni matukio yanayoratibiwa kwa umakini mkubwa na yenye tija kwa chama hicho. Wakati umma na upinzani ukijihusisha na matukio hayo, CCM huitumia nafasi hiyo kujipanga na kufanya mambo yao bila ya kujadiliwa. Mwisho wa matukio haya huwa na zao la 'wapinzani feki' watakaomwagwa kuelekea upinzani kuteka Majimbo na Kata. Na hata kuwa wagombea wa Urais.

Hakika, CCM ni very intelligent and genius katika kutengeneza matukio na wapinzani feki. Hupoteza maboya sana katika kukaribia uchaguzi mkuu. Kwa hilo wanahitaji pongezi!

Waione: Kiranga , tindo , BAK , Evarist Chahali , Daudi Mchambuzi, manengelo , Pascal Mayalla, hearly na wengineo
Asante Boss,umri wewe ni kijana mdogo lkn,akili zako ni za kiutu!
 
Sio kweli, kwa hiyo waliotaka kumpindua Nyerere ilikuwa planned ndani ya Serikali
Una akili kweli aisee. Ina maana Nyerere alikuwa anauhadaa upinzani? Aisee una akili wewe , tena kipindi kile Chadema na ACT makao makuu yalikuwa mikoani

Wewe ni kichwa, genius kweli , unajua vitu
 
Back
Top Bottom