Thinking beyond measures: CCM ni 'mafundi' wa kutengeneza 'matukio' na 'Wapinzani feki'

Mwenyezi Mungu amenijalia akili ya kufikiri. Naitumia kufikiri vyema kuhusu 'saga' inayoendelea ndani ya CCM. Nimeamua kufikiri vingine tofauti na kuona kuna mtifuano ndani ya CCM na hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula kuona mwisho wake. CCM ni mafundi na mabingwa wa kutengeneza matukio na wapinzani feki.

Wenye kuangalia vyema, kwa undani na kwa umakini watakubaliana nami kuwa CCM huanzisha songombingo kama lililopo sasa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani. Anzia mwaka 1995 (Mzee Mrema alipohama CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi).....kumbuka 2000 (Prof. Lipumba 'alipotikisa' ).....fuatia 2010 (Dr. Slaa alipomkosesha usingizi Mzee Kikwete) na tena usisahau 2015(Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa mgombea wao)

Fikirini tena na kwa umakini. Matukio yanayoendelea ndani ya CCM si ya bahati mbaya. Ni matukio yanayoratibiwa kwa umakini mkubwa na yenye tija kwa chama hicho. Wakati umma na upinzani ukijihusisha na matukio hayo, CCM huitumia nafasi hiyo kujipanga na kufanya mambo yao bila ya kujadiliwa. Mwisho wa matukio haya huwa na zao la 'wapinzani feki' watakaomwagwa kuelekea upinzani kuteka Majimbo na Kata. Na hata kuwa wagombea wa Urais.

Hakika, CCM ni very intelligent and genius katika kutengeneza matukio na wapinzani feki. Hupoteza maboya sana katika kukaribia uchaguzi mkuu. Kwa hilo wanahitaji pongezi!

Waione: Kiranga , tindo , BAK , Evarist Chahali , Daudi Mchambuzi, manengelo , Pascal Mayalla, hearly na wengineo
Sikupangi hata kidogo ila kaa ukitambua CCM Kama taasisi nayenyewe inapitia changamoto zake,kuhusu Lowasa ni kweli alitoka CCM nakujiunga CHADEMA lakini siafiki kuwa ulikuwa mpango maalumu kumbuka Kuna watu wengi tu hili swala la Lowasa liliwagarimu uwanachama wao,na kaa ukijua Lowasa ndio amechangia idadi hiyo ya wabunge na madiwani wa ukawa nakuhakikishia angekuwa Dr Slaa mgombea 2015 wasingepata idadi hiyo ya wabunge na madiwani kote nchini na inawezekana hata Mbatia asingekuwepo mbunge was vunjo leo. Kama haitoshi hata kura alizopata Lowasa visiwani Zanzibar asingezipata Dr. Slaa 2015( elewa kuwa Lowasa alimzidi Magufuli kura Zanzibar) nachelea kuamini kuwa Lowasa kwenda upinzani na kurejea CCM ulikuwa mpango mahususi ulioratibiwa na CCM. Kwenye hili Nina ushahidi asilimia zote Kuna mtu wa Karibu sana na Riz 1 alining'ata sikio. Pili hizi danadana za Makamba senior,junior,Membe etc ni hali halisi ilivyo huko CCM kwenye clip ya nape na kinana hakuna hata mmoja ambae angetamani Yale waliokuwa wanajadili yafike masikioni mwa Magufuli kumbuka ameitwa mshamba kwa vielelezo,halafu pia clip ya Nape na Ngeleja imemtaja mtu anaepewa ulinzi na raisi na Nape alisema huyo mtu aliingia na bastola bungeni kinyume KABSA na taratibu na walinzi wote wa bungen(tiss na police) waliufyata wakamuogopa, kwa hi mifano kadhaa nitakuwa mtu wa mwisho kuamini ulichokisema wakili msomi. Tatu tunajua wote jinsi maneno ya Musiba yalivyo fanya damaging kwa watajwa happy juu hili SITAKI kulieleza kirefu rejea maneno ya Musiba kuhusu pembe za ndovu na kuhusu magari ya ccm na mitambo ya kuchapishia magazeti ya ccm na kuhusu Deni la Makamba Nssf. To sum up ccm wasinge kuwa Wana dola wangeshapigana hadharani mchana kweupe kaa ukijua katibu mkuu kawaita wale wazee WAPUMBAVU.. Over
 
Inawezekana japo sio kanuni maana muunganiko wowote wa kibinadamu una hali ya kinafiki na kutoridhiana badhi ya mambo
 
Kipare wanasema HAVACHE, kifipa wanasema SANTE KALESA, kimakonde THANK YOU. Hakika umeunenea moyo wangu vema.

Tatizo ni moja tu, wana JF hujisahaulisha na kukurupukia watu, Sasa hivi wanasema KAZI NA BATA 2020 twende na Membe, na si ajabu wengi wanenayo hayo ni CHADEMA, hivi lile dole la kati la MREMA na MAMVI mmelisahau mara hii.

Hivi itakuaje kesho TUNDU LISU akihamia ACT WAZALENDO akaona gunfua kwamba ZITTO ni one man army akaamua kujiunga na CCM.

Itakuaje Mfalme Mbowe akichoshwa na maisha ya kuigiza akaamua kuunga jitihada za mheshimuwa Magu.

Chini ya jua kila kitu kinawezekana
 
Tatizo ni uelewa wa watz walio wengi. Ingekuwa Members wa Jf ni representative sample ya population ya watz ccm ingepata wakati mgumu sana. Mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watu, ulafi wa wachache na uroho wa madaraka. Evolution of mind italeta jibu ni muda lakini but ccm haitatatawala milele ikitumia mtaji huu wa sasa. Ni real democracy itakayoifanya ccm idumu kama Republics na democrats kule USA na conservatves na labours kule UK. Bila hivo ccm itapotea kama KANU, UNIP NA UPC nk. Na kusahalika. I tell you ni matter of time tu!
Sio kweli, kwa hiyo waliotaka kumpindua Nyerere ilikuwa planned ndani ya Serikali
 
Wengi wasioipenda ccm ni wanye uelewa mkubwa wengi wanaipenda wanafanana sana na waumini ambao kila wanaloambiwa na kuhani wao wanamini linatoka kwa Mungu. Hata wakiambiwa kunyweni sumu wanaweza kunywa.
 
Mwenyezi Mungu amenijalia akili ya kufikiri. Naitumia kufikiri vyema kuhusu 'saga' inayoendelea ndani ya CCM. Nimeamua kufikiri vingine tofauti na kuona kuna mtifuano ndani ya CCM na hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula kuona mwisho wake. CCM ni mafundi na mabingwa wa kutengeneza matukio na wapinzani feki.

Wenye kuangalia vyema, kwa undani na kwa umakini watakubaliana nami kuwa CCM huanzisha songombingo kama lililopo sasa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani. Anzia mwaka 1995 (Mzee Mrema alipohama CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi).....kumbuka 2000 (Prof. Lipumba 'alipotikisa' ).....fuatia 2010 (Dr. Slaa alipomkosesha usingizi Mzee Kikwete) na tena usisahau 2015(Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa mgombea wao)

Fikirini tena na kwa umakini. Matukio yanayoendelea ndani ya CCM si ya bahati mbaya. Ni matukio yanayoratibiwa kwa umakini mkubwa na yenye tija kwa chama hicho. Wakati umma na upinzani ukijihusisha na matukio hayo, CCM huitumia nafasi hiyo kujipanga na kufanya mambo yao bila ya kujadiliwa. Mwisho wa matukio haya huwa na zao la 'wapinzani feki' watakaomwagwa kuelekea upinzani kuteka Majimbo na Kata. Na hata kuwa wagombea wa Urais.

Hakika, CCM ni very intelligent and genius katika kutengeneza matukio na wapinzani feki. Hupoteza maboya sana katika kukaribia uchaguzi mkuu. Kwa hilo wanahitaji pongezi!

Waione: Kiranga , tindo , BAK , Evarist Chahali , Daudi Mchambuzi, manengelo , Pascal Mayalla, hearly na wengineo
Vizuri ndugu yangu kuweka bayana katika uzi. Nimeshasema sana kuhusu hili lakini wengi wanahadaiwa na CCM na movie zao na wanapiga vigelegele. Mmatatizo serious yakitokea CCM utawaona wanaweka vikao haraka. Hizi movie zina miezi zaidi ya sita na hakuna kikao chochote kilichokaa kuyaweka sawa zaidi ya viini macho na Political scintist wetu wa upinzani kina Salary Slip wakiongozwa na kigogo2014 wanaingizwa chakani bila kujua.

Najua wengi watakupinga lakini huo ndiyo ukweli uliouandika hapa leo.
 
Mbona nape amemwita mshamba halafu kinana akasema amechanganyikiwa hiyo nayo ya kudhalilishana ni mbinu?
Kwani hulijui hilo? wao wanafanya mchezo hata kama haujapangwa basi wanachokifanya wanatibuana na wale walitangazwa na upinzani kama wachafu mfano huyo Kinana. Upinzani kwa usahaulifu watampokea. Umesahau Makamba alipotemwa alikaribishwa na kina Zitto. Hapo CCM wanawabadilishia kibao. Ni vigumu kukubali lakini CCM ni wataalamu wa hayo mambo. Wakati wa chama kimoja CCM walipeleka watu nje kusomea propaganda za kisiasa na Mremo ni mmoja wa wataalamu wa Propaganda ambao ccm iliwazawadia upinzani.
 
Mwanzo nilifikifiria Mpinzani wa kweli ni Seif Sharif Hamad, lakini tangu ajiunge na Zitto nimekuwa na mashaka nae..
 
Wengi wasioipenda ccm ni wanye uelewa mkubwa wengi wanaipenda wanafanana sana na waumini ambao kila wanaloambiwa na kuhani wao wanamini linatoka kwa Mungu. Hata wakiambiwa kunyweni sumu wanaweza kunywa.
Sentensi yako ingekua nzuri sana kama ungemalizia na wale wanaoupenda upinzani ni kama watoto wenye ugonjwa uitwao Down syndrome maana wanasahau hata kujua viongozi wao walivyokuwa wapigaji tu kama CCM
 
Mwanzo nilifikifiria Mpinzani wa kweli ni Seif Sharif Hamad, lakini tangu ajiunge na Zitto nimekuwa na mashaka nae..
Huyu nilishamtoa Thamani mwaka 2000 baada ya uchaguzi mkuu aliwapeleka wafuasi wake mstari wa mbele wakiti yeye alikimbilia Ulaya na kuacha wakiuawa na dola.
 
Huyu nilishamtoa Thamani mwaka 2000 baada ya uchaguzi mkuu aliwapeleka wafuasi wake mstari wa mbele wakiti yeye alikimbilia Ulaya na kuacha wakiuawa na dola.
Sio vibaya alivyofanya, kwani kiongozi hatakiwi kuuwawa..
 
Tumeongea humu na tutaongea hakuna upinzani unaotokana na CCM.
Wapigaji wa kweli bado hawajakuwa.
Tunapigiwa kamchezo mchezo.
Alafu tunaaminishwa Ccm inakaribia kufa wakati inazidi imarishwa na hizi Saccos called Upinzani.
Inatia hasira aiseeee

Heshima kwako wakili Petro
Ndiyo ujue watu wengi hasa wafuasi wa upinzani wana kale kaugonjwa kaitwacho down syndrome. Utaamini vipi kama Membe atachaguliwa kuwa nominee wa CCM wakati katiba yao inasema Incumbent ndiye mbeba torch
 
Vizuri ndugu yangu kuweka bayana katika uzi. Nimeshasema sana kuhusu hili lakini wengi wanahadaiwa na CCM na movie zao na wanapiga vigelegele. Mmatatizo serious yakitokea CCM utawaona wanaweka vikao haraka. Hizi movie zina miezi zaidi ya sita na hakuna kikao chochote kilichokaa kuyaweka sawa zaidi ya viini macho na Political scintist wetu wa upinzani kina Salary Slip wakiongozwa na kigogo2014 wanaingizwa chakani bila kujua.

Najua wengi watakupinga lakini huo ndiyo ukweli uliouandika hapa leo.
Mkuu, Uzi huu ni kabla ya misamaha ya akina Nape na Januari
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom