Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Mwenyezi Mungu amenijalia akili ya kufikiri. Naitumia kufikiri vyema kuhusu 'saga' inayoendelea ndani ya CCM. Nimeamua kufikiri vingine tofauti na kuona kuna mtifuano ndani ya CCM na hivyo tuendelee kukaa mkao wa kula kuona mwisho wake. CCM ni mafundi na mabingwa wa kutengeneza matukio na wapinzani feki.
Wenye kuangalia vyema, kwa undani na kwa umakini watakubaliana nami kuwa CCM huanzisha songombingo kama lililopo sasa kila unapokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani. Anzia mwaka 1995 (Mzee Mrema alipohama CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi).....kumbuka 2000 (Prof. Lipumba 'alipotikisa' ).....fuatia 2010 (Dr. Slaa alipomkosesha usingizi Mzee Kikwete) na tena usisahau 2015(Lowassa alipohamia CHADEMA na kuwa mgombea wao)
Fikirini tena na kwa umakini. Matukio yanayoendelea ndani ya CCM si ya bahati mbaya. Ni matukio yanayoratibiwa kwa umakini mkubwa na yenye tija kwa chama hicho. Wakati umma na upinzani ukijihusisha na matukio hayo, CCM huitumia nafasi hiyo kujipanga na kufanya mambo yao bila ya kujadiliwa. Mwisho wa matukio haya huwa na zao la 'wapinzani feki' watakaomwagwa kuelekea upinzani kuteka Majimbo na Kata. Na hata kuwa wagombea wa Urais.
Hakika, CCM ni very intelligent and genius katika kutengeneza matukio na wapinzani feki. Hupoteza maboya sana katika kukaribia uchaguzi mkuu. Kwa hilo wanahitaji pongezi!
Waione: Kiranga , tindo , BAK , Evarist Chahali , Daudi Mchambuzi, manengelo , Pascal Mayalla, hearly na wengineo