Kwanini usielezee huo msingi wa kujibu swali kwa swali kama ulivomuelewa socrates then tukaenda sawa..
Elezea hapo mkuu
Kama nia ni kueleweshana na si kujibizana tu, kuuliza swali katika kujibu swali kunaweza kusaidia kuelewesha kuliko kujibu swali kwa jibu. Kunaweza kumfanya mtu apate jibu mwenyewe kwa kufikiri bila kupewa jibu na mtu mwingine, au, kunaweza kumshirikisha vizuri zaidi mtu katika kufikia jibu, na hata akipewa jibu baadaye, anakuwa ameshiriki katika mchakato wa kufikia jibu hilo.
Nitakupa mfano. Mfano huu ni kwa mujibu wa habari za vitabu vya dini, unatoka katika vitabu vya dini, lakini mimi nauchukulia kifalsafa tu.
Inaelezwa Yesu aliulizwa na watu, tumlipe kodi Kaizari au tusimlipe?
Hakujibu mlipeni, au msimlipe moja kwa moja.
Aliomba apewe sarafu. Akapewa. Akaionesha sarafu kwa watu. Akawauliza, sarafu hii ina picha ya nani?
Ukiwa unabeza habari za kujibu swali kwa swali, mpaka hapo Yesu anakuwa kashindwa. Maana kajibu swali kwa swali.
Watu wakamjibu. Wakasema, sarafu ina picha ya Kaizari.
Basi Yesu akawaambia, sawa, kama sarafu ni ya Kaizari/ ina picha ya Kaizari, mpeni Kaizari vya Kaizari.
Yesu angeweza kujibu kwamba mlipeni kodi Kaizari bika kuwauliza watu sarafu ina picha ya nani.
Lakini jibu hilo la moja kwa moja lisingeweza kuelimisha vizuri kuhusu sababu. Kwa nini Kaizari alipwe kodi.
Kwa Yesu kuanza kujibu swali kwa swali, aliwafikirisha waliomuuliza swali kuhusu jambo muhimu kabisa kwenye hilo swali.
Msingi huu wa kujibu swali kwa swali haukuanza kwa Yesu. Ukisoma habari alizoandika Plato kumhusu Socrates utaina kwamba Socrates alikuwa hapendi kutoa jibu la haraka yeye kwa maswali aliyoulizwa, bali alioenda kumuongiza yule aliyeuliza swali kwa utitiri wa maswali ambayo yangeweza kumfanya aliyeukiza seali mwenyewe aoate jibu, au hata akioewa jibu, awe kashiriki katika mchakato wa kulifikia hilo jibu kwa makubaliano, si kwa nsingi wa kuoewa jibu tu.
Ukielewa maandishi ya zamani kama ya Plato alivyiandika kuhusu Socrates na Galileo Galileo katika "Dialogues" utaona kwamba kuna msingi mzuri sana wa kujibu swali kwa swali.
Sent using
Jamii Forums mobile app