The Truth Behind The Scenes: Lowassa na Chadema!

kwa hiyo umesema JK unamjua vizuri na umefanya naye kazi, taabu sana. Ukasema nchi hii penda usipende inaendeshwa na Lowasa ili hali sisi tunajua rais ni huyo rafiki yako. Sasa mimi najiuliza wewe unamfahamuje JK? kwamba ni under performer au nini? imenichanganya sana
 
Nchi inaongozwa na Kikwete ila akitoka ndio kijiti atapewa Lowassa
 

Mshikachuma usifikiri ccm na usalama wa taifa hawajui nini kinaendela,na usifikiri hawajui kuwa watanzania wameamka kutoka usingizini,basi kwa kuwa wanaelewa hilo tambua kuna mambo yanawekwa sawa kwa gharama yoyote ile kwa kushiriana na intelligence za baadhi ya mataifa rafiki,kumbuka pale juu niliongelea neno "nguvu"sidhani kama ulinielewa vizuri
 
Usiwaze sana mwanakwetu EDWARD hana kufikiri ila akiamua kusema leo hii jinsi bosi wake alivyo leta richmond na mambo kina 6 na mawembe waliyo mfanyia basi hata wewe utampatia kura yako tusubiri wakati ukuta ata yazungumza yote hayo.
 
Lowassa anaongoza serikali? what a joke!!!
 

Nivea
Hebu niambie nini kilitokea kwa hawa vijana?
 
Siwezi ku-ignore ila wacha kwanza niyaweke kabatini haya.
 
Hili siyo jukwaa la kampeni,kama ni kampeni za chooni kazifanyieni hukoooo Monduli,LWS kitu gani katika nchi hii hachoki kujibaraguza tulishamsahau kitambo msiturudishe nyuma kukumbuka maovu ya Richmond,mbaya zaidi kufukuza watumishi kazi majukwaani,hivi kaharibia maisha watu wangapi na leo anataka kujisafisha kwao,Hatutaki hata kusikia jina lake mbali na yeye mwenyewe.
 
TT, hapo nilipoBOLD ndiyo nilikuelewa....si ulisema Lowassa ananguvu kuliko mtu yeyote? Pia inakuwaje hao hao ccm
ambao hawamtaki Lowassa wafanye kazi ya kumpigania kwa gharama yoyote ile ili aingie ikulu? muongozo tafadhali
 
kwahiyo matamshi ya mhe.Mnyika kuwa tumefika hapa kwasababu ya udhaifu wa KIKWETE ni ukweli mtupu basi??!iweje yeye ni ndiye aliyekabidhiwa dhamana na watanzania alafu mtu mwingine ambaye amechafuka na kupoteza imani kwa watanzania walio wengi amburuze,Kwanini kikwete akubali kuburuzwa na Lowassa kama hoja inaukweli?
kwanini Kikwete anyamazie vyombo kama TISS/UWT na rasilimali zake kutumika kwa lengo la kuwadhuru viongozi wa watu?
 
watanzania wote waelewe kwa sasa hivi Lowassa ndiye Rais ajaye na wasiwasi wake upo zaidi kwa chadema kuliko kambi tofauti ndani ya ccm


hapa hapa Jf tumeambiwa 2015 Lowassa atagombea kupitia Chadema.... sasa mnatuchanganya
 
Taraaaaaaaaa!!! directed by Wakwere. kama ni kweli basi mwisho wa hii picha nadhani movie itatoka kwenye TV na kuwafata watizamaji kumalizia ng'we yao....
 

Ukipitia vizuri thread za kisiasa, utasoma kwamba Tiss ina makundi kadhaa ambayo huwajibika kwa watu kadhaa pia. Wapo wanaomtii mtawala aliyepo na kufanya kile wanachoagizwa na wapo wasiopenda yale mabaya yanayotendwa na wakubwa. Hawa wa kundi la pili ndio hao ambao hutuvujishia habari zingali za moto toka jikoni ili tujiandae kwa lolote. Nadhani unanielewa
 


well said
 
Mimi kiingereza sikijui,
Lakini hapo kwenye RED unasema kwamba Rais Kikwete ni DHAIFU sio??
Orait........sasa nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…