Hamna haja ya kuwa na ratiba, ila ni bora na muhimu sana kuhakikisha mnaifanya walau mara moja kwa wiki. Kwa wana ndoa ambao bado wachanga, inafaa kila siku walau mara moja kwa miaka miwili ya kwanza. Mnapiga breki pale mke anakua kwenye siku zake.
Lakini kadiri miaka inavyokwenda ndivyo mnapunguza hadi mnaishia kwenye moja au mbili tu kwa wiki, hiyo ni wakati mpo kwenye zaidi ya miaka kumi ndani ya ndoa.
Cha msingi, mwanaume usije kumnyima mkeo wakati anajiskia, akitaja tu hapo usisubiri chochote, muonyeshe upo tayari. Jaribu kula vitu vinavyokupa nguvu, haswa mbegu za mlonge na maboga, pia tikiti maji, binafsi vimenisaidia sana miaka mingi kwa mke wangu.