Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,015
- 12,294
The Sinicization Of Religions In China
Huu ni utaratibu maalumu unaofanywa na nchi ya China kuzifanya dini zote za ng'ambo ziendane na utamaduni na mfumo mzima wa maisha wa jamii ya kichina.
Utaratibu huu umeanza karne na karne na umekuwa ukipitia maboresho kadhaa mpaka sasa chini ya China ya ukomunisti.
Utaratibu huu unafanyika maalumu kwa ajili ya kulinda tamaduni na mfumo mzima wa maisha ya wachina dhidi ya muingiliano wa tamaduni na taratibu za jamii za nje.
Utendaji kazi wa sera au utaratibu huu katika karne hii na miaka hii ya karibuni umeshuhudiwa ukitenda dhidi ya dini za ng'ambo kama Uislam na Ukristo.
Mtindo na tamaduni nyingi za waislam wa sehemu mbalimbali duniani ni nadra kutendeka China bali waislam wa China wameweza kujitofautisha kwa kiasi kikubwa na waislam wa sehemu kubwa duniani katika mambo mbalimbali.
Serikali ya ukomunisti iliyopo China mara kwa mara imekuwa ikisisitiza ni muhimu waislam wa China kufuata na kutii sheria na maagizo ya serikali katika utimizaji wa imani yao kwa kuendana na kuheshimu misingi na tamaduni za China ya usoshalisti.
Pia katika dini ya Ukristo utaratibu huu wa sanicization umeshuhudiwa dhidi ya madhehebu ya kiprotestanti na ukatoliki.
Kwa pamoja waumini, viongozi na wafuasi wa imani ya kikristo wamekuwa wakisisitizwa kufuata na kuheshimu taratibu na sheria za China zinazo wataka viongozi wakuu wa madhehebu kuteuliwa na serikali ya kikomunisti katika uongozi wa makanisa yao.
Mara nyingi kanisa katoliki limekuwa likiingia migogoro kadha wa kadha na serikali ya China kuhusu huu utaratibu unaoipa mamlaka serikali ya China kuteua na kuchagua makasisi viongozi wa ngazi mbalimbali za kanisa kinyume na taratibu za kanisa katoliki linalomtaka papa kufanya hivyo.
Pia serikali ya China imekuwa ikisisitiza umuhimu wa ukristo kwa madhehebu yote kuishi na kuheshimu taratibu na tamaduni za jamii ya kichina katika kujenga umoja wa kitaifa.
Sinicization ilianzishwa kale kwa misingi ya kulinda taratibu na tamaduni za China, kadiri muda unavyozidi songa utaratibu huu katika dini unazidi kutiliwa mkazo ili kuepusha na kupunguza ushawishi wa dini za ng'ambo kitamaduni ndani ya jamii za wachina.