Kinyambiss
JF-Expert Member
- Dec 2, 2007
- 1,374
- 76
Hata ukuu wa mkoa ni kumpendelea tu tena upendeleo wa wazi na hasa mkoa wenyewe ukiwa kama dar = chaos ... maana idadi ya watu ni zaidi ya mara tatu ya wale wanaomshinda kuwaongoza sasa, kwa hiyo inafaa kumuonea huruma na kumpumzisha kabisa, au kama anapenda sana madaraka awe mshauri wa mgambo... tosha
-----------
Tuna kazi ya kutafuta kazi
jamani naomba tuelewe kuwa CCM ni chaka la watu waliochoka kimawazo na wenye kuendekeza unafiki, fitina na majunguuu.... ujinga mtupu tunapowajadili hawa wazee wanaotoa mawazoo yaliyochokaaa...Mkuu Sekenke... si wewe peke yako mwenye dukuduku. Hii nayo ni thread aliyoanzaisha BabaDesi
Naungana na wajum,be wanaosema kuwa ni ujinga kujadili suala hili sasa. kwa kuwa utaratibu uko wazi kabisa. Si dhambi kuspeculate nani atamchallenge JK, au nani hataki awe challenged. Incompetency iliyooneshwa kwenye hii miaka mitano lazima ifungue milango.
Nikukumbushe tu kuwa John Shibuda alishatangaza nia yake ya kugombea hiyo nafasi ya urais mwaka 2010.
Hawa unaowasikia wanampinga Karume ,maana Karume anatayarishwa kuchukua nafasi ya Kikwete ,ikiwa Kikwete ataamua kuachia ngazi ,ila wapo katika kutoa ishara kuwa hakuna sababu ya Kikwete kuachia ngazi, kama unakumbuka Mwinyi alipomaliza kuwa Raisi wa Zanzibar alipewa wa Tanzania na ndio hivyo hivyo ,kama unavyofahamu taratibu za CCM ,ili kujificha na ile dhana kuwa Zanzibar haipewi uongozi wa Tanzania ,ndio inaonekana kuwa Karume apishwe katika kipindi hiki au hata Kikwete akimaliza miaka kumi yake kama akiipata apewe Karume.Ni utaratibu wanaosema wamejipangia au wameamua kuurudisha ili kudumisha muungano.
Hiyo ndiyo CCM tunayoifahamu baadhi yetu. Mgombea mwingine ni 2015.
Hata kama hiyo ndiyo CCM mnayoifahamu, sasa kwa nini zinaanza kutumika nguvu kuhalalisha mgombea wa 2010? Kulikoni?
Wampe Mheshimiwa Magufuli awafundishe kazi! Kikwetele wao hana jipya na hafai kwa lolote!
Gembe,
Mkuu kwani Uongo?
Nani CCM anaweza kuwa bora kuliko Kikwete naomba sababu au vigezo vya mtu huyo ktk Uongozi bora..
Gembe,
Mkuu kwani Uongo?
Nani CCM anaweza kuwa bora kuliko Kikwete naomba sababu au vigezo vya mtu huyo ktk Uongozi bora..
...Mkapa, aliwataka wana-CCM kuzingatia mambo matano muhimu katika kumchagua mgombea anayefaa ambayo ni pamoja na kujiuliza kama mgombea anakubalika na pande zote za muungano na katika ushindani wa vyama vingi, kuzingatia kuwa wapiga kura wengi ni vijana na wanataka nini toka kwa viongozi wao, kama mgombea amechipuka na kukulia kwenye chama na wachague mtu anayefahamu vizuri chama cha CCM.
Alisema chini ya uongozi wa kiongozi huyo ni lazima mapinduzi na muungano uimarike na Tanzania hiindele kuwa nchi yenye umoja. Aidha, kiongozi huyo asiwe na chuki, hasira
Aliwakumbusha wanachama wasichague mtu kwa kumpenda bali achaguliwe kwa sifa na kutoa mfano wa bangili kwamba hata ikiwa nzuri, lakini inapobana kwenye mkono haifai.
Rais Mkapa alisema kamwe mataifa ya nje hayawezi kuwachagulia Watanzania Rais na kuwataka wananchi wazingatie maslahi ya nchi.
Tujitahidi kutafuta mgombea mwadilifu kadri iwezekanavyo, mwenye dosari chache na asiyetumia madaraka yake vibaya, alisisitiza.
Aidha, aliwataka wanachama hao kukumbuka kuwa kabla ya kupiga kura wapunguze kujifikiria wao binafsi na kundi lao katika chama.
Aliwakumbusha kuwa Rais atakayechaguliwa atakuwa ni Amiri Jeshi Mkuu hivyo anahitaji kuheshimiwa na mtu mwenye msimamo thabiti asiyeyumbishwa.
Aliongeza kuwa hatutaki rais anayeyumbishwa, anayeanza kwa kuchechemea na anayefaa kwa wakati huu tu bali na ujao.