Mtu anaweza kusema JF haina nafasi ya aina yeyote katika kuathiri uchaguzi au maamuzi makubwa ya kisiasa Tz, sawa hayo ni mawazo yake maana wengine tunaweza fikiri kuwa wana JF ni kundi tu dogo sana la watu ambao wengi wao wako ughaibuni na hawana nafasi yeyote nyeti Serikalini au Vyamani au kwamba hawana kabisa ushawishi wowote wa nguvu katika vyama vinavyoteua hayo majina na hata kwa Wananchi-wapiga kura ingawa ni kweli kuwa Wananchi wengi hawana uwezo wa kuwa mtandaoni hapa kama sisi.
Binafsi ninakubali kuwa JF kama vilivyo vyombo vyovyote vya habari ina nafasi nzuri tu ya kuathiri kama si fikra basi matendo (au vyote) ya Watanzania wengi wakiwamo walio katika uongozi wa juu wa hivyo vyama vya sisasa. Na si lazima waje hapa kwa majina yao na kusema mimi fulani nawashukuru sana kwa mchango wenu ambao nimeufanyia kazi katika mada au jambo fulani ili kuthibitisha hili.
Wengine wanafikiri kuwa hapa JF kuna watu wapo kwa kutumwa kupata news na au kupima joto la 'reactions' za wananchi siwezi kulipinga hilo wala hata siwezi kupinga kuwa huenda JF imeanzishwa ili kukusanya habari na mikakati ya kulisaidia Taifa letu ili liweze kustawi na kumuendeleza Mtanzania.
Hakika, sijali kujua chanzo au kiini cha mwanzilishi au waanzilishi wa JF wala kutaka kuona eti watu wote hapa tunakubaliana na kuwa na mwelekeo mmoja katika kila jambo hasa suala nyeti kama nani anafaa (au nani achaguliwe) kuwa Rais.
Cha msingi kwangu ni kuwa watu wanapata nafsi ya kutoa maoni yao ambayo ni ya busara (au hata ya kuchekesha tu) yenye uelekeo wa kumuendeleza Mtanzania na tupo tunaofaidika na michango ya hapa iwe ni kupinga, kuunga mkono au kurekebisha au kutoa tetesi juu ya jambo fulani lenye maslahi ya Taifa.
Back to the topic:
Binafsi nadhani kuwa pengine ni vyema kuunda mkakati kwanza hata kabla ya kufikiria kuwa ni nani tunaona anafaa kutuongoza . Kwani ni kupitia njia ya mkakati wenye ufanisi ambapo hata nafasi ya kidemokrasia itapatikana katika kumchambua mtu yeyote kwa makini na katika wigo mkubwa hata nje ya JF.
Kuna thread humu zilikuwa zinagusia uwekaji huo wa mikakati mfano aliyoianzisha Mwanakijiji yenye jina:
CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!- Bofya hapa
(
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/20430-ccm-kumeguka-ni-muhimu-kwa-taifa.html) na hata ile yangu yenye kichwa cha habari:-
2009 kisiasa- Bofya hapa
(
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19251-2009-kisiasa.html)
Watu wamechangia juu ya mkakati ambayo kupitia njia hizo kweli Wananchi wanaweza kuanza kusema nani anawafaa. Na pia tujue kuwa hata hao viongozi wa vyama msifikiri kuwa huwa wanakurupuka tu na kuweka jina la mtu huwa wanapima uelekeo wa Wajumbe wa Mikutano yao na Wananchi kwa ujumla!