The Road to The 2014 FIFA World Cup - Brazil

The Road to The 2014 FIFA World Cup - Brazil

Status
Not open for further replies.
Timu ninazotarajia zitapita toka mzunguko wa kwanza toka kila kundi bila kujali mshindi wa kila group

Group A - Brazil na Croatia
Group B- Spain na Holland
Group C- Greece na Ivory Coast*
Group D- England na Italy*
Group E- France na Switzerland
Group F- Argentina, Nigeria
Group G- Germany na Ghana*
Group H- Belgium na South Korea

* - nategemea patakuwa na mabadiliko kiasi, baadhi ya timu zinazotarajiwa(wengi) kupita kiurahisi toka katika makundi hayo zitapata wakati mgumu kama sio kuvuka mzunguko wa makundi.
Sitashangaa kuona baadhi ya timu zenye majina hasa toka ulaya zikachemsha, mfano Ureno ikimkosa Cristiano,ambaye nategemea atachemsha (sababu ya majeruhi na uchovu wa ligi) itachemsha(Ureno). Sababu ya kuichagua Ghana mbele ya Ureno ni kuwa hawa jamaa wanaonekana kutoshiba au kulewa kwa sifa za mafanikio katika kombe la dunia tofauti na Waafrika wengine mfano Ivory Coast, Cameroon. Nategemea Ghana bado kuwa njaa walioionyesha ktk kombe la dunia lililopita, isitoshe watataka kufuta makosa waliyofanya Afrika Kusini. Kundi C nadhani lipo very open Ivory Coast kama watakaza makalio wanaweza kupita, tatizo nililonalo la hawa jamaa ni kama vile wanashiba sifa za kuwa nchi yenye wachezaji maarufu na mashuhuri kuliko nchi nyingine za Afrika kwa sasa. Hizi sifa ndo zinazotuponza Waafrika wengi, tunaanza kuringa kabla hatujafika mbali. Huu ndo mwaka wao wa mwisho kuonyesha uzuri wao katika level ya kimataifa ama sivyo watakuwa ndo wale wa "Enzi zetu, Enzi zetu". Sidhani Columbia kama watafanya makubwa toka katika kundi C kama inavyotarajiwa na wengi, wanaweza kuchemsha kama mwaka 1994 ambao walitarajiwa kuvuka mzunguko wa kwanza wakaishia wa mwisho katika kundi lao, cha ajabu hata Marekani iliwazidi mwaka ule. Greece wanaweza kushangaza dunia kama walivyofanya katika Euro 2004. Kundi D England na Italy watakuwa na kazi nzito kupita toka katika kundi hili, itabidi wakaze makalio, wasitarajie kupata miteremko ama sivyo mmoja wao atarudi kujiandaa na EPL na Serie A mapema.

Ni muonekano wangu, usinihukumu. Njoo na wako.
 
Tournament ya mechi 7 tuu kumbuka! Lazima wachezaji wanaoenda wawe na uzoeefu wa kutosha
 
_74706388_74692828.jpg


Mtoa hoja tuambie nani kapendelewa hapa?
Goalkeepers: Julio Cesar (Toronto FC, on loan from QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro).
Defenders: Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (AS Roma), Maxwell, Thiago Silva (both Paris St-Germain), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Henrique (Napoli).
Midfielders: Paulinho (Tottenham Hotspur), Ramires (Chelsea), Willian, Oscar (both Chelsea), Hernanes (Inter Milan), Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City).
Forwards: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Jo (Atletico Mineiro), Hulk (Zenit St Petersburg).
Standby: Diego Cavalieri (Fluminese) Miranda, Filipe Luis (both Atletico Madrid), Rafinha (Bayern Munich), Lucas Leiva (Liverpool), Lucas Moura (Paris St-Germain), Alan Kardec (Sao Paulo)
 
Wadau zimebaki siku si chini ya kumi na moja ili michuano ya kombe la dunia ipate kuanza,michuano hiyo inaanza huku kukiwa na utata mkubwa.Wenyeji wamekuwa wakipinga serekali kutumia hela nyingi na kitendo hiko ndio kimeibua vuruga kubwa.
Hakuna taifa lolote ambalo limekataa kupeleka timu yake nnchini humo au kujaribu kuishauri serekali ya nnchi hiyo cha kufanya.
Endapo ghasia hizi zingekuwa zinatokea uarabuni au kwenye nnch zinaongozwa kwa sheria za kislamu hadi muda huu tungekuwa tumewasikia mataifa ya ulaya na marekani yakiwa na shaka ya hali za usalama na milipuko ikihofiwa lakini kwa kuwa brazili wanaona ni sawa tu.Ila mi natilia shaka endapo vurugU azitadhibitiwa mapema nnchi zinazopeleka timu zao ziwe makini pia kwa raia wao wowote wataokuwa nnchini humo kushudia michuano hiyo.
je wewe mwana jf ni timu gani tokea africa inayoshiriki fainaili hizi utaishangilia itapokuwa nchini brazili
 
Mm nitawashangilia watakaokuwa wakikamatwa kwenye michepuko.
 
chanzo ni gazeti la champions ukurasa wa11. Jiji la campinas ambapo ureno na nigeria vitajifua kwa ajili ya kombe la dunia limekumbwa na ugonjwa wa homa ya dengue. Watu 32,384 wameathiriwa katika jiji hilo lililopo umbali wa saa zima kufika sao paulo na watu wa3 wameripotiwa kufa. Lakini wafanyakaz wameanza kuwaangamiza mbu wanaoeneza ungonjwa huo kabla ya timu za ureno na nigeria kuwasili. Polen jaman jiji la campinas. Naipenda nigeria.
 
huu ni ubaguz ulio wazi,unawezaje kumuacha negredo alie2pia goli kumi na k2 kwenye club yake af unamchukua torres mwenye goli 4 sijui 5 kwenye club yake,kama ndo hvyo what is the meaning of displaying ur good performance towards world cup,huyu del bosque toka zamani alikua na kikos chake mfukoni spain ilikua chama langu ila sasa natamka rasmi mimi ni team england.
Spain wazuri wengi,staa wengine wapo wengi la liga watu hawawajui,sio staa mpk sky news au bbc imtangaze
 
Laiti kukitokea mechi kati ya Marekani na Irani au Marekani na Korea ya Kaskazini
 
Inawezekana kuna mtanzania alienda nao huko campinas.
 
Fredericko.. Del bosque is the coach and he decide.... Lets wait and see...


mbona mkuu analia bure? wako na wenzake.

Torres,
David Villa,
Diego Costa,

Del Bosque; mojawapo ya makocha wanaoheshimika zaidi Spain nzima. Kocha amemchagua Torres kulingana na yale anayoweza kufanya.
Kuhusu Negledo kuachwa; angalia hata Man city wamekuwa wanamtumia Dzeko mechi nyingi sana kuliko Negredo; hasa katika mzunguko wa 2.

 
Spain wazuri wengi,staa wengine wapo wengi la liga watu hawawajui,sio staa mpk sky news au bbc imtangaze


kila timu ina utamaduni wake; tena TIMU YA TAIFA inapaswa kuwa na stability. Del Bosque anataka timu iliyozoeana; Torres amezoea kucheza na hao wenzake kwa muda mrefu kuliko NEGREDO. kocha anaweza pia kufanya makosa; lakini lazima afanye maamuzi yake kama kocha si kufuata maoni ya mashabiki tu. Coaches are hired to be fired.🙂
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom