Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,060
- 22,755
Mwisho napende nisema baadhi ya viongozi wa chadema ni makini lakini chama chao sio makini na wakigundua hivyo watafanya kama alivyofanya kafulila.
Yale yale ! Mara ooh, CCM ni safi ila viongozi ndiyo mafisadi au Kikwete poa ila serikali yake ndiyo goigoi ! Watanzania lini mtafunguka macho na kutambua kuwa bila watu hakuna chama ? Lini mtaerevuka kiasi cha kutambua kuwa Raisi ndiye anaunda serikali na kuisimamia ? Sokomoko, kama unakubali kuwa viongozi wa Chadema ni makini kwa nini chama wanachokiongoza kisiwe makini vile vile ? Naomba usituletee visingizio vya Makamba eti CCM si chama cha kifisadi huku kinaongozwa na mafisadi waliokubuhu. Unatenganisha vipi chama na watu wake ?