The Man behind 2PAC's Death

The Man behind 2PAC's Death

Mbeky

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
672
Reaction score
520
Habari wadau...naleta kwenu conspiracy theory hii ili tuijidali naamini humu JF kuna wajuzi zaidi....who is really behind the death of 2PAC. Je ni Natorious B.I.G au Suge Knight...??
Wakati nakua na kuanza fatilia muziki wa Marekani miaka ya 90 nilitokea kuwa shabiki wa 2pac lakini kwa kuwa tulikua tumelishwa story za mtaani kuwa B.I.G. na kundi lake(bad boys record) ndio walimua 2PAC basi nilimchukia Natorious pamoja na Puff Dady (Pdidy).
Na niliamini hivyo pasipo shaka lolote. Nafikiri wengi wetu tuliangukia kundi hili..
Ila baada ya kuelemika na kuanza kuhoji mambo na kufatilia mambo nilifanikiwa kupata matazamo tofauti kuhusu swala hili.
Hii ilianzia baada ya kuona movie ya maisha ya Natorious B.I.G ambayo imeonesha ni jinsi B.I.G alivyokua hausiki kabisa na kifo cha 2PAC na jinsi walivyokua marafiki hapo zamani.
Kilichokuja kunichanganya zaidi ni documentary moja ya "untold truth behind 2PAC death " kwenye hii documentary imempotray SUGE KNIGHT kama the man behind 2PAC's death.
Kwamba kipindi kile cha bifu lilozuka kati ya West Coast Rapers (mfn kina 2pac na death row, snoop dog etc ) na East Coast( wakina B
I G, bad boys na wasanii wengine wanaotoka New York) inasemekana Suge Knight kwa kupitia Death Row alipiga hela sana mauzo yaliongezeka kadri bifu lilipozidi kuwa kubwa.
Ila inasemekana mbeleeni kulipungua maelewano kati yake sugar knight na 2pac na ndipo 2pac akatangaza nia ya kujitoa Death Row inasemekana hiki kitendo kilimkera Suge knight ndio akafanya mpango wa kumuua 2pac katika mpango kabambe uliosukwa na baadhi ya corrupted corps ili ionekane kambi ya B.I.G ndio inahusika.
Cha kushangaza mpaka leo muuaji wa hawa watu wawili (2PAC na Natorious B.I.G) hajawai kupatikana pamoja na uwezo na ukubwa wa F.B.I katika kufanya upelelezi.
Je kuna mwenye infos zaidi kuhusu kifo cha nguli huyu wa Hiphop duniani
 
Mmoja kati ya Suge na Big anahusika na mauaji ya Pac, japo kwa kiasi kikubwa tuhuma zinaenda kwa Big small
 
Mmoja kati ya Suge na Big anahusika na mauaji ya Pac, japo kwa kiasi kikubwa tuhuma zinaenda kwa Big small

Kwa nini lawama zimuangukia BIG pekee
 
Behind it Kuna CIA pia. Ili kumaliza bifu lililokuwa linapamba moto Kati ya east na west. Both were killed by CIA. Period! But the question is " why the 7th day theory apply to the death of 2pac? Refer the kiluminati album!! Think big
 
US government hates rap wameweza kumfukua sadam hussein,osama na most notoriuos people in the world wakashindwa kumjua aliyemuua BIG na Pac! Na always marapper wazuri ndo huwa wanakufa! Rest in peace my nigga Pac n B.I.G for ever!
 
Ndio hapo na mi huwa haingii akilini wameweza kumpata Osama tena nje ya nchi yao afu eti wameshindwa kumpata muuwaji wa Pac na BIG ambaye yumo humo humo marekani..
Ushawai jiuliza angekua ameuliwa mweupe mwenzao ka Sir Elton John (bwabwa) au actor Anold wangeacha iishe juu juu tu hivi
 
hii kweli intelligence room...kama ni suge knight alicheza huo mchezo basi alijua kucheza na majira kufanya tukio coz kwa nnavyokumbuka kifo cha tupac kimetokea wakati bifu ndo limepamba moto na kundi la east cost team baada ya tupac kuachia ngoma ya HIT EM UP aliomchana BIG na kundi lote la east coast.
ila maswai ya kujiuliza kama BIG aliuawa kwa malipizi ya kifo ch tupac, kwa nini mauaji yasiendelee kwa kulipiza pia katika kikundi cha west cost? mauaji yaliisha baada ya kuondoka kwa hawa marapper wa juu tu.

na kama suge knight alimuua tupac kwa madai ya kutaka kujitoa death row, kwa nini BIG aliuawa kwa madai ya kisasi cha kifo cha tupac?

kingine ambacho ni kigumu zaidi..kushindwa kupatikana kwa wauaji kwa nchi kama marekani hapo ndo inanipa hisia kuwai ni consipiracy theory.
 
Unajua suge knight alianza bifu na snoop ambayo imedumu mpaka leo baada ya snoop kunukuliwa na vyombo vya habari akisema "pac was not murdered by bad boys....he was killed by his friend..." alipoulizwa who was behind that bila kupindisha maneno alisema ni "Suge Knight "
Mama ake pac mwenyewe mpaka kesho huwa anabisha sio BIG aliyehusika kwenye kumuua mwanae
 
kama ni suge ndiyo aliyemuua PAC vipi kuhusu BIG nani aliyehusika na kifo chake ? kuna uwezekano mkubwa kukawa na mkono wa serikali ya USA
 
sababu binadamu hatuna uwezo wa kutabiri siku zetu za mauti kama alivyofanya 2pac.

Pac alikua msomi na muumini wa filosofi za Makavel..mi simuelewi vizuri huyu jamaa ila inasemekana aliwai sijui kufa akarudi au something like alitabili kifo chake..so labda pengine Pac uwezo wa kutabili kifo chake aliupata kwenye mafundisho ya huyu mwanafilosofia.
Ila bado kuna kundi la watu wanaoamini Pac bado yupo hai mmoja wao ni mtoto wa kiume wa Will smith kwa hiyo sio wewe tu...mi mwenyewe na wish hiwe hivyo aissee
 
pac alikua msomi na muumini wa filosofi za makavel..mi simuelewi vizuri huyu jamaa ila inasemekana aliwai sijui kufa akarudi au something like alitabili kifo chake..so labda pengine pac uwezo wa kutabili kifo chake aliupata kwenye mafundisho ya huyu mwanafilosofia.
Ila bado kuna kundi la watu wanaoamini pac bado yupo hai mmoja wao ni mtoto wa kiume wa will smith kwa hiyo sio wewe tu...mi mwenyewe na wish hiwe hivyo aissee
ni kweli 2pac alisoma vitabu vya makavel, na makaveli hakutabiri kifo chake ila alitengeneza kifo fake ili kuwakwepa maadui wake na alipohakikisha maadui wote wakubwa wamefariki ndio akajiyokeza tena kwenye uso wa jamii after 14 years..pili
 
Kwa kweli swala la kifo cha PAC linamambo mengi ambayo ya pazia...binafsi hata mimi na maswali mengi ambayo nahitaji kupewa majibu na nilipoleta mjadala huu nilikua na matarajio ungepata wachangiaji wengi ili tubadilishane taarifa na tunayoyajua kuhusu utata huu..
 
kwa kweli swala la kifo cha pac linamambo mengi ambayo ya pazia...binafsi hata mimi na maswali mengi ambayo nahitaji kupewa majibu na nilipoleta mjadala huu nilikua na matarajio ungepata wachangiaji wengi ili tubadilishane taarifa na tunayoyajua kuhusu utata huu..
kikubwa anko ni kwamba wasanii wengi wa marekani wanajua pac alipo na nimesikia nyimbo mbili mmoja wa eminem anasema pac moved to cuba.
 
kifo cha pac ni kama watu wapo njia panda awajui kwa kuelekea maana haijulikani kama kweli aliuwawa au laa
 
kikubwa anko ni kwamba wasanii wengi wa marekani wanajua pac alipo na nimesikia nyimbo mbili mmoja wa eminem anasema pac moved to cuba.

Na kwa nini anafanya hivi..ka nikufata misingi ya Makavel imelezwa hapa Makavel alifake kifo ili awakimbie maadaui zake
 
Back
Top Bottom