The KGB, NATO and Post-Independence Africa (1960s-1980s): Vita Mpya vya Maslahi ya Wazungu (USSR-USA-EU) ndani ya bara la Afrika punde baada ya uhuru

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
The KGB, NATO and Post-Independence Africa (1960s-1980s): Vita Mpya vya Maslahi ya Wazungu (USSR-USA-EU) ndani ya bara la Afrika punde baada ya uhuru.

KGBbbnb (1).jpg


Ninakushauri uanze kwa kusoma thread hii kwanza: Patrice Lumumba University of Russia: Ngome kuu ya majasusi wa KGB ya kufunza itikadi za Ujamaa kwa wanafunzi kutoka nchi masikini za Dunia ya Tatu

2209607_IMG_20191111_092657_816.jpg


Katika kipindi cha baada ya vita ya pili ya dunia, idara ya ujasusi ya Soviet Union (KGB) ililazimika kufanya kazi kwenye bara la Afrika ambalo lilikuwa haijulikani kabisa hadi wakati huo (The Dark Continent). Kuna siku moja niliwahi kuuliza swali hili humu JF kwamba FOR GREAT THINKERS: Is Africa still a dark continent or a crucial partner in sustaining a better world?

Mnamo miaka ya 1950, idara hiyo ya ujasusi ya Soviet ilikuwa ina maslahi barani Afrika na maslahi hayo yalipatikana kwa urahisi na ilikuwa ni juu ya kupatikana kwa habari (Intelligence Gathering) kuhusu mipango na nia za nchi za Magharibi (NATO).

Wakati huo kambi nyingi sana za majeshi ya anga pamoja na yale ya majini ya Mataifa wanachama wa NATO zilikuwa katika bara la Afrika. Maslahi yao katika bara hili hayakuwa tu katika misingi na hoja za kimkakati. Hapana. Bali Afrika ilikuwa tajiri katika rasilimali za chakula na madini, na hifadhi yake kubwa ya malighafi muhimu kwa viwanda vya kisasa, kama vile uranium, cobalt, wolfram, shaba, nikeli, mafuta, na madini mengine mengi tu.

Kundi la kwanza la washauri wa masuala ya kijeshi kutoka USSR (Soviet Military Advisors) wakiwa kazini nchini Angola.
USSRnbhgfrt.png


Je! Ni kwa hatua gani na kwa kiwango kipi nchi za NATO zilitaka kutumia bara la Afrika katika mapambano yao na Umoja wa Soviet (USSR)? Idara hiyo ya ujasusi (KGB) ilikuwa ikitafuta majibu ya swali hilo. Kukidhi malengo haya awali, KGB ilitumia uwezeo wake iliyokuwa nayo katika mataifa ya Magharibi.

Katika Afrika yenyewe, ofisi za KGB zilikuwa za kiwango cha wastani katika nchi chache. Kulikuwa na ofisi ndogo tu huko Misri na Ethiopia, na mwisho wa miaka ya 1950s, ofisi zingine ndogo zilikuwa zimefunguliwa pia huko Sudani, Ghana, na Guinea. Idara za usalama za USSR zilianza kazi zake halisi barani Afrika kuanzia mwaka 1960, wakati mchakato wa ukombozi wa bara la Afrika ulipoanza kupata nguvu.

Kundi la Pili la washauri wa masuala ya kijeshi kutoka USSR (Soviet Military Advisors) wakiwa kazini nchini Angola.
image.jpg


Mataifa 17 huru yalionekana mara moja kwenye ramani ya bara la Afrika. Umoja wa Mataifa ulitangaza 1960 kuwa ni Mwaka wa bara Afrika. Ndani ya idara za usalama za USSR iliundwa ofisi maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala ya bara la Afrika. Majukumu ya ofisi hiyo yanaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

(1) Kuwezesha kufutwa kwa haraka kwa chembechembe na mabaki ya mfumo wa kikoloni.

(2)Kusaidia harakati za ukombozi wa kitaifa (National Liberation Movements) katika makoloni yaliyobaki.

(3)Kufuatilia sera za wakoloni wa zamani na wa sasa: Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, na Ureno;

(4)Kuchambua sera za USA kuhusiana na bara la Afrika;

(5)Kuchunguza hali ya kiasias katika kila nchi ya Kiafrika - je itabaki katika mzunguko wa mfumo wa zamani (orbit of the old system) au kuchukua njia mpya?

(6)Kupata marafiki na washirika miongoni mwa Waafrika.

Afisa muandamizi wa zamani ndani ya idara ya usalama ya KGB ambaye sasa ni Rais wa Russia ndugu Vladmir Putin akiwa na Rais wa Uganda ndugu Yoweri Kaguta Museveni.
MKMKJUHYHY.jpg


Kwa hiyo yaliongezewa masuala ya kiusalama kwa makoloni ya kidiplomasia ya Soviet, balozi, pamoja na taasisi zingine za Soviet. Miaka ya 1960s ilithibitisha kuwa ni miaka ya mwanzo wa changamoto kwa wote yaaani mataifa machanga ya Kiafrika na idara za usalama za USSR.

Nchi za Kiafrika ambazo ndio kwaaaanza zilikuwa zimeachiliwa huru ghafla zilikutana na mzozo mkali na watawala wao wa zamani, ambao walitaka kuendelea kudumisha nafasi zao za kisiasa na kiuchumi katika maeneo yao ya zamani.

Katika visa kadhaa hii ilisababisha kuibuka kwa hali ya mizozo, kama vile katika nchi ya Kongo iliyotawaliwa na Ubelgiji. Mapinduzi ya kijeshi ambayo yalitokea kutokana na baadhi ya nchi huru za afrika kuingiliwa na mataifa ya Magharibi pamoja na idara zao za usalama, ikiambatana na migogoro ya watu wa ndani kwa ndani, mizozo ya kikabila, na vita vya wenyewe kwa wenyewe, vikawa kama vile ni jambo la kawaida tu.

image1.jpg


Katika kila hali yenye utata, taarifa kutoka katika idara za usalama za Soviet zilikuwa zinahitajika ili kufahamu ni nani aliyeingia madarakani, ni makundi gani ya waasi yaliyofanya mapinduzi, na kwa muelekeo upi walikuwa wanakusudia kuiongoza nchi.

Kujibu maswali haya yote haikuwa kazi rahisi. Wakati mwingine washiriki katika harakati hizo za mapinduzi ya kijeshi hawakujua.

Ofisi za upelelezi kwa nchi za kiafrika, ambazo zilikuwa ndio kwaaanza zimeundwa tu na kwa kawaida zilijaa maafisa wachanga katika taaluma, hazikuweza kutoa majibu mazito na kamili kwa maswali haya yote magumu.

Lakini kwa uaminifu kabisa walipeleka habari moja kwa moja kutoka maeneo ya matukio, taarifa ambazo zilikuwa muhimu kwa Moscow kwa vile ilisaidia uongozi kuona na kutathmini matukio kwa uwazi zaidi.

USSRasasddd.png


Kuanzia siku ya kwanza kuanza kufanya kazi katika nchi za Afrika, maafisa wa USSR walikutana na shida kubwa sana. Kazi kukosa mpangilio kila siku, ukosefu wa mazingira masafi na hali ngumu ya maisha, na usumbufu katika usambazaji wa chakula.

Ilikuwa ngumu kutarajia kufanya kazi vizuri na hali ya kuishi katika mataifa yaliyopo nyuma kimaendeleo ambayo jana tu yalikuwa chini ya nira za wakoloni (under the colonizers’ yoke).

Lakini pia ugumu wa kufikia maelewano na Waafrika uliibuka kuwa ni mshangao kwa maafisa wa usalama wa KGB. Waafrika walikuwa na fikra pamoja na tabia tofauti. Ushamba na matumaini ya kupata msaada kwa haraka pamoja na hasira na kutoaminiana.

USSRSSDFDFGG.jpg


Nyakati za kikoloni zilikuwa zimewajenga kutowaamini wazungu, na kuwadanganya maafisa wazungu wa KGB ilichukuliwa kuwa ni jambo la kishujaa sana.

Haya yote na tabia za Kiafrika baada ya ukoloni yalibidi yashindwe na maafisa USSR tena kwa kijituma na kufanya kazi kwa bidii. Kupotea kwa makoloni kulidhoofisha mataifa ya Magharibi. Hiyo ilisaidia maslahi ya USSR na kuimarisha misimamo yake ya sera za kigeni.

Kwa hivyo, USSR uliunga mkono mapigano ya mataifa ya Afrika katika kupata uhuru wao wa kisiasa na kiuchumi.

USSRqaqassde.jpg


USA na nchi za kikoloni, kwa upande wao, zilitaka kuzuia mchakato huu kwa njia yoyote ile iwezekanayo, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa idara zao za usalama. Kwa njia hiyo, bara la Afrika liligeuka kuwa uwanja mpya wa mzozo wa kiitikadi na kisiasa kwa pande kuu hizo mbili.

Na kwa hivyo mapigano ya watu wa Afrika kujikomboa kutoka katika makucha ya kikoloniwao yakageuka kuwa kitu cha uhasama baina ya mataifa makuu mawili yenye nguvu kubwa. Hiyo ndiyo ilikuwa mantiki halisi ya enzi ya Vita Baridi.

ITAENDELEA NEXT TIME. NIPO BUSY KIDOGO HUKU DAR.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Mkapa.jpg


PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
 
Mkuu, Infantry Soldier, hii mada ni tamu sana kwa wakubwa kama mimi ila kwa watoto waliozaliwa juzi hawawezi kuielewa. Siasa hizi za Vita baridi.

Wazungu baada ya kumaliza kupigana katika ardhi yao, sasa wakaamua kuhamishia vita katika dunia ya tatu (afrika ikiwa ni moja wapo)

National Liberation Front of Algeria (FLN)

National Movement for the Liberation of Angola (MPLA)

African Party of Independence for Guinea and the Cabo Verde Islands (PAIG)

Mozambique Liberation Front (Frelimo)

People’s Organization for Southwest Africa (SWAPO)
 
Vp kuhusu Angola na Savimbi mkuu? Angola haikuwa uwanja wa mapambano?@
Hapo Angola Moto uliwaka kweli kweli tena kwa miaka mingi kuanzia mwaka 1975 mpaka kumalizika Vita baridi mwanzoni mwa miaka ya 1990.(MPLA,CUBA,USSR) Vs (UNITA,SOUTH AFRICA,USA).

Savimbi aliivuruga sana Angola ila mwisho wake ulikuwa mbaya.
 
Back
Top Bottom